Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini mtata anayesakwa na India kutua nchini?

Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini mtata anayesakwa na India kutua nchini?

Kwani wakristo wana hati miliki ya yesu kiasi kwamba hatakiwi kujadiliwa na watu wengine tofauti na wao?
Daaah hii mijadala ya Yesu na Mohamed kuwashindanisha ni upuuzi kwangu. So no time for that dialogue!

With due respect on them, pbut...
 
Muhammad sio mtume wa wote kwa sababu nyinyi hamumtambui na wala kwenye Bible yenu haimtamui.
Lakini kwa waisilam Yesu wanamtambua na Qruan ina mtambua na kwenye uisilam unamtambua mama yake yesu kama mwanamke mtukufu kuliko wanawake wote.
Unasemaje Mohamed sio wa wote na WAKRISTO wakiwemo ila unataka kila mtu amfuate. Kwenye hoja ya kumchambua unakataa, sio wa wote. Kila mtume aliletwa kwa ulimwengu, acheni azungumzwe, achambuliwe. Huyo sio miliki ya dini moja kama alivyo Yesu . Chuki inaanzia hapo na ubaguzi unaanzia hapo.
 
Samahani, wewe hutoi kibali, je serikali za Uarabuni wanaweza kunipa kibali kumhuburi Yesu na kumponda Mohamed??

Ndo maana nimekuuiliza mm ni afisa wa serikali huko uarabuni mpaka uniulize maswali kama hayo?
Kuna sehemu ulisha ona waisilam wana mponda yesu?
Waisilam watampondaje yesu hali ya kuwa ni moja wapo ya manabii wakubwa kwa mujibu wa imani yao?

Humu jf zimejaa nyuzi na comment za kumkashifu Muhammad lakini huwezi kukuta muislam ameanzisha mada za kumkashifu yesu.
 
Unaona ni sahihi dini moja kuzungumzia mambo ya dini nyingine? Au ni bora zaidi kila dini ikajikita kwenye malengo yake mahsusi?
Kumuongelea Yesu ni kuongelea dini nyingine?
Nimesha kwambia Yesu kwenye uisilam ni nabii,kwa hiyo wakristo wakimuongelea Musa au Ibrahim basi wanakuwa wameongelea waisilam?
 
Muhammad anatikiwa afaninishwe na akina mtume Petro au Paulo

Muhammad siyo wa kumlinganisha na YESU KRISTO ni dhambi kubwa sana na mtakuja kuilipia
Umenikumbusha vichekesho vya Max Na Zembwela.
 
Jesus au Yesu kristo ni tofauti kabisa na mtume wao wanaomtambua kama Issa bin Marium. Wao wamulinganishe huyo na mtume Mohamed
Ww huyo yesu ulisha wahi kumuona mpaka ujue kuwa walikuwa tofauti?
 
Daaah hii mijadala ya Yesu na Mohamed kuwashindanisha ni upuuzi kwangu. So no time for that dialogue!

With due respect on them, pbut...
Waisilam hawajawahi kumshindanisha Yesu na Muhammad kwa sababu kwa mujibu wa uisilam wote walikuwa manabii wa Mungu wenye daraja sawa.
 
Kwanini huko malaysia hawapati matatizo mpaka kafika hapa bongo kapita transist ngapi hajakamatwa wacheni kujitia wasi wasi kwa mambo yasiyo wahusu!
Mkuu huyu mleta mada ni mfuasi wa akina Mwamposa, ametumwa alete umbea huu ili huyo mhubiri azuiwe. Kwasabb wanaona sadaka makanisani zitapungua.
 
Unasemaje Mohamed sio wa wote na WAKRISTO wakiwemo ila unataka kila mtu amfuate. Kwenye hoja ya kumchambua unakataa, sio wa wote. Kila mtume aliletwa kwa ulimwengu, acheni azungumzwe, achambuliwe. Huyo sio miliki ya dini moja kama alivyo Yesu . Chuki inaanzia hapo na ubaguzi unaanzia hapo.
Muhammad hawezi kuwa mtume wako hali yakuwa humuamini ili umuamini ni razima uoneshe kwa vitendo na kwa maandiko.

