Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
Ni wazi kwa sasa siyo rahisi kuzuia maandamano ya Gen Z kutokana na kwamba vijana wako tayari kufa. Radicalisation iliyofanyika through mitandao na matokeo ya Oktoba 29 yanaonyesha hawana cha kupoteza.
Kwa ushauri wangu sioni ubaya Serikali wakawaruhusu waandamane kwa mujibu wa Katiba ya JMT na kuzingatia yafutayo:-
1. Level zote iwe kwa wilaya au mkoa lazima waandamanaji wajitambulishe kwa kuomba/ kutaarifu mamlaka
2. Maandamano lazima yabebe ujumbe maalum ambao wanataka kufikisha kwa public
3. Waseme wataanzi wapi na wataishia wapi.
4. Wakiruhusiwa, basi Polisi iwasindikize ili kulinda mali za wananchi wengine
5. Kama wakikaidi kufuata muongozo huo basi Polisi na vyombo vya dola wasisite kufanya kazi yao kwa mujibu wa Katiba
Hakuna sababu ya kupimana ubavu na Gen Z. Nao Gen Z watambue kuwa nchi ni yetu wote hakuna haja ya kuharibu miundombinu ya Serikali au kuiba mali za watu.