Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Serikali ingilieni kati, huu mfumo wa elimu utasababisha watoto waanze kuichukia shule

Shule zote chekechea, primary mpaka secondary watoto mwisho wa kusoma iwe saa nane na nusu au tisa.
 
Nimerudi nyumbani kutoka mahali ninapofanyia shughuli zangu, nimekutana na kitu kinanipa mawazo sana.

Mwanangu wa kwanza (4yrs old) alikuwa anapenda shule sana, mwaka jana alikuwa anasoma shule si mbali sana na hapa, walikuwa wanatoka saa 6 mchana, sasa mwaka huu nikaona nimtafutie nursery bora angalau hata mwakani aanze la kwanza.

Aisee sasa hivi ndio nimekaa nyumbani, yapata muda kidogo wife alinambia siku hizi dogo hapendi shule, nikamwambia labda hajapata marafiki hiyo shule mpya!

Sasa hawa watoto wa nursery wanaamka saa 11:30 saa 12 gari lipo getini, kutoka shule saa 12, homework kibao, mtoto muda wote namuona kachoka.

Leo kaamshwa kwenda shule mtoto analia tu, yaani hawa watoto wana ratiba ngumu kuliko hata watumishi, hivi kweli nursery mkiwaachia saa 7 kuna tatizo gani? Wanacheza na kurelax saa ngapi hawa watoto?

Leo naenda kukiwasha shuleni, mwanangu mwisho saa 8 atakua anakuja kuchukuliwa anapelekwa nyumbani, kama hawataki poa tu nitatafuta shule nyingine, uzuri private zipo kama utitiri.

Serikali wekeni miongozo ya elimu, hwa watoto wana ratiba ngumu hata physiological sidhani kama wanafurahia shule kama miaka yetu ile.

Elimu yenyewe hii ya kuja kukutana na mishahara ya laki 4 ukitoka chuo, upuuzi tu!
Changanya akili huna haja ya kulaumu wakati shule umempeleka mwenyewe.
Mimi wa kwangu alikuwa wa kwanza kuchukuliwa wa mwisho kurudishwa, so saa 12 gari inamchukua maana inaanzia kwangu, kumrudisha saa 12 na nusu muda mwingine saa moja muda mwingine hadi napgiwa simu foleni tutachelewa kama unaweza mfuate... Nikaona isiwe tabu nikamhamisha shule anasoma shule ya karibu yani kutoka napoishi hadi shule kama mimi jikitembea kwa miguu ni mwendo wa kama dakika 30 kwa mwendo wa kawaida... Ila nikaona nimlipie tu school bus, so inamptia saaa moja na nusu, inamrudisha saa 9 na robo yani kwa suala la muda wako vzuri ikizidi sana dakika 5 na yuko la tatu.
Wazazi muda mwingine tunakosea, mtu anaishi bunju mtoto anasoma mikocheni wewe unategema nini? Napo ukalaumu serikali.
 
Tutafute hela tuwasomeshe watoto mitaala tofauti na NECTA, wakati huo huo tukiwekeza ili waje waendeleze

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mkuu n kama ulikua kichwani kwangu, najichanga hapa dogo mwakani aende international school potelea pote akija kuzingua huko mbele ni juu yake mimi nimefanya sehemu yangu
 
Mkuu n kama ulikua kichwani kwangu, najichanga hapa dogo mwakani aende international school potelea pote akija kuzingua huko mbele ni juu yake mimi nimefanya sehemu yangu
Inabidi uwe na msuli hasa mkuu, Kila la kheri
 
