Serikali ikiondoa unafiki na chuki bado Kagera inaweza kuchomoza, Chalamila unatakiwa kujua haya

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Kinachosikitisha ni kwamba kila anayepanda jukwaa kuelezea kinachoitwa umaskini wa Mkoa wa Kagera anakuja na ngonjera za wingi wa maprofesa na ma-PhD holders kutoka mkoani mwetu. Lawama zote zinarundikwa kwa watu hao na Wanakagera kwa jumla.

Huo ndio ukasuku na unafiki wa watawala wetu ambao tumezoea kwa miaka mingi sasa. Watawala wanajifanya kama hawajui chanzo halisi cha kile wanachokiita umasikini uliokithiri mkoani humo. Bila tafakuri yoyote ya "tafiti" zinazodaiwa kufanywa na Serikali, wanakuja tu na porojo za jumlajumla kuhusu "umasikini" huo. Tafiti hizo za kimangumashi hazielezei chanzo cha tatizo la mkoa wa Kagera.

Haziangalii matokeo ya vita vya Kagera na uharibifu wa usalama na miundombinu uliosababishwa na ugomvi wa Serikali na Iddi Amin. Kwamba shughuli za uzalishaji na kiuchumi zilikufa kabisa kutokana na vita hiyo.

Hawaoni kwamba serikali ilikosea (kwa makusudi) kutotangazwa kwa hali ya hatari mkoani humo, kwa maana ya kujenga miundombinu upya na kuwasaidia wanakagera kurudia maisha yao ya kabla ya vita. Hawasemi Serikali ilifunga mpaka na Uganda, hivyo kusitisha shughuli zote za kiuchumi, ambapo soko kuu la mkoa wa Kagera lilikuwa Uganda. Baada ya vita Ukimwi uliotokea Uganda ulimaliza nguvukazi kubwa ya mkoa huo kwa kupuputisha maisha ya maelfu ya nguvukazi wa Kagera.

Wanajifanya hawajui kwamba MV. Bukoba ilizama na kuua mamia ya watu, wengi wao wakiwa Wanakagera. Hapohapo, MV. Victoria "iliharibika" na kufanya Wanakagera kukosa kabisa usafiri wa kuwaunganisha na nchi yao, huku mazao yao ya kiuchumi yakishindwa kusafirishwa kwenda kwenye masoko makubwa ya kibiashara ya hapa nchini kama Mwanza na Dar es Salaam. Serikali haikuona umuhimu wa kuwapa Wanakagera vyombo vingine vya usafiri ili wajimudu kiuchumi.

Ndipo pia ulipoingia "Ugonjwa wa Mnyauko" wa migomba uliopigilia msumari wa mateso na umasikini wa wanakagera. Yapata sasa zaidi ya miaka 15. Je, Serikali ilichukua hatua gani kuwasaidia wakulima wa kilimo cha migomba mkoani Kagera? Hakuna! Wakati huohuo Wanakagera walikatazwa kuuza kahawa yao nchini Uganda ambako walikuwa wanapata bei nzuri kulingana na gharama za uzalishaji. Waliopatikana na uvushaji wa zao hilo waliadhibiwa, ikiwemo vifungo au kufilisiwa, huko kahawa ikilimbikiziwa "tozo" lukuki bila kutilia maanani gharama za wakulima za uzalishaji.

Hiyo ni mifano michache tu ya hujuma ya serikali dhidi ya mkoa wa Kagera kwa miongo mingi sasa. Matokeo yake ni nini, Wananchi wa mkoa wa wa Kagera waliona serikali ilikuwa haiwataki, haiwapendi. Wakasema isiwe taabu, wakaamua kuhamia mikoa nyingine nchini na kuwekeza huko. Je, serikali inajifanya haioni uwekezaji wao mkubwa na uliotukuka katika mikoa mingine nchini, ikiwemo Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha na kwingineko?

