Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Serikali: Idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imeongezeka na kufikia Sita(6)

Tuna ongezeko la wagonjwa wawili ambao wamethibitika kuwa na Corona Tanzania, mmoja kutoka Zanzibar yeye ni Mjerumani ana miaka 24 na tayari yupo kwenye uangalizi, na hapa DSM tuna Mmarekani mwenye miaka 61 amebainika kuwa na Corona pi
HAWA NI WAGENI WAMEKUJA KWETU. KARIBUNI SANA WAGENI.

MGENI NJOO, MWENYEJI A............ NISAIDIENI KUMALIZIA
 
Hujui kitu. Nchi nyingi kama Iran imeambukizwa na Mchina. Italy Mchina.
Marekani ni Mmarekani aliyekuwa China ila hakuletwa na serikali
China iliweza kuthibiti kusambaa zaidi kwa Corona kwa kuufunga mji wa Wuhan kuingilika na kutoka kwa watu.

Ndiyo maana hatusikii wachina kusambaza kwenye mataifa mengine tofauti na hao wapuuzi waliofuata raia wao Wuhan ili wanaonekane wanajali sana watu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kama Ghana,Cameroon na nchi nyingine wamefunga mipaka, sisi sijui tunasubiri nini.Yaani seriously kabisa tunaendelea kupokea wageni kutoka nchi zilizoathirika. Eti wanapimwa joto airports halafu wanaachwa wajichanganye na general population.
Nasikia kuna mtu amesema China ni nchi rafiki hatuwezi kuwazuia kuingia! As if viruses wanajua mambo ya urafiki wa binadamu.
Anyways Europe, US, Iran na Italy ni marafiki zetu pia! Lete maneno.
 
Je serikali haioni umuhimu wa kuwa na maabara zaidi ya hii moja ya hapa Dar? Kuwa na maabara zaidi kutasaidia kugundua wagonjwa mapema hivyo kupunguza kasi ya kueneza ugonjwa!
 
Hivi kama Ghana,Cameroon na nchi nyingine wamefunga mipaka, sisi sijui tunasubiri nini.Yaani seriously kabisa tunaendelea kupokea wageni kutoka nchi zilizoathirika. Eti wanapimwa joto airports halafu wanaachwa wajichanganye na general population.
Nasikia kuna mtu amesema China ni nchi rafiki hatuwezi kuwazuia kuingia! As if viruses wanajua mambo ya urafiki wa binadamu.
Anyways Europe, US, Iran na Italy ni marafiki zetu pia! Lete maneno.
Tukifunga mipaka tutadhoofisha utalii
😀😀😀😀
 
Tatizo la uelewa nchi hii limekuwa kubwa sana!

Umewafikia kutokea wapi? Si hao waliofuata raia wao Wuhan ndiyo wanasambaza.
Mkuu kama nakuelewa,

Laiti nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini wangeacha tatizo liwe contained China huenda ugonjwa usingesambaa sana kama ilivyo sasa..

Ni kweli Nchi zilizo evacuate raia wao kutoka China ndio wamekuwa chanzo cha ugonjwa kusambaa kwa kasi nchi nyingi Duniani...

Nchi nyingi zilizoripoti kesi ya kwanza, wagonjwa wengi ni kutoka katika mataifa walio evacuate raia wao kutoka China.

We didn't evacuate our beloved, but we are paying the price of those who chose to evacuate.
 
Tukifunga mipaka tutadhoofisha utalii
😀😀😀😀
Inaonekana hii ndio sababu, lakini ni counterproductive. Hivi nchi ikiwa na wagonjwa wengi, kuna watalii watakuja kweli? Tayari naambiwa watalii wengi wamecancel bookings, hawaji, wanasubiri hali itulie.
Halafu wananchi wengi wakiugua itaathiri shughuli nyingi za kiuchumi.
 
Nimekuelewa ingawa kulikua na contradiction kuhusu taarifa kutoka Zanzibar
Mkuu pakaywatek nadhani katika mambo serious kama hili janga la CORONA tuache mzaha kabisa. Je Zanzibar ina waziri Kiongozi? Je Mh. Kassim Majaliwa si ni Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Including Zanzibar) ?. Mkuu tuache mzaha.

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia "UPEPO WA KISULISULI" ndio hii Corona sasa, dah. Huyo wa Dar ikisemekana alipanda kwa kugombania "MWENDO KASI", itakua kasheshe.

Kesho utasikia wamepatikana wagonjwa 5 wa kisulisuli, wawili Tandale, mmoja Mbagala, na wawili Manzese.

Lugha yako ya mwishoni daah haya
 
Jamani kama hawafungi mipaka na kuzuia waletwao na ndege toka ng'ambo, basi watupe muongozo sisi akina pangupakavu tujifiche chaka gani?!! make sio wanasubiri ugonjwa usambae zaidi halafu ndo watupige marufuku ya kujifungia ndani kama "kuku mataahira" ilhali wengi wetu bila mihangaiko watoto mikono haiendi kimyani- si tutakufa kwa njaa jamani kabla ya hata masahibu ya corona hayajabisha malangoni petu!!

Sometimes huwa najiuliza hawa watawala huwa wanawaza kwa kutumia nini jamani ikiwa tu wameshindwa kuhimili vifo vya mama&mtoto wakati wa kujifungua, sembuse kupambana na hiyo CORONA?? Maandalizi yenyewe ya ajabu ajabu kama "kukanda unga wa ngano"!

Maweee twafaaa, MWENYEZI MUNGU EPUSHIA MBALI BARAA HILI.
 
Wanasubiri hadi iwe janga Tz ndio wafunge mipaka, kuna uzembe sana kwenye maamuzi dhidi ya hili janga kwa TZ.
Funga kwanza milango yako ubaki ndani na familia yako tuone kama unao uwezo wa kumudu hata wiki moja. Kama ilivyo milango kwa nyumba yako ndivyo ilivyo mipaka kwa nchi. Huna dawa, huna kila kitu ndani unategemea kitoke nje then ufunge milango?
 
Back
Top Bottom