Serikali isikubali kutangaza “total lockdown” au Karantini. Wanaoishawishi ama hawajui wanachokishauri au ni wabinafsi


Kwanza naomba nikupongeze kwa ''kukomaa nae'' ndugu mtoa mada, umeonyesha kuhimili mjadala na kuwasilisha kile unachokisimamia kwa umahiri mkubwa. Hongera sana dada Rebeca 83
Naomba nianze kuchangia mjadala kwa kunukuu maneno yako haya...

''I believe hivi vifo tunavyoviona sasa hivi vinatokana na hao walioambukizwa KABLA ya lockdown na sio NEW PATIENTS ….(what I believe)''

Uhalisia wa mambo ni kwamba nchini Italia bado kuna maambukizi mapya kila siku.

Imani yako inakinzana na data za kisayansi.
Kwa hoja hii tu (belief), unapoteza uhalali wa kuendelea kujadili mjadala huu ambao umejikita kwenye sayansi zaidi.

Mchango wangu kwenye mada:
Naungana na ndugu MM Togolani kwamba kwa sasa, lockdown haitakua njia muafaka na stahiki ya kukabiliana na mlipuko wa COVID19 pamoja na ''madhara yake'' (sio vifo pekee).

Sababu zangu:
1. Aina ya maisha tunayoishi. (mtoa mada kaeleza vya kutosha)
2. Nature ya ueneaji wa ugonjwa husika dhidi ya ''tabia zetu'' (Mtu mmoja anatoka nje anaweza kuwaletea balaa mliopo ndani).

NB; Unapotatua tatizo moja, hautakiwi kusababisha tatizo jingine kubwa kuliko lile unalolitatua. (Total lockdown kwa sasa, kwa Tanzania, itakiuka hii kanuni).

Ieleweke wazi kwamba tunaopingana na lockdown tunaunga mkono jitihada na njia zingine zinazosaidia kupunguza kasi ya kuenea na madhara ya COVID 19 kama tunavyoshauriwa na wataalamu wa afya.
 

Umesema ''we don't need to have scientific research au data kujua kama lockdown inasaidia kupunguza kasi ya maambukizi ya COVID 19 ama la...''

Halafu ukaja kusema ili kupambana na huu ugonjwa uhataji kutumia ''common sense na little medical knowledge kupambana nao, sio academic papers au research''

Mkuu mulwanaka hauoni kama hiyo itakua ni namna dhaifu sana ya kupambana na janga ''serious'' kama la COVID19 ?
 
Sio lazima twende kwenye total lockdown, lakini tufanye machache:
(Hatua za kuchukua ndani)
1. Elimu kwenye media zote kuhusu Corona,
Msisitizo ngazi ya serikali ya mtaa. (Elimu bado sana, ushahidi alichofanya Masanja Dodoma, angalia baadhi ya viongozi nyendo zao si za kuzingatia tatizo la sasa)
2. Hatua ya pili iwe ya kiutawala, mikusanyiko isiyo ya lazima isimamishwe. (Serikali imetekeleza kwa kiasi ila bado sana),
3. Mikusanyiko ya lazima inahitaji iboreshwe, hapa ushirikishaji wa wananchi kwa ngazi ya kata, wilaya hadi mkoa kujua namna gani bora ya kutekeleza hii hatua ngumu lkn muhimu.
4. Mengineyo
 
Mkuu hi ni emergency mda wa scietific research na academic presentations haupo tena, nchi kama Brazil wingereza US wamebadilisha viwanja vya mipila kua emergency medical facilities,........ hapa huwezi kutafuta utafiti wa kisayansi kuhusu effectiveness ya lock-down ndo maana kuna haja ya kua na ginius leaders wenye uwezo wa kufanya maamuzi kwa wakati kama hu, sio wale wa kusikilizia kwanza kuona upepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What is the solutions
 
Mkuu umeandika ''nitajihu'', nadhani tu tuelewe kwamba makosa ya kiuandishi ni mambo ya kawaida tu kama ujumbe unaweza ukaeleweka.
Nilikuwa nimelewa jana ndio maana nikaomba hivyo na bahati mbaya nikakosea!Kuna typing error na syntax error,i hope umeelewa!Naomba niulize,hivi hangover iking'ang'ania unatumiaga nini kupata nafuu?
 
