Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

Maliyamungu mnyima watu haki ya kuishi ndo mshika remote ya TV
 
Nasikia mtaalam wake kwenye mambo ya anga,anaogopa kuangushwa hvyo mtasubiri sana
 
Tatizo ni pale unapouliza Magufuli anakwama wapi kwa huyu Makonda, wakati Magufuli hajawahi kuwa na consistent and coherent agenda popote.

Hapa atakwambia anapiga vita rushwa, kule kauza nyumba za serikali nje ya utaratibu mpaka kwa hawara zake. Pia anasema trafiki kupewa rushwa ni "hela ya kupiga viatu brashi tu".

Hapa atakwambia yeye ni rais wa wanyonge, na maendeleo hayana vyama, pale atakwambia atapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Hapa atamfukuza kazi Kangi Lugola kwa kupiga dili ambalo halijapitia bungeni, kule atanunua ndege bila idhini ya bunge, tender ya wazi wala kuruhusu ukaguzi wa CAG ATCL.

Hapa atasema anawakilisha maslahi ya wakulima wanyonge, halafu hapo hapo ataingilia manunuzi ya korosho na kuharibu soko kwa namna ambayo inaangusha mapato ya mazao ya kilimo kwa asilimia 55 katika mwaka mmoja tu unaoishia Agosti 2019, kwa mujibu wa ripoti ya Bank of Tanzania ya Oktoba 2019.

Sasa mtu kama huyu utategemea vipi ajielewe zaidi ya wholesale politics?

Na watu waliokuwa sane serikalini waliotaka kummdhibiti Makonda na kufanya "damage control" kama kina Dr. Mahiga ndiyo wanaondokewa kwenye prominence. Go figure.

Wizara ya Mambo ya Nje sasa hivi tungehitaji sana watu wenye busara na uzoefu wa kimataifa. Lakini wameondolewa, wamewekwa die hard ideologues waimba sifa. Clear mesage kwamba hatutaki watu wa busara, tunataka watu wa kujikomba kwa mkuu.

For all I know yeye Magufuli na Makonda hawajapishana sana katika kufikiri, na sasa wanaandaa vita dhidi ya "mabeberu".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna Rais wa hovyo haijawahi kutokea!
 
Atumbuliwe kwa kosa gani wewe wakati mtu anafanya kazi nzuri. Hebu nieleze biashara ya madawa ya kulevya iko kama zamani? Vijana wamenusurika wangapi. Wauzaji awamejaa korokoroni ndio hao wanalilia kichwa cha makonda. Kuna hospitali kule chanika imejengwa kwa juhudi za makonda..kuna mambo mengi ukurada hautoshi. Mwacheni makonda afanye kazi.
 
Mjinga sana wewe praise team wa lumumba jiandaeni kwa sabotage za CIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama asipoondolewa Kuna uwezekana mkubwa wa kupigwa ban kwa viongozi wengine. USA wana evidence na matendo yake.hawakurupuki tu.
TUTAELEWANA TU! Tumepiga sana kelele hapa kuhusu Serikali hii na Makonda kuuwa raia wasio na hatia mkawa mnatukejeli tu, sasa naona tunaenda pamoja.
 
Kwani tz Bila marekani si tunaweza ishi sasa wasitutishe Kama vp watembee na wasitubabaishe na uyo makonda ni kwamba hizo haki za binadamu anawezaje kuvunja za marekani za Tanzania ambapo ndio kwao hasizivunje???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…