Nimeshangazwa na maoni ya watu wengi. Lakini Mimi ninaamini Mzee Mahita kakosea, labda kama ana matatizo ya akili. Na kama ana matatizo ya akili wa kulaumiwa ni waliomruhusu mgonjwa kumiliki silaha.
1. Kuwa IGP hakumfanyi mtu kuwa juu ya Sheria. Labda kama ile kauli ya TII SHERIA BILA SHURUTI ni kwa watu fulani fulani tu.
2. Mahita ni kiongozi. Kiongozi anapaswa kuishi maisha ya kuigwa na wengine. Kama ambavyo mtoto huiga kwa wazazi wake, kadhalika na maofisa wa ngazi za chini. Alichokifanya kinaweza kuwa hamasa kwa maaskari wa ngazi za chini kuiga.
3. Mahita anafahamika. Kama alichotendewa ni kinyume cha Sheria, angeweza kuwapigia viongozi wakubwa kama Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP, RPC, OCD, n.k., na suala lake lingeshighulikiwa kwa heshima. Hilo lisingemfanya aonekane dhaifu bali mstaarabu.
4. Kati ya sifa muhimu kwa kiongozi ni kuwa na uwezo wa kuthibiti hisia zake. Naamini anafahamu kuhusu emotional intelligence. Mtu mwenye kuwezo wa kuthibiti hisia zake asingefanya maamuzi kama hayo.
5. Makonda alipokuwa RC wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, wamiliki wote wa silaha mkoani kwake wazipeleke Polisi kwa ukaguzi. Miongoni mwa walioitikia wito wale ni John Magufuli.
Utii waagufuli haukumaanisha kuwa alikuwa akimwogopa Makonda, bali alionesha vile kiongozi anavyopaswa kuwa. Ukitamka kujua soda halisi ya mpeojawapobya hivi: fedha au madaraka. Mwenye inferiority complex akipata mojawapo ya hivyo huweza kugeuka kuwa tabu kwa watu wengine. Mzee Mahita kaonesha mfano mbaya kiasi chatu kuweza kuhoji kama hiyo nafasi aliipata tu kwa bahati au alistahili?
6. Watu wanadai kuwa gari la Mahita halilazimiki kuzingatia Sheria za parking kwa kuwa ni IGP mstaafu. Labda cha kujiuliza, huo IGP alikuwa analizwa au alikuwa anatoa msaada? Mbona nafasi kama hizo zinatamaniwa na wengi ila tu hawabahatiki kupewa?
Mahita hakuwa akitoa msaada. Alikuwa mwajiriwa wa uma na alikuwa akilipwa kwa Kodi za Watanzania. Anapaswa kuwaheshimu hata kama ni watu wanyonge kwake. Ajue ni hao wanyonge ndiyo waliompeleka yeye kufikia cheobcha IGP.
7. La mwisho, wengi wa waliochangia wanaonekana kama ama wametawaliwa na hofu au pengine hawazijui hata haki zao kama raia. Hofu haisaidii. Hofu huzuia akili kufanya kazi kwa ufasaha.
Kwa ufupi, Mimi naamini kuwa IGP mstaafu, Omari Mahita kakosea. Kafanya jambo lisilo la kistaarabu. Kama alikuwa amekosewa, angelishighulikia hilo kwa hekima kama impasavyo kiongozi msomi, makini na mstaarabu. Na hata kama alikuwa amekosewa, angeonesha mfano kwa kunyenyekea japo anajua huyo kijana asingeweza kumfanya chochote.
Hayo yangeshindikana, ndipo angewapigia wakubwa simu ili waje kumshughulikia huyo kijana.