Lakini CCM mnatuonaje yaani
Mnatuona kama manyani siyo?
Mnateka kila anayekuwa kinyume nanyi
Mkishaweka kodi ya kuumiza wananchi, mnajipanga kuwafuatilia wanaolalamika ili kuwadhibiti kwa nguvu
Mnatuonaje yaani? Mnatuchukulia kana kwamba mmetuumba na mko huru kutuvuna mtakavyo kwa sababu mnajiona mpo kwenye nafasi ya Mungu siyo?
Umeme umekuwa anasa kwa wananchi badala ya wananchi wafurahie matunda ya kodi zao wanazokuwa wakilipa ili kujengwa kwa JKNHP siyo?
Mmezifanya Maliasili za nchi hii kuwa mali zenu binafsi, na ndiyo maana hamuwezi kutengeneza kodi kutoka huko, mmezigawana nyinyi kwa nyinyi huku mkiwarundikia kodi wananchi ilihali mkijua kabisa wapo hoi tabani kiuchumi na wengi wao wanakula mlo mmoja kwa siku! Hawana uwezo wa kusomesha watoto wao kwenye shule nzuri mnazosomesha watoto wenu, hawana uwezo wa kutibiwa kwenye hospitali mnazotibiwa nyinyi! Hata hivyo Mungu ni fundi! Anakufa masikini na tajiri pia!
Mmewatengenezea matabaka, watoto wao wanasona shule ambazo baada ya hapo wanapata ajira za hadhi yao ili hali nyinyi mkimega keki na vijana wenu kwa raha zenu
Hii ni dhambi kubwa sana muifanyayo!
Tuendako kunazidi kusogea karibu na asubuhi!
Mungu ibariki TANZANIA
Mungu utupe viongozi wanaoumizwa na hali mbaya za wananchi!