KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Malipo yamekamilika 54258576457
9001241831819325017
2.4KWH

3706 2135 9107 0844 7144

Cost 713.94
VAT 18% 128.50
EWURA 1% 7.14
REA 3% 21.42
Debt Collected 2000.00
TOTAL 2,871.00
Wabongo tuna maisha magumu sana, hii ni sample tu.

Mimi kwangu natumia umeme wa sh 70,000/= kwa mwezi.

Hizo unit 2 labda iwe dharura tu ya kupitisha usiku.
 
Hiyo siyo bei ya umeme, ni kodi ya jengo.

Kama unaishi nyumba ya kupanga na una mita ya peke yako maana yake unamlipia kodi mwenye nyumba.

Hawa mwisho wao hauko mbali, Mungu amewatia upofu hawataamini ikifika punda anapogoma.
Una mikwala mingi mingi
 
Hii nchi ilipofikia inahitaji maandamano kama ya Kenya, ukipandisha hii maana yake kodi ya nyumba nayo imepanda, ilipandishwa na nani?
Umeme wenyewe kama hivi ghafla tu umekatika watu tunaangalia Taarifa za habari baada ya kutoka makazini na kwenyewe hali sio rafiki unasema upumzike kidogo unajikuta gizani hivi ni nani wa kutukomboa na kadhia hii?kiukweli hali sio shwari kabisa Mungu atutie nguvu ila tulipo hapavumiliki kiukweli sema tu ndio hakuna namna unaweza kujikuta unalala kwenye karakana na kuamkia Arusha kisha Ukatalii hifadhini Katavi ila Mungu anawaona
 
Leo kanunua umeme wa buku mara mbili hakupewa token ndo mana kakasilika mtoa mada😂😂😂
 
Hawa Jamaa wanatuibia sana ,leo kuna jamaa alikuwa na emergence akata nimtumie elfu 17 ,nikatoa BANK kwenda kwenye simu yake aiseee wamenikata Buku 2.....Huu wizi sijui kama BOT wanajua.
Yaan Mimi ilibidi ni note kabisa kiasi Cha pesa kilichosalia bank baada ya siku ya kwanza kuhisi makato ni makubwa sasa Jana ndio naenda kutoa fedha nikagundua 7500 imekatwa kutoa 300,000
 
Kwa sasa makato ya kodi unaponunua LUKU yameongezeka kutoka TZS 1,000 mpaka TZS 2,000.

Tunaomba maelezo kwanini gharama hizi zineongezeka? Kuna sababu gani ya kuendelea kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu ili hali mabwawa ya umeme yaliyotumia matrilioni ya kodi za wananchi yameshafunguliwa?

Je, kodi wanazotozwa wananchi bado hazitoshi? Je, mmeshindwa kutumia rasilimali zilizopo nchini, kuna madini, maliasili na vivutio mbalimbali vya utalii n.k pamoja na vyanzo hivi vya mapato, serikali imeshindwa kuwa bunifu na kutegemea tozo na kuendelea kunyonya na kufanya maisha ya watanzania yazidi kuwa magumu?

Hali hii itaendelea mpaka lini?

View attachment 3030797
Lakini ilikopunguza Kuna nafuu zaidi ya hiyo jero.

Sema imeongezwa sehemu ambayo inaleta kero Kwa watu
 
Ipo siku Tu....mjuaji atajulikana...hasira zikipanda, Malawi nayoyatakatwa...mpk mizizi yake...ENDELEA Kuwanyonya wananchi ili wajukuu wako waishi Kwa neema..
 
Kenya hali ni mbaya sana.. hawa jamaa (CCM) hawana budi kujifunza.
 
Back
Top Bottom