Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

... na hapa DSM tuna Mmarekani mwenye miaka 61 amebainika kuwa na Corona pia”
Wamwangalie sana huyu Babu/Bibi vinginevyo Tanzania itakuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, Kati na Kusini kufungua chapter mpya ya Coronavirus manake hivi virusi vina chuki sana na vizee!! Yaani utadhani vinawaonea gere hawa wazee kwa kuendelea kudunda duniani wakati wameshazeeka! Wakati c wenyewe binadamu tunaona poa tu ku-compete Oxygen na hivi vizee lakini Corona wanaumia kweli kweli vikiona jamaa wanaunda tu!!
 
Nchi ya Chad, ambayo bado haijapata mgonjwa au mshukiwa wa virusi vya Corona, imefunga mipaka yake yote na viwanja vya ndege ikiwa ni sehemu ya juhudi kuhakikisha virusi hivyo vinadhibitiwa.
NB:Idriss Deby ni raisi diktekta wa kweli sio wale uchwara..maana alipindua Chad toka 1990 mpaka leo raisi ...lakini anafunga mipaka ya nchi yake ili watu anaowaongoza wasife...Hapa kwetu viongozi hawana huruma na watu wanaowaongoza ...
hawajui kuna biashara zetu zita dorora,
Ajira hayatoi still bado wanaachilia mipaka. Nahisi yenyewe yana sehemu ya kukimbilia kikinuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kuona na hutawahi kuona Logic kwa vile wewe ni sehemu ya huu mfumo dhalimu ambao upo tayari kuweka rehani maisha ya Watz 50m + kwa kisingizio Cha Utalii...!

Hivi kwa kumbukumbu zako katika hatua alizotangaza Majaliwa ay Ummi umesikia ZUIO LOLOTE LA NDEGE ZA ABIRIA KUINGIA NA KUTOKA NJE YA TANZANIA? Hii ni hatua muhimu Sana lakini mazwazwa ya CCM yamekaa kimya....!!!
Ndege zilizozuiwa ni za ATCL tu zisiende China zikaongeza ugonjwa ambao tayari unapungua kwa kasi huko. Wachina ni rafiki zetu viongozi wetu wamesema hatuwezi kuwazuia wasiingie nchini ila wabongo wasiende China. Tunahitaji watalii kwa gharama yoyote!
 
Sijaskia hata serikali ikitangaza kuajiri madaktari na wapo wengi tu mtaani na MD zao tunataka madaktari wakuu waache kutibu wagonjwa wengine wahusike kupima Corona tuu na huduma nyingine wagonjwa wazidi kuugua
 
Serikali ajirini madaktari wa taadhali tunajua hatuna madaktari wakutosha sio tu kutoa elimu kwa matangazo kuwe na physical doctors kila mahali km ilivyokuwa usajili wa NIDA
 
Inaanzaga hivi hivi mwisho inafikia elfu 10.
Mungu asimamie upande wetu na jinsi tulivyokuwa hohe hahe mwee familia ya watu sita vyumba viwili nyumba ina vyumba sita wakaaji 16 choo kimoja bafu moja nawaza mbali mwenzenu sijui tuanze kupungua mjini kurudi vijijini manake kule hakuna mbanano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo alie safiri sweden na ufaransa ni meneja wa diamond salam sk...
 
Mngewatenga wagonja karantini air port na mngefunga mipaka kusingekuwa na uzembe huu wa watu kufatiliwa mitaani ona gharama sasa za kufatiliana.
 
Kwanza nichukue nafasi hii Kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru binaadamu na tatizo hili,

Pili, naishauri serikali iwe makini na namna inavyotoa taarifa za idadi ya wagonjwa wa corona, sababu naona ni kama wamecopy tu mfumo unaotumika maeneo mengi.

Kwa mfano, kutuambia tu eti Tanzania kuna wagonjwa wangapi wa corona haitoshi kusaidia mapambano juu ya tatizo hili, nahisi kuna kipengele cha msingi kinakosekana.

Ituambie, ni waginjwa wangapi wameambukizwa ugonjwa huo wakiwa Tanzania. Ama sivyo naona ni kama inatengeneza hofu isiyo ya lazima.

Nawasilisha.
 
Mficha magonjwa, mauti humwumbua. Ni kweli kwamba wale wanaotajwa na serikali tu ndo idadi halisi? Hawa wanaotajwa tajwa kwingine mbona kwenye list hawawekwi?
Screenshot_20200319-160059.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Diamond na wenzake wote wawekwe chini ya uangalizi.

Radio Free Africa kupitia kipindi cha Mambomambo, muda huu wamedai Meneja wa Diamond alikiri kuwa na huo ugonjwa wa Corona.
 
Back
Top Bottom