DOKEZO Serikali imchunguze Mwalimu huyu wa Shule ya Mandimu (Singida), matendo yake ni tishio kwa Wanafunzi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huyo mwalimu kama akampiga mwanangu kwa staili hiyo,ndo mjue vita ya nne ya dunia imeanza rasmi
 
Inaonekana hujawasoma vizuri watanzania wa miaka hii, hawana muda wa kufuatilia kabisa mambo ya msingi kwenye jamii wanazoishi Wako bize na mambo ya kipuuzi tuu kama mipira, kubeti/mabonanza, ulabu, mademu etc...unaweza kukuta ulivyoambiwa ni kweli kabisa but they don't have time,pamoja na kuwa na kamati ya shule.

Hapo watakuja kukurupuka wakisikia mwanafunzi kuvunjwa mkono au kafariki kwa kipigo, utawaona watakavyoandamana.

Kiufupi tuna janga kubwa sana kwenye society zetu. Kibwagizo: Juzi kuna jamaa mmoja nimeona akihojiwa na Azam Media, akasema yeye yuko kwenye magroup ya Whatsapp zaidi ya 100 na pia yuko social media zootee kuanzia facebook mpata X...na yuko very active!! Baada ya kuona watu wanachangiana sana hizi mambo za Harusi, send off nk basi yeye akawa ameandaa wazo lake zuri la biashara.

Kwenye mtaji wa hiyo biashara akawa ana nusu ya pesa na imepungua nusu (nadhani alitaka kama millioni 2 hivi).

Basi bwana jamaa akaamua awashirikishe wanagroup wenzake kwenye magroup yote na pia kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kufanya hivyo kilichotokea ni kwamba kwenye baadhi ya magroup walimuondoa, wengine kwenye mitandao walimblock na mwishowe anasema hakupata hata mia!!! Je tunajifunza nini hapooo???
 
Kazi nzuri, lakini Kwa nini usitumie pia taaluma yako kupambana na wabadhirifu wa mali za umma ambao wamekuwa wakibainishwa na CAG kwenye ripoti zake za kila mwaka?
 
Mwalimu Frank jela inakubeep.

Kimbia fasta.
Ni Stress sijui baadhi ya walimu wanayo..Kwanini umpe mtoto wa mtu mwingine kipigo kikali ??Ukiona ni mkorofi ameshindikana achana naye

Kujitafutia matatizo bure,mara umeua unajitafutia matatizo bure.
 
Wanakijiji wamekujaza majungu na fitina na wewe umeyachukua kama yalivyo na kwanini umeconclude bila kusikiliza upande mwingine kwa kumuuliza muhusika.
Na wewe ulivyo mjinga Jambo la kijiweni kwenye kahawa unaleta hukuu? Shamba umepata kwanza wewe...kenge jike wewe
 
Wazazi wamewaachia malezi yote walimu. Shida inaanzia hapo.
Wazazi wawalee watoto wao vema waache visingizio.
Mtoto akiwa vizuri kwenye malezi ya nyumbani kamwe hawezi kuadhibiwa ovyo shuleni.
Sasa hivi wazazi wanawapelekea walimu mitoto mijambazi!
Mitoto iliyoshindikana. Mitoto mila bangi. Mitoto.....
Poleni sana walimu kazi yenu ni ngumu sanaaa lakini mwenyezi Mungu atawalipieni. Msikate tamaa. Hakuna aliyemo humu JF hakupita kwa mwalimu. MMEGEUKWA!
 
Ningefungua uzi kuwauliza jamii forums mods, acha niwaulize hapahapa kwemye comments na kama wanajari kweli watanijibu, (Naomba anaejua kutag awatag moods hapa)

Kwanza nawapongeza kwa kutoa feedbacks za baadhi ya nyuzi za madokezo kama nyuzi ile ya vyoo vichafu vya stend na tatizo la maji ambayo wadau walitoa kero hzo hapa jf na kero hzo zilipo tatuliwa kwa msaada wa sauti ya jamiiforums mods walileta mrejesho ikimaanisha kwamba walikua wakifatilia na kufanyia kazi madokezo ya wadau wake.

