KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mawazo ya waziri wa fedha ni finyu sana kama mtu wa diploma tuu. Ni kweli lengo ni Zuri kuongeza makusanyo ya kodi. Lakini swali langu kwanini mzigo mkubwa unabebwa na wachache??? Kama lengo ni kupata kodi kupitia hiyo ya makato ya umeme nyumba zenye umeme ni kama 1/3 ya nyumba zote Tanzania sasa kwanini asije na sera ya kila nyumba lazima iwe na umeme ila akusanye kodi kubwa?? Jamaa ana PhD ila namuona kama ana diploma tuu. Hana ubunifu
 
Hii ni dharau kubwa sana kwa wananchi mimi naipenda CCM ila kwa hili hapana.angalau wananchi tungepewa taarifa.
 
Mama anaupiga mwingi sana
 
Sh 9000 unapata unit 57? Ni umeme upi huo? Zanzibar au Rea?
 
Sasa Msigwa Alipofika Bei Pesa Zinatakiwa Zitoke Huko Alipwe
CCM Haina Aibu
 
Sasa kwa nini wasitoe taarifa kwa umma watu wakajua nini kinaendelea, hii nayo ni taharuki kwa wananchi. Watu wanaichukulia jero kimasihara sana hawa.
 
Shida ya watanzania ni moja tuh, wanaopenda kufanya maandamano hewa yaani ya mtandaoni tuh.

Twende Kwenye uharisia pesa za wa Tanzania Kwenye nyumba tu mfano tuna nymba milioni kumi zenye umeme maana yake Kwa buku tu wanakusanya bilioni kumi Kwa mwezi.

Ukija Kwenye matozo mengine ni mamia ya mabilioni Kwa mwezi.

Je kama tunakopa pesa za ndani hizi zinaenda wapi??
 
There are news circulating that the Property Tax has been increased and now Tanesco after these monthly deductions will be paying the Municipal directly?
 
Kama hamtaingia barabarani hamna jambo litafanyika. Shauri yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…