Huwa napata ukakasi tu ninapoona mtu anafanya makosa ya kizembe,yaani nakuwa irritated kabisaa!
 
Mkuu yamepita!Sasa ngoja nitulie kidogo hangover iiishe nitakuja na mchango wangu kwenye hii hoja!
 
Ngoja na mimi nitoe maoni yangu.Kwa mazingira ya kwenye usafiri,masoko si rafiki kwa jinsi ugonjwa huu unavyoambukiza yatahatarisha maambukizi kwa wingi ambayo yataathiri kupita uwezo wa miundo mbinu na mfumo wa usimamizi wa Afya wa nchi yetu.

Watu hawana jinsi wanalazimika kwenda kutafuta riziki katika mazingira ya kifukara,kuwazuia ni kama kumlazimisha ndege mwenye mbawa asiruke kwenda kutafuta lishe.Hakuna suluhu.Mazingira haya hufanya watu kuendeleza Imani potofu za kumuachia Mungu awafanyie miujiza kwani hawana jinsi.

Tatizo hasa ni uongozi.Uongozi. Uongozi hulinda mifumo na miundo inayotoa viongozi butu wasio na uwezo.Viongozi wamewaweka wananchi kwenye mazingira haya magumu yanayoleta maisha haya ya mateso.
 
Huyo genius leader afanye hayo maamuzi basing on what ?
 
What is the solutions

Mtoa mada ameshaeleza (kama unafuatilia mtiririko wa huu uzi) ongeza na measures zingine ambazo wataalam wa afya wamekua wakizieleza kila siku kupitia njia mbalimbali. Hata humu JF kuna nyuzi nyingi zinaeleza hayo, sidhani kama natakiwa kuzirudia moja baada ya nyingine.
 
Endeleeni kuleta utani kwenye mambo ya msingi hivyo hivyo siku mwanaccm akipata korona ndio mtatia akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
We ulitakaje? Unapesa wewe ya kukas ndani siku tatu? Kama we unayo umewaza kuhusu shangazi zako, wajomba zako, mama zako, dada na kaka zako wakiwa na familia zao.? Je wote kwao wans system za maji safi au wengine wanapanga foleni kwa jirani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good thinking
 
Yaani uumwe corona halafu ufanya kazi ngumu halafu utegemee kupona?

Kama ndio unajidanganya hivi pole.
 
Mnapigania kwa nguvu nch iweke Lock down sababu mnajua ili wananch wawe upande wenu ni lazima wawe na njaa ndiomana hata mwanzo mlikua mnapambana ili tu nch inyimwe misaada watu maisha yawe magum muanze siasa zetu Kama India wameshindwa hio lock down nyie bongo mtaweza au mnatafuta sos ya machafuko ILI mteremke nayo?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuambie walio Lock down maambukiz yapo au hayapo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudi kwanza ukajifunze kuandika, nyie ndio wahamiaji haramu halafu mkipata bahati ya kupewa kitambulisho cha uraia mnaanza kujifanya wazawa ili mpate uongozi.
Shubaamit

Sent using Jamii Forums mobile app

Haya unamwambia mtoa mada?

Ndo hajui kuandika? Aisee.....

Hebu eleza kuna kosa gani la kiuandishi katika makala yote??

Mimi sijaona kosa....

Na kiukweli, ameandika na kuiwasilisha hoja yake vizuri sana....

Na si tu uwasilishaji wa hoja yake ni mzuri, bali pia hoja ina logic kwa 100%....

Nami binafsi nakubaliana naye kwa 100%, we don't need a "total lockdown" here in Tanzania....!!
 
Huko Urusi au Alaska kuna kipindi baridi inakuwa kali sana mpaka -45.
Basi shule zinafungwa. Na vyuo siku hio vinafungwa kwa sababu ni hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…