KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

KERO Serikali imeongeza tozo LUKU kutoka Tsh 1,500 mpaka Tsh 2,000 kimya kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hiyo ni kodi ya majengo, na haikuwa 1000, ila ilikuwa 1,500 na sasa ni 2,000 na mwaka ujao wa fedha itakuwa 2,500 bila shaka.

Ubaya wa kodi siyo tu huko kupanda kwake, ila kutozwa kwa mfumo wa wizi, kwamba haitozwi kwa jengo kama inavyopaswa, ila kwa mita ya Luku.

Hivyo, kama jengo moja lina mita tatu za Luku, basi jengo hilo litalipiwa kodi hiyo mara tatu, ambayo kimsingi ni wizi. Kwani hata wenye msamaha wa kodi, wanakatwa tu.

Ova
 
Hilo ni tatizo si luku hata kwenye huduma za kuangalia bank Kwa mobile ni wizi umekithiri unakuta unafungua kuangalia balance unakatwa 100 halafu unajibiwa network error Kwa kweli ni wizi uliopindukia mipaka kabisaa Kwa hii nchi,mnamiliki Rasilimali nyingi ikiwemo maporomoko ya kuujenga mabwawa ya kufua umeme baada ya kuwa nafuu Kwa wananchi inakuwa maumivu kama tunachokiona hapo,gas nayo juzi tu inapandishwa mpaka unajiuliza kimiliki Rasilimali zilizopo ndio tupate tabu hivi unakosa jibu.
 
Kuongoza hii nchi ni rahis sana.
Leo watu wameandamana kumpokea Chama, vijana wengi issue za msingi zinazohusu mustakabali wao hawajali kabiisa...betting, ushabiki wa mpira kuanzia asubuh, gudugudu, pool na vitu vingine vya ovyo kabisa.
 
Ni elfu 2000 kweli aisee.
超级截屏_20240701_200405.png
 
Back
Top Bottom