Sasa swali langu ni juu ya hizi taarifa za ukatili wa walimu kwa watoto/wanafunzi na ukatili wa walimu wakuu/ makatibu wa elimu ngazi mbali mbali kwa walimu wa kawaida kwanini hua hatupati mrejesho kama mhusika kafatiliwa??

Mirejesho mingi hua naisoma fb, whatsapp, etc na si hapa jf, kama hua wanaandika na sizioni basi shukurani sana kwenu kwa kujari.

Majibu yenu/ mirejesho ndio yatatutia moyo wa kuendelea kuleta taarifa za kufichua maovu.
ASANTENI SANA.
 
Kazi nzuri, lakini Kwa nini usitumie pia taaluma yako kupambana na wabadhirifu wa mali za umma ambao wamekuwa wakibainishwa na CAG kwenye ripoti zake za kila mwaka?
Tutafika huko ili mradi tu kuhakikisha usawa wa kijamii unafikiwa maana ukishakuwa kwenye field ya sheria hutakiwi kuogopa chochote as long as unachopambania is for public interest mkuu.
 
Reactions: K11
Mleta mada nasubiri mawasiliano ya huyo Mwalimu ama hata ya Afisa Elimu Wilaya.

Hapo kijijini huwezi kukosa mawasiliano ya Mwalimu. Natamani nisingekuwa busy kipindi hiki, kesho asubuhi ningekuwa hapo kijijini nije niongee na huyo Mwalimu very friendly lakini asipoonesha kubadilika basi atajuta kwasababu sheria itamfunza namna ya kujali haki za watoto.
 
Tutafika huko ili mradi tu kuhakikisha usawa wa kijamii unafikiwa maana ukishakuwa kwenye field ya sheria hutakiwi kuogopa chochote as long as unachopambania is for public interest mkuu.
Nakutakia kila la heri na Mungu wa Tanganyika awe pamoja nawe.
 
Dkt. Gwajima D tunakuomba Mheshimiwa Waziri wetu msikivu fuatilia dokezo hili usipuuze maana hakuna wa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili zaidi ya sisi kama jamii na wewe kama kiongozi mwenye dhamana.

Kupitia mtoa dokezo una access ya kufanya mawasiliano na mhusika mwenyewe ama wakuu wake ili wafanye uchunguzi.

Kama jamii inatupasa tuwe watu wa kuzuia maovu kuliko kuyatatua maana ikifikia stage ya kuyatatua maana yake mambo yameshakuwa mabaya.
 
Kama kweli haya yooote yanafanyika na.....
Afisa elimu kata yupo.
Afisa elimu wilaya yupo.
Mtendaji wa kijiji yupo.
Mwenyekiti wa kijiji yupo.
Mabalozi wa nyumba wapo.
Wanakijiji wanaume wababa wapo.
Vijana wenye kujitambua na wenye nguvu wapo.
 
Kama umepita shule utakua unajua adhabu za jumuia kama za upiga kelele darasani wote mfiche uso kwenye dawati bila kujali kama ulipiga kelele au laa, hapo malezi ya mzazi yanaingiaje?

Mtoto kakulia kwenye gas na umeme au mkaa, anakuta shule wanapasua kuni hajui shoka wanashikaje na hana nguvu kivile, asipopasua kuni ni fimbo sana na kutokula hapa unakuta mzazi hajui au ni shule gani wanaandika kweny fom kua "tunapikia kuni na mtazipasua"? Malez ya mzaz yanahusika?

Kuna shule mtoto anapigwa sana kisa hajamaliza ada (kama hukupitia haya huwez kunielewa).

Mtoto hajafikia wastani wa alama kwenye tests za week)mwez atakula fimbo kulingana na masomo atakayo kua amefeli, wewe kama mzaz hapo unahusikaje?
Kwa kifupi makosa yasiyo husiana na malez ya wazaz ni mengi sana na adhabu zake hua n mbaya.
 
Maelezo yako kwa kiasi kikubwa yameunga mkono hoja yangu.
 
Shule yenyewe ni Mandimu unataka mwalimu awe maembe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…