Serikali imekuwa ikipiga kelele nyingi eti wahaya wameshindwa kujenga soko na kituo cha mabasi mjini Bukoba, ikijifanya haijui kwamba jukumu hilo ni lake na vyombo vyake, ikiwemo TAMISEMI. Kwani vituo vya mabasi na masoko ya Dodoma, Morogoro, Dar Es Salaam, Mwanza na kwingineko vimejengwa na nani kama sio Serikali? Nimalizie kwa kuishauri Serikali kwamba iwekeze mkoani Kagera kama ambavyo imekuwa ikiwekeza sehemu nyingine nchini.

Ikiwekeza Kagera, kama ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kufanya kwa kujenga kitengo cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), mkoani humo, basi itarajie kwamba maprofesa na PhD holders kutoka mkoani Kagera watarudi nyumbani kufaidi fursa za uwekezaji wa serikali. Ni matumaini ya wengi mkoani Kagera kwamba Mkuu mpya wa mkoa wa Kagera, Mhe. Chalamila ataelewa chanzo cha "umasikini wa mkoa wa Kagera."
 
Tatizo lenu ni ego ! Yaani kila kitu unalaumu serikali.

Kilimanjaro imehujumiwa sana kuliko Kagera, iko mpakani kama Kagera, wana Kahawa kama Kagera tena Kagera wana Ardhi nzuri na kubwa zaidi, wasomi kama Kagera. Sasa tofauti iko wapi ? Ni utamaduni pamoja na kwamba kuna wasomi wengi Kilimanjaro wananchi wa Kilimanjaro wana wathamini zaidi wafanyabiashara kuliko wasomi. Pili Kilimanjaro kuna utamaduni wa harambee za shule, makanisa, na hata barabara za mitaani. Tatu watu wa Kilimanjaro wana wekeza nyumbani kwao na ku lobby ili wapate pesa za maendeleo. Nne Kilimanjaro wamewawezesha wanawake kwenye maendeleo kuanzia biashara hadi kilimo.

Hakuna hujuma mpaka makatibu wa CCM walitoka huko🤔 badala ya kulalamika jiangalieni wenyewe
 
Tatizo lenu ni ego ! Yaani kila kitu unalaumu serikali.

Kilimanjaro imehujumiwa sana kuliko Kagera, iko mpakani kama Kagera, wana Kahawa kama Kagera tena Kagera wana Ardhi nzuri na kubwa zaidi, wasomi kama Kagera. Sasa tofauti iko wapi ? Ni utamaduni pamoja na kwamba kuna wasomi wengi Kilimanjaro wananchi wa Kilimanjaro wana wathamini zaidi wafanyabiashara kuliko wasomi. Pili Kilimanjaro kuna utamaduni wa harambee za shule, makanisa, na hata barabara za mitaani. Tatu watu wa Kilimanjaro wana wekeza nyumbani kwao na ku lobby ili wapate pesa za maendeleo. Nne Kilimanjaro wamewawezesha wanawake kwenye maendeleo kuanzia biashara hadi kilimo.

Hakuna hujuma mpaka makatibu wa CCM walitoka huko[emoji848] badala ya kulalamika jiangalieni wenyewe
Sorry Kilimanjaro ishawahi pata vita yoyote...na watu zaidi ya 2000 kufa?
Tuanzie hapo kwanza

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Umetoa visingizio vyakitoto sana.Yaani unasingizia vita vya miaka 40 iliyopita.Mambo mengi uliyoyataja hapo yameshindwa kwasababu ya wananchi wenyewe kulala.Kama watz tulivyolala ndivyo ambavyo nanyie mmelala.Kuna mikoa yakulalamika ila sio kagera kwasababu kuna kila kitu chakuwafanya mpige hatua.
 
Mkuu nasikia kagera kila nyumba kuna profesa . . Ni kweli ??
Ndiyo ni kweli, ila maprofesa hao na PhD holds wa Kagera ndio wana waelimisha watu wa Kigoma, Mara, Mtwara na kwinginko! Hawahudumii Kagera tu! Ni Tanzania nzima na kwingine duniani.
 
Kinachosikitisha ni kwamba kila anayepanda jukwaa kuelezea kinachoitwa umaskini wa Mkoa wa Kagera anakuja na ngonjera za wingi wa maprofesa na ma-PhD holders kutoka mkoani mwetu. Lawama zote zinarundikwa kwa watu hao na Wanakagera kwa jumla.

