Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini mtata anayesakwa na India kutua nchini?

Serikali imejipangaje kidiplomasia kumruhusu mhubiri dini mtata anayesakwa na India kutua nchini?

Nimeona tangazo la Dr. Zakir Naik anayetafutwa kufikishwa mahakamani na mamlaka za nchi yake ya India tangu mwaka 2016 kwa makosa ya ugaidi, utakatishaji fedha na kauli za chuki kuwa nchini wiki ijayo kwa shughuli za kidini.

Hili jambo tumepima kama halitatuleta shida zinazoepukika na utata usio wa lazima na India ambao ni marafiki zetu wakubwa na washirika muhimu wa kibiashara na maendeleo?

View attachment 3187483
Siamini tumekua careless namna hii
 
Jibu limepatikana. Huyo mhubiri anakuja kutafuta wakristo awasilimishe. Lakini Uarabuni ni marufuku mkristo kumhuburi hata tu kumtaja Yesu. Chuki, mauaji ugaidi na uislam ni Pete na kidole.
Kwani tanzania ni ukristoni?!
 

Attachments

  • Screenshot_2024-12-29-14-09-42-158.jpg
    Screenshot_2024-12-29-14-09-42-158.jpg
    342.9 KB · Views: 1
Nimeona alivyopigwa maswali nchini Kenya, muhubiri Dr. Zakir Naik amepanick sana, ana dharau kwa wauliza maswali, anadharau elimu ya wauliza maswali, anadharau ya asili ya mtu, anadharau na imani ya mtu ... ni mtu anayelenga kukosoa imani ya mtu na siyo kuhubiri imani yake anayoamini ..

26 December 2024
Nairobi, Kenya

Lecture : Prophet Muhammad in the Bible - Dr. Zakir Naik | Talk + Q&A | Kenya, East Africa

View: https://m.youtube.com/watch?v=C4jvfQRrXg8

Imani haihojiwi. Kinachohojiwa ni fact.

Ukishahoji imani ushakosea.

Imani imewekewa kinga ya kutohojiwa kikatiba na pia kama sehemu ya haki za binadamu.

Kila siku ninapotaka uthibitisho wa kuwepo Mungu hapa nahoji fact, si imani.

Kwenye imani ingawa mimi siamini Mungu yupo, ila nitatetea watu wanaoamini Mungu yupo waweze kuamini hivyo bila kuhojiwa.
 
Midahalo ya wale mitume na mikesha ya maombezi kwa Mkapa inaruhusiwa ila kwa huyu mhindi ukakasi unatoka wapi? Atahubiri kama wale wazungu wengine tu tuwe wavumilivu
Hujitambui mkuu japo sisapoti hii movement ya wana JF. Hiyo ya wazungu na mitume sio midahalo mkuu ni mahubiri. Unaposema midahalo unamaanisha kuna pande mbili zinao debate mkuu.

Pia wazungu, mitume na mikesha ya maombezi haitaji dini wala kujihusianisha na dini nyingine bro. Ukishasema Yesu unamaanisha Ukristo. Ni bora wangeandika kwenye tangazo lao Muhammad V/S Issa hiyo isingewahusu watu wa dini nyingine.

Nafikiri ndio hoja ya wengi japo mi binafsi sioni shida katika hilo mkuu.
 
Imani haihojiwi. Kinachohojiwa ni fact.

Ukishahoji imani ushakosea.

Kioa siku ninapotaka uthibitisho qa kuwepi Mungu hapa nahoji fact.

Kwenye imani ingawa mimi siamini Mungu yupo, ila nitatetea watu wanaoamini Mungu yupo waweze kuamini hivyo bila kuhojiwa.
Hongera umeandika kitu kizuri mkuu. Hili sikuwa nalijua.
 
Mimi shida yangu iko sehemu moja tu; Jesus anahusika vipi na hiyo shughuli yao?
Na hii ndio hoja ya watu wengi pia tangazo lao kisema Muhaamed Vs Jesus.

Nifahamuvyo ukishasema Yesu inaihusanisha na dini ya Kikristo. Ingekuwa Muhammed VS Issa isingeleta shaka. Mashaka ya wengi yapo hapo.
 
