Serikali iboreshe sheria ya Ndoa za Kikristu ili ziruhusu talaka kuepusha mauaji na fumanizi

Yaani Dini in mapungufu Hadi waumini wanaomba serekali ndo iboreshe maandiko yake
Kwasababu serikali ndiyo inatoa vyeti/hati na kuzisajili!
Hivyo iweke taratibu nyepesi za kufuta
 
Zingine ni ibada za shetani!..Kuna matukio ya wanawake wanaombwa tigo na waume zao! Hapo Kuna ibada au uchuro!!
Ibada gani Mme kumtindua mkewe hivyo!
Je, kwenye kitabu imeandikwa kuwa hiyo ruhusa!?
 
Kwasababu serikali ndiyo inatoa vyeti/hati na kuzisajili!
Hivyo iweke taratibu nyepesi za kufuta
Ndo za kikristo ni mtego mwanamke anaweza kukufichia makucha yake had utakapo muoa ndo aanze kukudhihirishia tabia yake chafu kwakua anajua huwez kumuacha na dini hairuhusu kuachana had kifo kiwatenganishe Sasa kwanini kondoo wa bwana asiamue kumtanguliza mwenza wake kuzimu kwakua din imeshindwa kumsaidia kuachana kwa amani
 
FYI serikali haijatunga sheria ya ndoa ya Kikristo, sheria ya ndoa yas Kikristo inatokana na Maandiko matakatifu na Kanisa. Serikali haizuii talaka wala mitala, wanaoingia kwenye ndoa ndio wanatakiwa ku-declare wanafunga ndoa ya namna gsani: Kiislamu, Kikristo au Kimila.

Vv
 
Uneona eeh
 
Cheti cha ndoa anatoa nani kama si serikali
 
Cheti cha ndoa anatoa nani kama Si serikali
Cheti cha ndoa kina sehemu kinauliza aaina ya ndoa (Kimila, Kikristo, Kiislamu, Kiserikali) na wahusika wanajaza aina ya ndoa kutokana na hizo zilizoainishwa. Katika hizo aina, kila moja ina sheria zake na iwapo kuna mgogoro baina yao sheria ya ndoa ambayo wahusika waliijaza ndio itazingatiwa.

Vv
 
Watu hawana Elimu ya sheria ya ndoa hata wewe mtoa mada hujui kitu kuhusu sheria ya ndoa, ndoa zote iwe imefungwa kikristo, kiuslam na kimila zinasimamiwa na sheria ya nchi ya ndoa hivyo sheria ya talaka pia hutolewa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya nchi na sio ya kanisa.

Hakuna sheria ya kikristo wala ya kiislam, kama ndoa ipo kwenye migogoro isiyorekebishika hata baada ya kusuluhishwa kwa taratibu za kidini au kimila, shauri hupelekwa mahakamani na pande moja au zote kwajili ya talaka, waislam huwanatoa talaka kwa utaraibu wao ila kama mmoja akaona haki haijafuatwa anaweza kwenda mahakani.

Ni vema kujua ndoa zote husimamiwa na serekali kwa mujibu wa sheria dini na taasisi zingine ni wakala tu wa serekali wa kufunga ndoa, ndiyo maana hati zote za ndoa hutoka serekalini, pale kwenye hati yako ya ndoa utaona hati ya ndoa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
"Hadi kifo kitutenganishe"
Mtu anaamua kumtanguliza mwenzie ili kutimiza maandiko.
dmkali hii ni sababu ndoa za kikristo watu wanatangulizana. Ulichosema ni kweli lakini kama mtu hajui utaratibu wa kuvunja ndoa za kikristo atadhani unalalamika tu. Jiulize kwanini Ben Paul alibadilisha dini ilikukimbia ndoa.
 
Unakuta huyo ni Social worker au Hakimu kwenye kesi yako ya ndoa. Utajuta.
 
Hilo ni suala la taratibu za Dini husika Wala sio la kiserikali.

Kama wanataka kutalikiana wanaweza. Hakuna wa kuwazuia. Mfano nikitaka kutoa talaka kwa mwenza Wang siwezi kukosa sababu hata ndoa iwe ya namna gani..! Dini sio sababu ya kufa na tai shingoni.
 
Mtu Kama uliolewa mwenyewe.kwa hiari yako na muuaji ulitarajia Nini?

Kuoa na kuolewa mtu anatakiwa ashirikishe Mungu

Sasa Kama ulikurupuka tu ukalipata uaji .Hilo chaguo lako unavuna ulichopanda
Yah nimekuelewa, vijana wa sasa wanakurupuka sana, mwishowe anajivalisha mkenge unakuta anaingia kwenye ukoo wa wasio olewa alafu yakisha mkuta anaishia kulia na kusaga meno,turudi kama zamani tutumie mabalozi kupata wachumba wazuri
 
Serikali haiwezi kuingilia mambo ya kidini zaidi na kikatiba wananchi wamepewa uhuru wa kuchagua dini wazitakazo ikiweno kufunga ndoa katika dini wazipendazo.
Cheti unachopewa cha ndoa ni cha serikali siyo dini.

Kimsingi Kuna utata mkubwa kwenye issue ya ndoa za kikristo. Naunga mkono kwamba dini za kikristo na serikali ziangalie upya Sheria hii.

Kwa vile ule ni mkataba, mmoja Kama hataki kuendelea na mkataba wa mahusiano uvunjwe kwa masharti rafiki.
 
Hakika
 
Serikali inahusika nini na masuala ya ndoa ya kikristo?
 
Serikali na mambo ya dini wapi na wapi kama hauelewi huko njo katika uislam unaweza kuoa Leo 4 kesho ukawaacha wote ukaoa wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali haiwezi kuingilia mambo ya kidini zaidi na kikatiba wananchi wamepewa uhuru wa kuchagua dini wazitakazo ikiweno kufunga ndoa katika dini wazipendazo.
Lakini cheti cha ndo kinachotolewa kanisani na kusainiwa na pande zote ni cha serikali. Basi irahisishe kwamba wao wabaki na dini zao lakini kiserikali ndo ivunjwe na cheti cha ndoa kilichotolewa na mfungisha ndoa kwa niaba ya serikali kifutwe na kirudishwe serikalini. Nao ndoa iwe imeisha kiserikali.
 
Wazo zuri sana
 
Mtoa mada!

Sio kwamba serikali haiwezi kuvunja ndoa za kikristo, inaweza kufanya hivyo. Kumbuka madhehebu mengi ya kikristo yanatumia cheti cha serikali wakati wa kufunga ndoa.

Hivyo, mahakama zina uwezo na zimekuwa zikitenganisha ndoa nyingi tu za kikristo kwa kuruhusu wenza wapeane talaka.

Shida inakuja kuwa makanisa mengi ya kikristo hasa haya mainstream, hata kama ndoa ikitenganishwa na mahakama wao bado wanaendelea kuchukulia kuwa hiyo ndoa bado ipo.

Matokeo yake ni kwamba wahusika wote wawili mtatengwa na hamtaruhusiwa kufunga tena ndoa ndani ya kanisa husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…