Serikali imehamishiwa Dodoma kwa gharama kubwa, kwanini bado mnatutesa kwa misafara isiyoisha huku Dar? Hamna huruma?

Serikali imehamishiwa Dodoma kwa gharama kubwa, kwanini bado mnatutesa kwa misafara isiyoisha huku Dar? Hamna huruma?

Halafu hawa askari wanaanza kusimamisha magari wakati mwenzao ndo kwanza anapaka wanja.

Kuna haja ya kufanya utafiti kujua misafara hii ya viongozi inasababisha hasara kiasi gani kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] eti anapaka wanja lol.
 
Watanzania bhna!"Eti hamna huruma"?

Yaani CCM washindwe kukuonea huruma ndani ya miaka 60 ya uhuru kwenye suala la huduma ya msingi kabisa ya maji na umeme waje kukuonea huruma kwenye ishue za misafara?

Halafu huenda Mtanzania ndiye binadamu mjinga kuliko wanadamu wote duniani.Serikali ni mtumwa wa wananchi kwa sababu imeajiriwa na wenye nchi ambao ni wananchi.

Sisi ndiyo boss na wao ndiyo waajiriwa kwa sababu sisi ndiyo tunawatuma serikali watufanyie kazi na kisha tunawalipa ujira.

Sasa kati ya boss na mwajiriwa ni nani anapaswa kumuonea mwenzake huruma?Boss anaemtumikisha mwajiri wake au mwajiri anaetumikishwa na boss?Anaepaswa kuonewa huruma ni anaetumikishwa au anaetumikisha?

Wewe kwa akili zako unataka mtumwa amuonee huruma boss.Yaani anaepigwa mijeledi na kulishwa uji(Serikali) ndiye amuonee huruma anaetandika mijeledi(boss).Ni akili za wapi hizi?!
Wee mzee wa chura unaiongelea TZ hii au? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wee mzee wa chura unaiongelea TZ hii au? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dunia nzima principle ni moja,serikali ni mtumwa na wananchi ambao ndiyo wenye nchi ni maboss.

Ukiona Serikali imebadilika na kuwa boss halafu wananchi ambao ndiyo wenye nchi wakawa watumwa basi jua ni sawa na Baba mwenye nyumba amesaliti majukumu yake akaamua kuolewa na mke wake na yeye kuwa mke/mama mwenye nyumba ambapo gharama yake kwa huyo Baba mwenye nyumba ni kubwa sana kwani mke alieoa sasa atakuwa anaingiza wanaume wengine ndani ili kuenjoy maisha.

Ni kama vile sasa Tanzania CCM wanakataza mikutano kwa vyama vya upinzani kinyume na katiba halafu wao wanafanya mikutano kwa rahaa zao.
 
Chanjooooooooo
 
Toa sababu angalau nne kuonesha kwamba halikuwa jambo lenye tija

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
1:Gharama kwa serikali isiyo na sababu.
2:Kwa technology iliyopo mwananchi anatakiwa ajihudumie kokote alipo, mambo ya kwenda katikati ya nchi na mambo ya kale.
3: Usumbufu usio na tija kwa wafanyakazi walio kazini tayari
4: Serikali haikujipanga kwa jambo hilo, ndiyo mana kuna ofisi zingine zilikuwa kwenye mabanda ya mabati
5: Hali ya hewa ya Dodoma siyo nzuri, so hata balozi nyingi zingebaki/zimebaki Dar
 
Back
Top Bottom