Huo ndio ukasuku na unafiki wa watawala wetu ambao tumezoea kwa miaka mingi sasa. Watawala wanajifanya kama hawajui chanzo halisi cha kile wanachokiita umasikini uliokithiri mkoani humo. Bila tafakuri yoyote ya "tafiti" zinazodaiwa kufanywa na Serikali, wanakuja tu na porojo za jumlajumla kuhusu "umasikini" huo. Tafiti hizo za kimangumashi hazielezei chanzo cha tatizo la mkoa wa Kagera.

Haziangalii matokeo ya vita vya Kagera na uharibifu wa usalama na miundombinu uliosababishwa na ugomvi wa Serikali na Iddi Amin. Kwamba shughuli za uzalishaji na kiuchumi zilikufa kabisa kutokana na vita hiyo.

Hawaoni kwamba serikali ilikosea (kwa makusudi) kutotangazwa kwa hali ya hatari mkoani humo, kwa maana ya kujenga miundombinu upya na kuwasaidia wanakagera kurudia maisha yao ya kabla ya vita. Hawasemi Serikali ilifunga mpaka na Uganda, hivyo kusitisha shughuli zote za kiuchumi, ambapo soko kuu la mkoa wa Kagera lilikuwa Uganda. Baada ya vita Ukimwi uliotokea Uganda ulimaliza nguvukazi kubwa ya mkoa huo kwa kupuputisha maisha ya maelfu ya nguvukazi wa Kagera.

Wanajifanya hawajui kwamba MV. Bukoba ilizama na kuua mamia ya watu, wengi wao wakiwa Wanakagera. Hapohapo, MV. Victoria "iliharibika" na kufanya Wanakagera kukosa kabisa usafiri wa kuwaunganisha na nchi yao, huku mazao yao ya kiuchumi yakishindwa kusafirishwa kwenda kwenye masoko makubwa ya kibiashara ya hapa nchini kama Mwanza na Dar es Salaam. Serikali haikuona umuhimu wa kuwapa Wanakagera vyombo vingine vya usafiri ili wajimudu kiuchumi.

Ndipo pia ulipoingia "Ugonjwa wa Mnyauko" wa migomba uliopigilia msumari wa mateso na umasikini wa wanakagera. Yapata sasa zaidi ya miaka 15. Je, Serikali ilichukua hatua gani kuwasaidia wakulima wa kilimo cha migomba mkoani Kagera? Hakuna! Wakati huohuo Wanakagera walikatazwa kuuza kahawa yao nchini Uganda ambako walikuwa wanapata bei nzuri kulingana na gharama za uzalishaji. Waliopatikana na uvushaji wa zao hilo waliadhibiwa, ikiwemo vifungo au kufilisiwa, huko kahawa ikilimbikiziwa "tozo" lukuki bila kutilia maanani gharama za wakulima za uzalishaji.

Hiyo ni mifano michache tu ya hujuma ya serikali dhidi ya mkoa wa Kagera kwa miongo mingi sasa. Matokeo yake ni nini, Wananchi wa mkoa wa wa Kagera waliona serikali ilikuwa haiwataki, haiwapendi. Wakasema isiwe taabu, wakaamua kuhamia mikoa nyingine nchini na kuwekeza huko. Je, serikali inajifanya haioni uwekezaji wao mkubwa na uliotukuka katika mikoa mingine nchini, ikiwemo Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha na kwingineko?

Serikali imekuwa ikipiga kelele nyingi eti wahaya wameshindwa kujenga soko na kituo cha mabasi mjini Bukoba, ikijifanya haijui kwamba jukumu hilo ni lake na vyombo vyake, ikiwemo TAMISEMI. Kwani vituo vya mabasi na masoko ya Dodoma, Morogoro, Dar Es Salaam, Mwanza na kwingineko vimejengwa na nani kama sio Serikali? Nimalizie kwa kuishauri Serikali kwamba iwekeze mkoani Kagera kama ambavyo imekuwa ikiwekeza sehemu nyingine nchini.

