Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Nimerudi nyumbani kutoka mahali ninapofanyia shughuli zangu, nimekutana na kitu kinanipa mawazo sana.

Mwanangu wa kwanza (4yrs old) alikuwa anapenda shule sana, mwaka jana alikuwa anasoma shule si mbali sana na


Wewe ni mzungu au muafrika??
 
Mkuu upo sahihi.

Waalimu watussidie hapa. Hii kumkaririsha mtoto mpaka namba 1,000 shule ya awali inakuwaje kwani?
Lea mwanao Hadi miaka 5 , miaka 6 ndio aanze kwenda Shule ya msingi

Kabla ya hapo fanya homeschooling mwenyewe,
 
Nawaona saa 12 wanaenda shule kwa mguu, najiuliza ,saa hii wanaenda kufanya nini
Ni kutesa watoto..
Nishaona mtu kwenye daladala Yuko na kabinti kake kamesinzia na kanaonekana darasa la kwanza...na ni Saa kumi na moja alfajiri ...sijawahi kuelewa
 
Yaani hizi shule zina ujinga mwingi. Mwanangu darasa la kwanza wanatoka saa 11, anafika home saa 12, kachoka hawezi lolote, kapungua balaa. Namhamisha shule hii term ijayo, potelea mbali. Mimi nimesoma kayumba na sikuteseka hivyo na shule.
Yaani nimetoka kuwaamshia hapa, wanajifanya wanasusa eti uamuzi ni wako, nafanya utaratibu wa usafiri Kila saa 8 awe anatoka shule arudi nyumbani,muda mwingine wazazi tufanye màamuzi kwa maslahi mapana ya vizazi vyetu
 
Kosa ni lako mzazi mtoto wa miaka minne unampeleka shule ya mbali.

Hapo anakuwa wa kwanza kuchukuliwa na wa mwisho kurudishwa. Unaweza kukuta anawahi kutoka ila anazunguka mji mzima kurudisha wenzake.

Mtoto mdogo unampeleka daycare za jirani za kutembea tu dada anampeleka saa saba au nane anaenda kumchukua.

Unapochagua shule ya kumpeleka mtoto unaangalia factor nyingi sana moja wapo ni umbali
 
Shule ya karibu na nyumbani wanachapa sana wanafunzi, mtoto akipata chini ya 80 atakula fimbo za maana. Siku moja nilipita nikasikia watoto wanalia balaa, kuuliza naambiwa wanakula mboko sana
Unamkimbiza asichapwe ?
 
Hili nimeliona, nimeenda kuongea nae wananisusia eti utajua mwenyewe, nafanya utaratibu wa usafiri awe anaenda saa 2 saa 8 anatoka

Wengine tunatafuta kipato mbali kidogo na familia zetu hivyo tukipata hata muda wa kupumzika wiki 2 ndo mambo kama haya tunayaona
 
Unasema kweli kabisa. Ila mimi naona hili ni suala la wazazi wenyewe na uongozi wa shule na siyo serikali. Mimi nikiona mushkeli kidogo tu kwenye shule huwa nawasiliana na uongozi na wakileta ujuaji namhamisha kwenda shule nyingine. Japokuwa shule za Tanzania ni kama wanaigana namna ya kuendesha shule (miundo na uendeshaji umejaa makosa mengi) lakini bado kuna chache wanazingatia taratibu nzuri.

Kuna shule moja nilimhamisha kwa sababu ya kuchapa. Ilikuwa gari la shule likifika mtoto anaanza kuangua kilio, wakati alikuwa anapenda sana shule, kuuliza anasema wanachapwa. Nikaenda shuleni mwalimu mkuu anasema hii shule inapendwa na wazazi kwa sababu ya kuchapa watoto ili waelewe vizuri na wawe na adabu. Ujinga ulioje!
 
Hizi daycare kasoma mwaka Jana ilikua hapa tu, mwaka huu nikapewa recommendation na mtu Kuna nursery nzuri ndo nikawa nimempeleka huko, ila nimegundua nilifanya Kosa kubwa sana

Leo nimeenda shuleni nimewaambia mwanangu ataripoti saa 2 saa 8 anatoka usafiri ntamtafutia mwenyewe au nimtoe hapa, wamekubal kishingo upande
 
Changamoto hapo Mtoto wako anaweza akawa anakaa mbali na Shule kwahiyo anakuwa wa kwanza kuchukuliwa halafu wa mwisho kurudishwa na gari la shule.!

Na kule shule unakuta ratiba ya masomo inaisha saa nane au tisa mda uliobaki unapotelea njiani.!
Kama mzazi angalia shule iliyopo karibu na Mtoto wako kuepusha vitu kama hivi kwa mtoto wako.!
 
Labda wanaamini wazazi wengi muda wa saa 7 wanakuwa wako kazini kwahiyo wanawachelewesha ili wakutane jioni.
Hiyo ni kwa sababu wapo wazazi huwapeleka watoto nursery kama kumtunza tu(huku alison's) wakati yeye akiwa kazini.
Ni kosa kuamini bila kushirikisha wazazi.
 
Unamkimbiza asichapwe ?
Kuna kuchapwa lakini sio viboko vilivyopitiliza. Sisi tulichapwa lakini sio kwa ajili ya kupata chini sijui ya 80, tulichapwa kwa makosa yakueleweka. Utampchapaje mtoto kapata chini ya 80, huu ni ukatili kwa watoto.
 
Wazazi huwa tunaangalia shule inayofanya vuzuri bila kuangalia vitu vinginr. Kuna rafiki yangu nilimshauri amwamishe mtoto shule ya karibu aachane na huo ujinga. Ndani ya miezi miwili mtoto alinenepa. Tunawapa watoto mateso sana
 
Heri uvuje damu wakati wa mazoezi ili uje kutoka jasho kidogo wakati wa vita. .....ukipenda iwe kama uanvyotaka wewe au ukimuonea huruma chalii wako kuna uwezekano mkubwa wa kuja kujuta baadae
 
Siku moja nawahi usafiri nimeamka zangu saa kumi natoka nje nakutana na mwanafunzi na begi lake anaenda shule ,nilishangaa sana

Hizi elimu za sasa ni utumwa kabisa
 
Mfumo wa Elimu au ni utaratibu wa genge la watu flani wenye kupambania maslahi yao binafsi? Mimi nina jirani yangu watoto wake wanatoka nyumbani saa kumi na mbili kasoro wakiwa na mabegi makubwa mno kama kilo 15 hivi za vitabu na madaftari kila mmoja na wanarudi saa 12++ jioni kila siku mpaka jumapili! Wanasoma shule ya serikali kabisa ya msingi ya kingleza inayopatikana iringa mjini!

Elimu hasa hii ya shule ya msingi imekuwa changamoto mno yaani huko mashuleni hakuna ratiba na mwalimu yoyote anaweza kuingia muda wowote kufundisha somo lolote hii inasababisha wanafunzi kubeba madaftari yote kabisa kitu ambacho hata sisi tuliosoma zama za mawe tulikuwa tunafuata ratiba!

Tunao walimu wakuu waliochoka kufikiria wanatumia mabavu kuliko akili na kama mjuavyo walimu walivyo waoga hakuna anayeweza kukemea hili hata kama na wao linawabana kufanya mambo yao
 
Heri uvuje damu wakati wa mazoezi ili uje kutoka jasho kidogo wakati wa vita. .....ukipenda iwe kama uanvyotaka wewe au ukimuonea huruma chalii wako kuna uwezekano mkubwa wa kuja kujuta baadae
Wewe unaona Sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…