Serikali iingilie kati ukatili dhidi ya Watanzania waishio Uturuki na nchi za Kiarabu

Serikali iingilie kati ukatili dhidi ya Watanzania waishio Uturuki na nchi za Kiarabu

Tena wanapaswa wakamatwe na washitakiwe kwa kufanya biashara haramu ya kuuza miili, tena mabalozi wasijihusishe kuwasaidia kabisaa
 
Tatizo kubwa Dada zetu wanapenda maisha ya miteremko kutofautiana na uhalisia wa nchi yetu. Sasa mwisho wa siku huishia kuingia pasipoingilika . Wengine wanaenda wakijua wanaenda kujiuza
 
Waarabu co watu wazuri dada zetu hawasikii, unaendaje nchi ya mbali bila kua na info zozote. Nawaonea huruma lakn imeandikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa . Yan hao waturuki wana roho mbaya sana sana
Wengine huko huko wametengeneza maisha wanawatumia home kwao wamejenga na wanasomesha ndugu zake na ukombozi wa familia.
Hata hapa Nchini wanateswa tena zaidi kuliko hata huko.
 
Kama wanaenda kujiuza wacha sheria za huko zichukue mkondo wake. Ila kama wameenda kwa shughuli nyingine halali halali halafu wananyang'anywa passport na kutekwa na kuingizwa ktk madanguro hapo ndiyo serikali iingilie kati.
 
Eti mnataka kuwalaumu wachina/waturuki/waarabu, mara mnataka kilaumu serikali kwa sera mbaya ya uchumi. Huo wote ni ulimbukeni.
Kila kona duniani kuna biashara ya umalaya. Hao akina dada wengi walikua wanajua fika kwamba wanakwenda hizo nchi kufanya nini. Hakuna mtu alishikwa mkono aende huko. mambo yakishagarambuka ndio wanazuga Eti wananyanyaswa wanataka msaada. Waachane na sisi, wasituvuruge vichwa.

Na mleta mada kama maisha ya useaman huyajui uwe mada nyingine unafikiria. Kama wewe ni mjanja, msafiri na mtoto was mjini huezi leta mada kama hii hapa. Kuna watu kibao wako hizo nchi, wanfanya mambo yao ya maana, mtaishia kuharibia Kila mtu sasa.
 
Solution sio kuwazuia kwenda nje kusaka riziki, muhimu ni kuwatengenezea mazingira salama nje, huwezi mzuia binadamu mwenye akili timamu.Utamzuia airport anaondoka njia za panya anaepandia nchi jirani ndege anaenda nje.Pamoja na kuwazuia Bado wanaondokea nchi jirani.

Muhimu mazingira salama aendako, wapewe seminar kabla ya kuondoka,nk.Huwezi ukamzuia mwanadamu mwenye akili zao.Na si watz pekee ndo uenda arabuni karibu nchi zote za asia kusini uenda fanya kazi za ndani arabuni.Tumeshindwa watenganezea vijana ajira Nchini Acha wakazisake nje.
 
Kama wanaenda kujiuza wacha sheria za huko zichukue mkondo wake. Ila kama wameenda kwa shughuli nyingine halali halali halafu wananyang'anywa passport na kutekwa na kuingizwa ktk madanguro hapo ndiyo serikali iingilie kati.
Kunyanganya pasipoti ya nchi nyingine ni kosa hapo serikali inapaswa kuingilia
 
Binadamu wema na wabaya wapo kwenye jamii zote duniani,kuwahukumu waarabu wote ni wabaya kupitia wachache ni kutowatendea haki.
 
Hivi kuna wanaoondoka Tanzania kwa kujua kuwa wanakwenda kuwa makahaba?
Wengi tu msingi kiuno akirudi ana mtaji wa kutosha then ugeuka madalali na kuwachukua wengine kuwauza nje.
Kama huna asili ya ukahaba hata ukienda nje utakuwa vipi kahaba sasa, yaani ukose hata akili ya kuomba msaada wa mteja akusaidie?
 
Shida atujapata bado kiongozi sahihi atakaeshuka chini na kuishi maisha ya watz, Bado kuna fursa nyingi Sana hazijatumika kwenye raslimali zetu Kama zingetumika vizuri kimkakati zingemaliza tatizo la ajira nchini.
 
Wengi wao wanaenda hali wamejitoa muhanga, wakijua fika ni nini kinawapeleka na nini chaweza kuwakuta.

Wengi wanaenda kihalali wanatumikia mikataba yao, wanarudi salama.
Hao wadangaji hata huku Bongo huwa wanakamatwa.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Sababu wanaenda kufanya uzinzi haina shida acha wapate stahiki zao, ila kama ingekuwa wameenda kwa ajili ya shughuli nyingine kama za kielimu na mfano wake, hapo ningeunga mkono hoja.

Lakini watoto wa kike kwani lazima kwenda kutafuta maisha nje ? Na huku kila siku wanaambiwa kuna madhila ya kila aina ?
 
Kwani nani huwa anawapeleka huko?
Lipo genge la wahuni hapa Tanzania na huko waendako.

Ni network fulani hivi ya biashara.

Kuna Tatizo kubwa sana ktk airport na borders zetu.

Hili suala kingekwisha.
 
Piganeni na hali zenu haya madanguro mbona hapa Tz yamejaa telee tena ya kila dizaini mnaonaje tukaanza kusafisha hapa ndani,kisha tukawakurupusha waendao huko,mleta mada tuwekee ushahidi wa hayo uliyotongoa,iliingia fitina mupaka sasa madada zetu imekuwa mtihani kupata kuondoka kwa kwenda kufanya kazi ughaibuni kwa kisingizio cha kulazimishwa kufanya ugahaba,sasa nini kazi ya mabalozi wetu huko ?

Unajua kwenye kundi la mamba na kenge wamo.
Mawakala kwa kutetea upuuzi hamjambo.

Nonsense.
 
Back
Top Bottom