Serikali: Idadi ya Wagonjwa wa COVID19 kwenye baadhi ya vituo yapungua

Serikali yatoa Update ya Corona Nchini .

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe amesema kuwa wagonjwa wa corona nchini wamepungua katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuwataka watoa huduma za afya kujitahidi kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mengine pia


VIDEO NI KWA HISANI ya Millard Ayo wa Ayo Media.

 

Watu ni kuwa hawaendi hospitali wameamua kfia nyumbani. Hakuna kupungua
 
😳😳😳😳😳😳
 
Kumbe maabara inaendelea kupima? Si Walisema sasahivi hawapimi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa unahitaji maombi mengine ya siku tatu mfululizo maana naona yale Mkulu alituelekeza yaliacha baadhi ya wenzetu nyuma wewe ukiwemo.
 
endelea kufuata propaganda za mzungu utakuja kuelewa baadae
 
Darwin Theory law of the jungle survival for the fittest.
Kwa hiyo wanyonge hawatakiwi kulindwa?
 
Mimi sidhani kuwa hali imekuwa nzuri.
Wagonjwa wengi wanakwepa kwenda kwenye vituo vilivyotengwa maana huduma hairidhishi.
Wengi wanaamua kujitibia majumbani mwao.
 
Kapimeni watu huko waliko ,haya ya vituoni kupungua sio kipimo cha kuonyesha hali halisi ya wagonjwa ,wengine hawaendi vituoni,kwanza ilitakiwa mtoe orodha ya vituo vya kupimia corona kwa kila wilaya.
 
Takwimu pekee zilizobakia hapa Tanzania na za kuaminika ni za madereva ya malori ya mizigo, ambao ni wale wavukao mpakani kuingia nchi za jirani, ambapo wenzetu wanatusaidia kuwafanyia vipimo ya Corona na hatimaye kutupa matokeo yake, wakati sisi kwa upande tukiendelea na zoezi la "herd immunity"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Sawa
Taarifa Njema Iwapo Ni Kweli
Kama ni uongo muulizeni mtoto wa mbowe maana alikua kwa wagonjwa mtuonyeshe picha za wagonjwa walio jazana kama mnavyo dai maana kila kitu mijitu inabisha .

Send by APOLO 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…