Changanya akili huna haja ya kulaumu wakati shule umempeleka mwenyewe.
Mimi wa kwangu alikuwa wa kwanza kuchukuliwa wa mwisho kurudishwa, so saa 12 gari inamchukua maana inaanzia kwangu, kumrudisha saa 12 na nusu muda mwingine saa moja muda mwingine hadi napgiwa simu foleni tutachelewa kama unaweza mfuate... Nikaona isiwe tabu nikamhamisha shule anasoma shule ya karibu yani kutoka napoishi hadi shule kama mimi jikitembea kwa miguu ni mwendo wa kama dakika 30 kwa mwendo wa kawaida... Ila nikaona nimlipie tu school bus, so inamptia saaa moja na nusu, inamrudisha saa 9 na robo yani kwa suala la muda wako vzuri ikizidi sana dakika 5 na yuko la tatu.
Wazazi muda mwingine tunakosea, mtu anaishi bunju mtoto anasoma mikocheni wewe unategema nini? Napo ukalaumu serikali.
Nimeenda Leo tumekubaliana atakua anaenda sa 2 kutoka saa 8 ila usafiri ntajitegemea
 
Ni kutesa watoto..
Nishaona mtu kwenye daladala Yuko na kabinti kake kamesinzia na kanaonekana darasa la kwanza...na ni Saa kumi na moja alfajiri ...sijawahi kuelewa
Kuna mtoto anatoka Tegeta anaenda Diamond kila siku, Mzazi anaona furaha kweli

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Yaani hizi shule zina ujinga mwingi. Mwanangu darasa la kwanza wanatoka saa 11, anafika home saa 12, kachoka hawezi lolote, kapungua balaa. Namhamisha shule hii term ijayo, potelea mbali. Mimi nimesoma kayumba na sikuteseka hivyo na shule.
Ni swala la Wazazi wenyewe kuamua, swala la kuachia shule zifanye uamuzi hapana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Shule ya karibu na nyumbani wanachapa sana wanafunzi, mtoto akipata chini ya 80 atakula fimbo za maana. Siku moja nilipita nikasikia watoto wanalia balaa, kuuliza naambiwa wanakula mboko sana
Sasa wewe watakiwa uende shuleni kulalamika, au huyo anayejifanya anachapa sana umchape na yeye

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Unasema kweli kabisa. Ila mimi naona hili ni suala la wazazi wenyewe na uongozi wa shule na siyo serikali. Mimi nikiona mushkeli kidogo tu kwenye shule huwa nawasiliana na uongozi na wakileta ujuaji namhamisha kwenda shule nyingine. Japokuwa shule za Tanzania ni kama wanaigana namna ya kuendesha shule (miundo na uendeshaji umejaa makosa mengi) lakini bado kuna chache wanazingatia taratibu nzuri. Kuna shule moja nilimhamisha kwa sababu ya kuchapa. Ilikuwa gari la shule likifika mtoto anaanza kuangua kilio, wakati alikuwa anapenda sana shule, kuuliza anasema wanachapwa. Nikaenda shuleni mwalimu mkuu anasema hii shule inapendwa na wazazi kwa sababu ya kuchapa watoto ili waelewe vizuri na wawe na adabu. Ujinga ulioje!
Shule hizo hukaririsha tu watoto na sio kuelewa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hizi daycare kasoma mwaka Jana ilikua hapa tu, mwaka huu nikapewa recommendation na mtu Kuna nursery nzuri ndo nikawa nimempeleka huko, ila nimegundua nilifanya Kosa kubwa sana

Leo nimeenda shuleni nimewaambia mwanangu ataripoti saa 2 saa 8 anatoka usafiri ntamtafutia mwenyewe au nimtoe hapa, wamekubal kishingo upande
Ukienda International Schools unakuta kuna gari zipo zinawasubiria watoto kuanzia asubuhi hadi muda wa kutoka na ikifika saa 6 wanafunzi wanaruhusiwa kutoka shule

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wazazi huwa tunaangalia shule inayofanya vuzuri bila kuangalia vitu vinginr. Kuna rafiki yangu nilimshauri amwamishe mtoto shule ya karibu aachane na huo ujinga. Ndani ya miezi miwili mtoto alinenepa. Tunawapa watoto mateso sana
Wazazi wengi ni wapumbavu, hawawapendi watoto wao

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom