Kwa nchi zetu hizi za kujuana sana.
Kufunga lock gari ya IGP mstaafu ni kujitafutia matatizo tu. Huyo mfunga lock ni mpumbavu pia.
IGP mstafu huwezi kwenda kumshitaki popote ukamshinda.
Atakuwa mpumbavu tu kama alichofanya kinakinzana na mwongozo wa kazi yake. Lakini kama alilofanya ni hitaji la Kisheria, basi anastahili pongezi. Ameiheshimu kazi yake na ameukataa unyonge.
Miaka ya nyuma, kulikuwa na utaratibu wa ulinzi shirikishi maarufu kama sungususungu mkoani Arusha.
Siku moja, wakati vijana waliohitimu mafunzo ya mgambo wakiwa kwenye doria, waliliona gari linakuja na mmoja akalisimamisha. Hilo gari halikusimama mahali lilikopaswa, lilienda kama mita hamsini mbele zaidi ndipo likasimama.
Kumbe gari lilikuwa la wanajeshi (JWTZ). Kitendo cha kufahamu kuwa wamelisimamisha gari la Jeshi, wanasungusungu wote isipokuwa mmoja walikimbia na kutokomea machakani. Mwenzao kwa ujasiri kabisa, huku akijua alichokuwa akikifanya, alilifuata hilo gari na kuwaamuru wote waliokuwemo washuke. Waliposhuka tu, aliwaamuru waanze kuruka kichura kwa kosa la kutokusimama kwenye kizuizi. Kama vile maigizo, masoja walitii walichoamriwa. Baada ya kuruka hatua chache, aliwaamuru warudi kwenye Lori lao na kisha kuondoka.
Inawezekana hao Askari walitii kwa vile walikuwa na mkubwa wao. Huyo mgambo alionesha ujasiri wa hali ya juu kwa kuwatendea wanajeshi vile walivyomfundisha alipokuwa kwenye mafunzo ya mgambo.
Kesho yake, wanajeshi wakiwa kwenye Land Rover ya Jeshi walienda eneo husika kumtafuta huyo mgambo. Wenzake waliposikia, waliamini kuwa mwenzao kayatimba, kumbe ni kinyume chake.
Alienda kupongezwa kwa ujasiri aliouonesha, Jana yake Usiku na akaishia kupewa ajira Jeshini.
Huyo aliyelifunga gari la Mahita hakukosea kama alichofanya ni matakwa ya Sheria. Aliyekosea ni Mahita. Alichofanyiwa kilikuwa ni fursa ya kuonesha hekima yake au upumbavu wake.
Nina mashaka kama alichokionesha ni hekima.