Mfano Paulo hawezi kuwa mtime wa waisilam kwa sababu hawamuamini.

Ibrahim ni ni nabii wa waisilam wa waisilam na wakristo kwa sababu wana muamini lakini hawezi kuwa nabii kwa wahindu na mabudha kwa sababu hawamuamini.
 
Kumuongelea Yesu ni kuongelea dini nyingine?
Nimesha kwambia Yesu kwenye uisilam ni nabii,kwa hiyo wakristo wakimuongelea Musa au Ibrahim basi wanakuwa wameongelea waisilam?
Kumuongelea Yesu ni kuiongelea dini ya Kikristo! Kumuongelea Mtume Muhammad, ni kuiongelea dini ya Kiislam!!

Ukimtukana Mtume Muhammad, umewatukana Waislam! Na vivyo hivyo ukimtukana Yesu umewatukana Wakristo! Shida iko wapi kiasi cha kushindwa kuielewa concept nyepesi kiasi hiki?

All in all, tunawasihi muepukane na chokochoko za kidini. Maana mnapenda sana kulazimisha watu wote duniani kuwa na mtazamo kama wa kwenu, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
 
Utetezi wote huu ni kuzuia na kumlinda Mahamed asiguswe kisije kikanuka, hitimisho ni rahisi. Ukidhani unajua ya wenzako, nao wanayajua yako ila wamenyamaza.
 
Azam kuna mda wanakuaga km wapumbavu
Azam huwezi kuwatenganisha na udini!! Na hili ni jambo ambalo liko wazi kabisa. Hata tamthiliya zao nyingi za Kituruki huwa zina lengo la kuutukuza Uislam wao, huku wakiuponda Ukristo kiaina.

Binafsi huwa ninalipia king'amuzi chao kila mwezi, kwa sababu tu ya kuangalia mechi za Ligi kuu ya Tanganyika. Kinyume na hapo, hata nisingejishughulisha nao kwa lolote.
 
Huyu mtu kaletwa na Islamic foundation, anakuja kuleta mhadhara kuhusu Yesu na Muhammad. Nashangaa mamlaka zinamruhusu vipi mtu wa dini nyingine aje kuongelea Imani isiyomhusu. Azam tv watamweka mbashara wakati uwanja wa taifa umefinguwa kwa matengenezo anaruhusiwa kuja kutumia..
Tukisema serikali ina mwelekeo wa kidini mtabisha? au Azam Wana mwelekeo wa kidini mtabisha?
 
Huyo muhubiri apigwe marufuku,ni moja ya mawakala wa ugaidi,tuwe makini nae kukaribisha watu kama hawa nchini ni kuleta mtafaruku hasa ukizingatia mada yake imekaa kichochezi na leo ovu nyuma yake.
Tatizo ni wanasiasa wengi walio madarakani wana mitizamo na mielekeo ya udini
 
Kumuongelea Yesu ni kuiongelea dini ya Kikristo! Kumuongelea Mtume Muhammad, ni kuiongelea dini ya Kiislam!!

Ukimtukana Mtume Muhammad, umewatukana Waislam! Na vivyo hivyo ukimtukana Yesu umewatukana Wakristo! Shida iko wapi kiasi cha kushindwa kuielewa concept nyepesi kiasi hiki?

All in all, tunawasihi muepukane na chokochoko za kidini. Maana mnapenda sana kulazimisha watu wote duniani kuwa na mtazamo kama wa kwenu, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Mkuu usicho kielewa ni kipi hapo?
Yesu ndani ya uisilam anatambulika kama nabii hivyo akiongelewa ataongelewa kwa mkitadha wa unabii wake kwa mujibu wa Quran kama wanavyo ongelewa manabii wengine.
Huwezi kuwakataza waisilam kumuongelea nabii wao.

Lakini nyinyi wakristo hamuwezi kuwa na haki ya kumuongelea Muhammad kwa sababu hamumtambui na wala kitabu chenu hamumtambui.