Ikiwekeza Kagera, kama ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kufanya kwa kujenga kitengo cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), mkoani humo, basi itarajie kwamba maprofesa na PhD holders kutoka mkoani Kagera watarudi nyumbani kufaidi fursa za uwekezaji wa serikali. Ni matumaini ya wengi mkoani Kagera kwamba Mkuu mpya wa mkoa wa Kagera, Mhe. Chalamila ataelewa chanzo cha "umasikini wa mkoa wa Kagera."
Viongonzi Kama Chalamila,ni wakupuuza, Hawa ni wanafiki Kama wanafiki wengine kujifanya wazalendo kumbe ni Kati ya wale waliojilimbikizia ukwasi KWA njia za wizi kipindi Cha mwendazake huku akujifanya mzalendo, Hawa ndo huwasimanga wananchi na umaskini wakati bado nikupitia wananchi hao wanakwapua pesa ,

Sawa kagera bado ipo nyuma ila vipo Tanga, Songea, Tabora, hivi nao hawaendelei kisa vingereza vingi? Huyu ni mshamba bado Kama washamba wengine, Kama kiongozi badala ya kuwa mbunifu na kuja na suruhu namna ya kuwakwamua wananchi KWA kutoa mawazo mbadala,upo na vitisho na ubabe, huyu huwa Kati ya watu wanaokurupuka Sana katika kauli zake
 
Sorry Kilimanjaro ishawahi pata vita yoyote...na watu zaidi ya 2000 kufa?
Tuanzie hapo kwanza

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Dar-Es - Salaam pekee kwa wiki wanakufa zaidi ya hao watu 2000.

Idadi ya watu 2000 kwa mkoa mkubwa kama kagera ni ndogo sana kiasi iufanye mkoa usiendelee wa ajali iliyotokea miaka almost 30
 
Ukimwi, Vita, kushika kwa bei ya kahawa, MV Bukoba siyo sababu za msingi kwasabb haya yaliathiri na mikoa mingine pia.

Labda kodogo ugonjwa wamnyauko uliikumba Kagera pekee
 
Viongonzi Kama Chalamila,ni wakupuuza, Hawa ni wanafiki Kama wanafiki wengine kujifanya wazalendo kumbe ni Kati ya wale waliojilimbikizia ukwasi KWA njia za wizi kipindi Cha mwendazake huku akujifanya mzalendo, Hawa ndo huwasimanga wananchi na umaskini wakati bado nikupitia wananchi hao wanakwapua pesa ,

Sawa kagera bado ipo nyuma ila vipo Tanga, Songea, Tabora, hivi nao hawaendelei kisa vingereza vingi? Huyu ni mshamba bado Kama washamba wengine, Kama kiongozi badala ya kuwa mbunifu na kuja na suruhu namna ya kuwakwamua wananchi KWA kutoa mawazo mbadala,upo na vitisho na ubabe, huyu huwa Kati ya watu wanaokurupuka Sana katika kauli zake
Unapokoasolewa sio dhambi, bali chukua mawazo ya anayekukosoa uyafanyiekazi na usonge mbele.
Tuje kwenye hojja za Chalamila. Mmeletewa Pesa ya Kujenga soko la Kisasa toka mwaka 2016 lakini hadi leo 2022 vikaoni mnalumbana mahala pa kujenga soko lenu wakati mikoa ya Wenzenu masoko yalisha isha na yanatumika, kesi hii iko Kagera na Katavi.
Mna fedha ya kujenga Stendi mnabishana kwa Viingereza vya Lubisi ijengwe wapi mwaka wa 6 sasa wenzenu mliokuwa nao kwenye batch moja ya Mradi Sumbawanga, Katavi, Iringa, Pwani nk wana Stendi mpya zinatumika nyinyi bado mnabishana upuuuzi.
Kwa mifano hii michache utetezi wenu wa Vita, UKIMWI mliojiletea kwa Nyegez zenu na MV Bukoba kuzama inachangia wapi???
Acheni ujuaji kenge nyie
 