Issa kiarabu, kiswahili yesu,nyie mna husda sana na chuki, yaani mnazungukazunguka hamueleweki hamtaki nini,si muende mkam-challenge kama mnajiamini sana,midahalo ya kisiasa mnaitaka ya dini hamuitaki
 
Issa kiarabu, kiswahili yesu,nyie mna husda sana na chuki, yaani mnazungukazunguka hamueleweki hamtaki nini,si muende mkam-challenge kama mnajiamini sana,midahalo ya kisiasa mnaitaka ya dini hamuitaki
Acha kudanganya. Hakuna kiarabu kinachosema Issa bi Yesu mkuu. Ukiacha Quran vitabu vyote vya kiarabu hakuna Issa badala ya Yesu.

Kimsingi sijui watu wanahofu ya nini humu JF japo mleta mada hajasema hayo unayoyaleta wewe na wengine, yeye ameongelea kwenye angle ya Diplomasia
 
Mnapenda kujitia hofu,huyo kishafika,kama una swali kamuulize

Dr. Zakir Naik ni muhubiri muoga sana akipigwa maswali magumu kama alivyopigwa maswali hapo Nairobi.
Na kizuri nchini Kenya lugha waliyotumia katika mdahalo ni kiingereza na hadhira inafahamu kiingereza pia jukwaa walilotumia ni la eneo local siyo kitaifa kupitia kituo cha televisheni cha kitaifa kama Azam TV.

Lakini kwa Tanzania kuna ajenda maalum kuzidi zile za Sheikh Mazige, Sheikh Mwaipopo n.k sasa kundi la Dr. Zakir Naik badala ya kutumia jukwaa online TV au ukumbi wa Diamond Jubilee au uwanja wa Benjamin Mkapa huyu muhubiri anataka kwa udi na uvumba kutumia jukwaa la kitaifa la Kituo tajwa cha televisheni kuingia katika kila sebule ya nyumba ya raia mtanzania kupitia kituo kikubwa kabisa cha kurushia matangazo ya televisheni cha Azam TV.

Nadhani haijawahi kutokea Tanzania kituo kikubwa kabisa cha Televisheni nchini ngazi ya taifa kikatumika ku test ukweli ya mitume, imani, biblia, Quran, Hadithi n.k kwa upande mmoja wa imani kujikita kusema kuwa kuna mapungufu kati imani inayotumika msikitini, kanisani, hekaluni au katika kusanyiko lao.

Siku zote katika jukwaa la kitaifa kupitia chombo cha umma kikubwa kama Azam TV, ITV n.k hutumika kuswalia, kusali, kuhubiri yale ya imani zao na siyo mashambulizi kuelekezwa imani nyingine.

Hii ni historia au precedent mpya inajaribu ku najengwa kwa chombo umma cha kitaifa kutumika kushambulia imani ya dini, dhehebu na mitume yao pia vitabu vya imani nyingine.

Kufanyika mdahalo Diamond Jubilee, online TV isiyo ya kitaifa, uwanja wa wazi Benjamin Mkapa hiyo siyo shida ila serikali kuruhusu vyombo vikubwa vya umma vya kitaifa kama Azam TV kuwa jukwaa la imani mmoja kushambulia imani nyingine siyo sawa.

Hii ya chombo cha mawasiliano cha kitaifa Tanzania kutumika kushambulia imani nyingine, ni sawa na Radio ile ya Rwanda radio RTLM ilipotumika vibaya WaTutsi kushambuliwa kwa propaganda na Wahutu au wengine kisha historia ikatuambia 1994 ilifikia hitimisho jamii hizi za Rwanda kupata mihemuko na kuleta Maafa ya 'vita ya makundi' ikaishia Mauaji ya Kimbari.

Radio Télévision Libre des Mille Collines (RTLM) nicknamed "Radio Genocide" or "Hutu Power Radio", was a Rwandan radio station

Wewe unawakilisha kundi la watu wanaokurupuka. Umechukua sehemu tu ya mada badala ya kuandika mada yote
"Jesus & Muhammad, peace be upon them, brothers in faith" Yani
"Yesu & Muhammad, amani iwe juu yao, ndugu katika Imani". Hadi hapo kwanza hakuna tatizo lolote.