Nabii pekee ambaye ikimgusa moja kwa moja una kuwa umeugusa ukristo ni Paulo kwa sababu yeye ndo aliye uhasisi ukristo, Yesu hakuwahi kuuhasisi ukristo na mpaka ana kufa hakuacha dini inayo itwa ukristo.

Kwahiyo kuanzia sasa waisilam waache kuwaongelea akina Ibrahim,Isahaka,Musa ,Daudi kisa na wakristo wana watambua kama manabii?
 
Wewe Kafiri acha kutema matapishi hapa kwa chuki za kijinga,

Hao mitume wenu mbona hua hulalamiki?

Yule Kiboko ya wachawi kutoka DRC aliwapiga hela watu kisha akarudi kwao na kuwacheka ulitoa hili povu?

Mwaka 2020 kule Moshi walikufa watu 20 wakigombania kupaka mafuta ya upako,ulitoa hili povu? hao mitume wenu kila siku wanajaza watu na kuwauzia udongo na mafuta,mbona hua upo kimya?
Hao wote uliowataja wote fake tu na mkristu anaejielewa hawezi kuwasapoti.

Lakini, shida ya huyo shekhe Dr. Zakir Naik ni kuwa anafuga majin mengi sana takribani elfu 80 Mpaka India ilibidi wamkimbize, sasa nani anataka aje nayo huko bongo, jamani tutapata shida nani anataka hizo shida ?
 
Nimeona tangazo la Dr. Zakir Naik anayetafutwa kufikishwa mahakamani na mamlaka za nchi yake ya India tangu mwaka 2016 kwa makosa ya ugaidi, utakatishaji fedha na kauli za chuki kuwa nchini wiki ijayo kwa shughuli za kidini.

Hili jambo tumepima kama halitatuleta shida zinazoepukika na utata usio wa lazima na India ambao ni marafiki zetu wakubwa na washirika muhimu wa kibiashara na maendeleo?

View attachment 3187483

Naona umepindisha kidoogo story yako ilitakiwa isomeke hivi , "

"Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini anayesakwa na India kwa kuwasilimisha wahindu na wakristo wengi kwa hoja zilizo wazi kutua nchini? "​

Huyo ni mwanafunzi wa ahmed deedat (Allah awe radhi naye) ni moja ya mada'i wakubwa mno duniani amefanys ziara nchi nyingi sana kulingania dini na Allah (the almighty) amejaaliia yeye kuwa sababh tya mamilionj ya wahindu , wakristo na wabudha kuupokea uislamu kwa hoja zilizo wazi kabisa.

Huyu mwamba amehifadhi QURAN, BIBLIA , VEDAS , UPANISHAD na vitabu vengine va uhindu, pia ni msomi wa Afya ya mwili wa binadamu , hii inawafanya watu wengi washindwe pa kumbana na maswali maana Allah (the almighty) amemjaalia kipawa kama hicho anakupiga na hoja za kitabu chaako mwenyewe 🤣 achana na wakina mazinge.

Halafu kama haujui tu mbona alishafika Tanzania 2017 na akafanya ziara yake kisha akaondoka na mwaka kesho ndo anarudi tena so hii si mara yakee ya kwanza .

N.B
Mwalimu wake Ahmed deedat (Allah awe radhi naye) naye alikuwa da'ai na aliwahi kum challenge papa john paul II kwenye mdahalo wa kidini na akamwambia papa achague ukumbi anaotaka yeye na atalipia gharama zote ila sharti kila kitu kirikodiwe na kisambazwe ulimwenguni Papa akachomoa , enzi zake ndo kulikuwa na miamba wa kikristo si sasa hivi kuwataja wachache

1. Reverend jimmy swaggart
2. Reverend anis shorosh
3.Reverend stanley sjoberg
4.Reverend eric bock
5. Pastor robert douglas
6. Reverend john gilchrist
7. Professor floyd E. Clark
8. Pastor R.P.D Green
9. Pope john paul II ( Aligoma mdahalo)
10. Billy graham (Aligoma mdahalo)
 
Back
Top Bottom