KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
wakuu mbona mimi wamenikata zaidi inamaana wamenifanya ng'ombe wao wa maziwa. wamenikata elfu 6 serious?
Screenshot_20240701-200627.png
 
Mwezi wa 6 ulinunuwa umeme? Isije kuwa unadaiwa kodi ya miezi miwili.

Umeongea Point sana Dr.

Wanasema kwamba Tar 26 July 2023 Serikali ilipandisha kodi kutoka 1000 hadi 1500 ,kwahiyo kama walinunua umeme kati ya tar 1 hadi 25 July 2023 basi kuna deni la 500/= Tsh ,kwahiyo mwaka Mpya wa Serikali umebadilika leo tar 1 July 2024 ,kama una deni la 500 basi litajumlishwa na 1500 na kuwa 2000 kwa Mwezi huu wa July ,ila mwezi ujao ukinunua LUKU utakatwa 1500 kama kawaida ,hayo ni Maelezo ya TANESCO wenyewe baada ya kubananishwa na wadau kwanini bei imepanda.
 
Malipo yamekamilika 54258576457
9001241831819325017
2.4KWH

3706 2135 9107 0844 7144

Cost 713.94
VAT 18% 128.50
EWURA 1% 7.14
REA 3% 21.42
Debt Collected 2000.00
TOTAL 2,871.00
 
Mimi makato ya ATM NMB ndio bado sijayaelewa kabisa, kutoa laki tatu kwenye ATM nakatwa 7500?

Hawa Jamaa wanatuibia sana ,leo kuna jamaa alikuwa na emergence akata nimtumie elfu 17 ,nikatoa BANK kwenda kwenye simu yake aiseee wamenikata Buku 2.....Huu wizi sijui kama BOT wanajua.
 
Haya maisha ya samia mbona mabaya sana
 
Lakini CCM mnatuonaje yaani

Mnatuona kama manyani siyo?

Mnateka kila anayekuwa kinyume nanyi

Mkishaweka kodi ya kuumiza wananchi, mnajipanga kuwafuatilia wanaolalamika ili kuwadhibiti kwa nguvu

Mnatuonaje yaani? Mnatuchukulia kana kwamba mmetuumba na mko huru kutuvuna mtakavyo kwa sababu mnajiona mpo kwenye nafasi ya Mungu siyo?

Umeme umekuwa anasa kwa wananchi badala ya wananchi wafurahie matunda ya kodi zao wanazokuwa wakilipa ili kujengwa kwa JKNHP siyo?

Mmezifanya Maliasili za nchi hii kuwa mali zenu binafsi, na ndiyo maana hamuwezi kutengeneza kodi kutoka huko, mmezigawana nyinyi kwa nyinyi huku mkiwarundikia kodi wananchi ilihali mkijua kabisa wapo hoi tabani kiuchumi na wengi wao wanakula mlo mmoja kwa siku! Hawana uwezo wa kusomesha watoto wao kwenye shule nzuri mnazosomesha watoto wenu, hawana uwezo wa kutibiwa kwenye hospitali mnazotibiwa nyinyi! Hata hivyo Mungu ni fundi! Anakufa masikini na tajiri pia!

Mmewatengenezea matabaka, watoto wao wanasona shule ambazo baada ya hapo wanapata ajira za hadhi yao ili hali nyinyi mkimega keki na vijana wenu kwa raha zenu

Hii ni dhambi kubwa sana muifanyayo!

Tuendako kunazidi kusogea karibu na asubuhi!

Mungu ibariki TANZANIA

Mungu utupe viongozi wanaoumizwa na hali mbaya za wananchi!
 
Back
Top Bottom