Pili Waislamu wanaamini kuwa Yesu na Muhammad wote ni wajumbe wa Mungu. Wewe hapo shida yako hasa ni ipi?

26 December 2024
AZAM MEDIA LTD PAMOJA NA THE ISLAMIC FOUNDATION …


UJIO WA DR ZAKIR NAIK TANZANIA - RATIBA YAKE YOTE

View: https://m.youtube.com/watch?v=PLO0zcQm7ok

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA WANAKULETEA MHADHIRI MASHUHURI WA KIMATAIFA , DKT ZAKIR NAIK AKIAMBATANA NA MWANAE SHEIKH FARIQ NAIK KATIKA MDAHALO WA MASWALI NA MAJIBU :

TAREHE 31/12/2024 MSIKITI ZINJIBAR, UNGUJA ZANZIBAR KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA


TAREHE 2/01/2025 DIAMOND JUBILEE DAM KUANZIA SAA 1 USIKU HADI SAA 6 USIKU

TAREHE 5/01/2025 BENJAMIN MKAPA STADIUM UWANJA WA TAIFA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA


MATANGAZO HAYA YATAKUJIA LIVE - MUBASHARA KUPITIA CHANEL YA ZBC2 WEMA UNAOENDELEA


PIA TUTAKUWA MUBASHARA KATIKA DUA TV AOMBWAE NI MOLA PEKEE JESUS AND MUHAMMAD PEACE BE UPON THEM BROTHERS IN FAITH

1735472268416.jpeg

1735472302602.jpeg

1735472337296.jpeg
 
Mwafrika bado ana safari ndefu sana kujitambua.

Karne ya 22 watu bado wanafikra kama vile elimu ni siri....!
 
India ni nchi ya wahindu, waislam ni chini ya Milion 300 katika watu Bilion moja na nusu, na kuna chuki kubws ya wahindu kwa waoslam, kwa Dr. Zakir Naik kupewa kesi ya ugaidi ni issue ya kisiasa tu haimaanishi kwamba kweli ni Gaidi ni kama kesi ya Ugaidi ya Mbowe na Nelson Mandela ilivyokuwa, huyu ni mhubiri wa Dini ni mtu wa midahalo, anaishi Malaysia na wala hakuna Diplimatic Querels baina ya India na Malaysia kwasabab yake. Tanzania ni nchi ambayo haina dini ila wananchi wake wana dini na wana uhuru wa kuabudu. Zanzibar ni nchi ya waislam wengi, kwa Dr. Zakir Naik kufika huko haipaswi kuwa agenda kubwa ya kushupaza shingo. Kila mtu ana uhuru wa kuabdu na kufuata anachoona ni sahihi, kama mijdala ya huyu Dr. Zakir haikuvutii au inakukera haipaswi kukushughulisha kama ambavyo mie niliachaga kumfuatilia.
Na uwanja WA mkapa tar 2 ni Zanzibar!
 
Kusikia muhubiri wa kiislam anakuja,chuki zimewajaa kama zote,
Kila siku wachungaji kutoka nje wanakuja ila huoni hili povu,

Yule Kiboko ya wachawi alitoka DRC akawapiga hela kisha akarudi kwao kuwacheka ila wala hawaoni tabu,kule moshi walikufa wato 20 kwa kukanyagana wakigombea kupaka mafuta ila hatukuona hili povu.
Tatizo heading ,Jesus anahusu nini?
 
Kusikia muhubiri wa kiislam anakuja,chuki zimewajaa kama zote,
Kila siku wachungaji kutoka nje wanakuja ila huoni hili povu,

Yule Kiboko ya wachawi alitoka DRC akawapiga hela kisha akarudi kwao kuwacheka ila wala hawaoni tabu,kule moshi walikufa wato 20 kwa kukanyagana wakigombea kupaka mafuta ila hatukuona hili povu.
Hata mi binafsi sioni shida hadi mapovu kutoka mengi hivi.
 
Back
Top Bottom