Na ndo maana Serikali inafeli Sana ,badala ya kusikiliza wananchi wapi Mradi flani ujengwe Ili kuleta ufanisi ,mnakurupuka jenga popote Ili Hali mpate 10 % , angalia stendi zenu mnapozijenga, hayo masoko mnapo yajenga KWA kutosikiliza wananchi wa maeneo husika, inakua dhahama na mateso kwa wananchi,
Nenda Songea ,njombe, Dodoma, Dar, lakini ipo ile stendi ya mail mbili kibaa, hii ndo kichekesho, stendi nzuri ila hamna kitu

Swali
Serikali mnajenga soko au stendi,Ili kujenga tu au mnajenga Ili kuleta ufanisi kwa wananchi? Na Kama ni kuleta ufanisi KWa nini pasiwepo ushirikishi KWa wananchi wa eneo husika?
Tatizo serikali imewazoea Sana wananchi siku mkivulumishwa na wenye nchi kwenye mavi8, na ofisi za viyoyozi za uma, akili ndo utawakaa sawa, na KWa serikali itakayo kuwa Madarakani kipindi hicho, haitaweza kuja na kauli za hovyo za namna hii KWa wananchi, si mnasema Tukahamie Burundi, ila mtatangulia wenyewe,
 
Kwa hiyo nyie wananchi wa Kagera mnajadili miaka Sita wapi mjenge soko na stand?
Mko very serious aisee
 
Ninasema hata sie wa ,Njombe, Iringa, Songea n.k tulitakiwa shirikishwa wapi masoko na Stendi vijengwe, hili la Kagera ni mfano tu unaonesha ni KWa namna GANI wananchi Tunaburuzwa na Serikali, kwamba kwenye Miradi inayotugusa moja kwa moja hatushirikishwi, sawa WENDA miaka sita ikawa mingi tokana na malumbano wapi Mradi utajengwa ,ila ni kazi ya viongonzi kupima hoja na kuja na suruhu sio toa maneno ya hovyo,
Kuna pengine yamejengwa ayo masoko tz hii na stendi tena KWa gharama kubwa ila yatachukua miaka hata 30 bila kutorudisha gharama, Sasa nijibu,
Lipi zuri ,jenga mradi KWa mwaka au mda mfupi ila ufanisi wake unakua sufuli, au chelewa kujenga na ukajenga pale ambapo ufanisi ni 100% jibu mkuu
 
Tatizo la wahaya kinachowamaliza ni kujifanya wajuaji wa kila kitu....mama yangu ni muhaya alikuwa ananisisitiza sana kumuowa muhaya....mimi niligoma kabisaaa siwezi kumuowa mtu atakaekuwa mjuaji wa kila kitu...
Wewe muongo sana. Uliyoyasema yanahusianaje na halmashauri kutenga fedha za kujenga miundo mbinu. Serikali ina nia ovu na kagera. Fedha za kuendeleza uwanja wa ndege kqjunguti mbona zilipelekwa chato.
 
Anaongea kiushabiki, ni kabila GANI tz hii ambalo wanaume au wanawake hawana mapungufu, wanasema ndugu zetu hupenda sifa, n.k unajiuliza anaeongea hivi alikwisha kaa na makabila yote?
Kama sifa kila binadam anapenda sifiwa na ndo maana viongonzi wengi, wasanii Wana machawa wakusifia,
Kiongozi akiwa Mbele ya Rais atasifia ,mh 20 ndani ya maneno matatu,
Hakuna kabila halina mapungufu, mengine ni kujifariji tu,
 
Mkuu nasikia kagera kila nyumba kuna profesa . . Ni kweli ??

sio tu ilo kuna watu wamefanya vizuri na mchango mkubwa nje na ndani na hawa julikani wapo kimya
 
Umetoa visingizio vyakitoto sana.Yaani unasingizia vita vya miaka 40 iliyopita.Mambo mengi uliyoyataja hapo yameshindwa kwasababu ya wananchi wenyewe kulala.Kama watz tulivyolala ndivyo ambavyo nanyie mmelala.Kuna mikoa yakulalamika ila sio kagera kwasababu kuna kila kitu chakuwafanya mpige hatua.

jifunze kujua athali basi !. mfano nyumba yako imeungua ujatoa hata chupi !. miaka 40 iliyopita unazani utakuja kuwa sawa mpaka sasa
 
Back
Top Bottom