Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Jumapili iliyopita nilifuatilia ibada ya kitume kutoka Kanisa la Askofu Gamanywa kupitia Shallom tv na ilitangazwa kuwa muhubiri wa misa ile ni raia wa Marekani ambaye ameingia nchini Ijumaa iliyopita.

Hii maana yake ni kuwa mmarekani huyu hakukaa katika karantini ili kujiridhisha kabla hajakutanishwa na umati wa watu..... Aliingia nchini siku ya Ijumaa na kuhudumu siku ya Jumapili.

Nimekumbuka hili baada ya kusikia hotuba ya PM Majaliwa kuhusu wagonjwa wawili wapya raia wa Marekani na Ujerumani

Nawatakia Kwaresma yenye baraka!
 
Imefika wakati sasa serikali ifunge mipika, idhibiti usafiri wa ndani ikiwemo daladala na mwendokasi, iboreshe maeneo ya upimaji na caranteen, iombe msaada wa makampuni na watu binafsi katika kusaidia wananchi wa hali ya chini kupata vifaa vya kujikinga, watoe elimu kupitia kampeni maalumu hasa vijijini,

wananchi waelekezwe kujiwekea akiba ya chakula majumbani, waone namna ya kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula na viosheo, waimize wananchi kupunguza kwenda mjini bila sababu, wawashauri wabeba abiria kuepuka kuwabeba raia wa kigeni bila taadhari,

watoe utambulisho maalumu kwa wageni waliopo nchini ambao wamepimwa na kubainika wapo safe ili wanapopita maeneo mbalimbali waweze kupatiwa huduma nk
 
Waliosomaaa utabirii wajanaaa leooo tumeanza kusikia MH majaliwa Idadi inaongezekaaa

Mengineyo MENGI yanakuja mola tusitiri
 
ndio maana jana waliamua kufunga shule, kuna uwezekano idadi ikazidi
 
Kaka hadi 2018 tulikuwa na wagonjwa 1.6M wenye maambukizi ya VVU. Hatujui baadhi yao wata respond vipi wakipata hii corona. Italy wanakufa zaidi wazee. Huku Tanzania tuna hilo kundi. Je, bado unadhani unatukuzwa zaidi?

Kwelii kabsaa mkuu Ni ugonjwa hatari ila wameukuza sana. Sijui Nini Kiko nyuma ya pazia.
 
Ulimsikia Gwajima lakini? Alisema ugonjwa wa Corona haupo Tanzania na hajakamatwa kwa uchochezi mpaka sasa.

Nenda wewe utangaze uone shughuli yake. Hii nchi inawaogopa sana watu maarufu.
 
Back
Top Bottom