PostGE2025 Serikali iruhusu maandamno ya D9 lakini yawe na viongozi, ujumbe na destination

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Nadhani Gen Z ni kizazi Bora na jeuri kuliko vyote (ukiondoa kizazi kile cha Nyerere) kuwahi kutokea katika historia ya Tanganyika.

Muda utaongea.
 
Mimi siyo Kamanda bali ni raia mwema nina share hekima zangu tu
 
Haya maandamano hayahitaji ruhusa ya viongozi,kwani yale ya Mo29 yalikuwa na ruhusa.!?


Nashauri serikali iyapige marufuku na Leo Samuya atoe tamko la kuua watanganyika wote watakaoandama huku akiwatumia km km
Hapana, hii siyo approach nzuri. Muafaka ni jambo jema
 
Uliambiwa nchi hii inaserikali? Mnafikili Gen Z ni malofa kama nye. Hatuhitaji ruhusu ya yeyote mpaka tuunde serikali na jeshi linalotambua wananchi. Bata wahed na bado
Kwani Gen Z wa Nepal na Madagascar waliunda Serikali yao? Forget about this dream
 
Mnataka kuwe na viongozi ili muweze kuwa-target kwa urahisi na kuvuluga mpango mzima?

Mnataka kujua route ya maandamano ili muweke snipers juu ya nyumba?

Jibu ni, kila muandamanaji ni kiongozi na route mtaijua siku ya tukio
Where leadership falters and authority is absent, anarchy rushes in to fill the void.
 
Hivi ni sahihi kabisa.
 
Jambo lolote bila uongozi huzzah fujo, na madhara ya fujo ni mabaya
 
Wanaotaka uchaguzi huru ufanyike baada ya huu batili kuyeyuka unashauri waelekee ofisi ipi Ili kufanikisha jambo hili kwa amani kabisa?
 
Jambo lolote bila uongozi huzzah fujo, na madhara ya fujo ni mabaya
Sasa ni kwamba maandamano yanayofuata hayatokuwa na kiongozi na wala hayataeleweka yanaanzia wapi kama yale ya tarehe 29.

Kila mtu atajiongoza popote yatakapomkuta naye ataelezea malalamiko yake.
 
Hawawezi kukubali kuweka viongozi.

Serikali ikitaka kuongea na Machinga au boda boda au Waalimu au Waislamu au Wachimbaji wadogo wadogo....

CHA KWANZA SERIKALI INAWAAMBIA TUONYESHENI VIONGOZI WENU.

Then wanakuletea gari na dereva wa serikali akulete ofisini kwa RC. Kupanda tu gari la serikali na kukaa meza moja na RC jitu hohehahe la Tandale kwa Mtogole linaona limefika kilele cha maisha, linauza wenzie. Mchezo umekwisha.

GEN Z WALISHASHTUKIA

GEN Z SIO CHAMA CHA WALIMU WA UPE

WALA GEN Z SIO CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO
 
Hizi hasira hata sisi wenye biashara zetu tunazo sana sio nyinyi vibaka tu.. na kwa taarifa yako safari mkiiba tena na kuvunja vitu vyetu itakuwa mara mbili ya October 29...
Huna akili kabisa waliouwawa wengi walikua majumbani. Mie huku nilipo hakukuwa na maandamano kabisa ila bado kuna watu zaidi ya 10 walipigwa risasi. Mbaya zaidi wengi waliuliwa ndani ya mageti kabisa!!

Yaani hawakuandamana wilaya nzima na bado walibaki ndani kwenye curfew ila bado mkaona haitoshi hadi kuwafuata vyumbani!!

Sasa wewe unaleta utani hapa, watu wana machungu huku unadhani mjinga mmoja akigawa silaha huku itatokea nini? Embu acheni kushabikia upumbavu.
 
Hatuwezi kufika huko,
Nani aliwahi dhani vijana wangechachamaa ile October 29? Mie binafsi hata mboga tu sikuwa nimenunua maana nlijua business as usual!!

Sasa kwa ughafla ule ule (God forbid) wanaweza chukua maamuzi magumu wakageuzia kisasi kwa wazanzibar wa bara!! Unadhani hali itakuaje?

Embu tujitafakari na kujenga umoja kuliko hizi kauli za kejeli humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…