Serikali isikubali mtafaruku wa Bandari kuchukua mkondo wa kidini, ni ngumu kuidhibiti

Serikali isikubali mtafaruku wa Bandari kuchukua mkondo wa kidini, ni ngumu kuidhibiti

Kwani lazima wao? Au labda kilishapokelewa cha juu miaka ya nyuma kwa ahadi ya kupewa hiyo bandari sasa huu ndio wakati wa utekelezaji, nchi ina siri nyingi sana, haiwezekani mother akashupaza shingo namna hii.
hawa wanalichukulia hili jambo kiulahisi ila naona kabisa red light kwaajili ya huu udini wanao utanga majukwaani watakuja kushtuka Taifa halitawaliki tena
 
Unajua ni kwa muda gani hizi kelele zimeanza kupigwa? Lakini hakuna anayejali ndani ya serikali zaidi ya kutuma makada wao waupigie debe mkataba huu badala ya kujibu hoja za wakosoaji. Mpaka hapo unaweza kuona tuna serikali ya namna gani na sidhani kama unaweza kuruhusu busara kwa watu kama hawa.

mpaka hapa unaona hawa viongozi wa tec wapo sahihi kwa msimamo wao.

halafu hili suala lilishachukua mkondo wa kidini mapema tu kwa hawa wenzetu kuamua kuungana na serikali mazima bila kuhoji chochote. Lazima mtu mwenye akili ujiulize inamaanisha nini.
can you imagine zitto ni wa kukaa kimya kuhusu mambo mazito yanayoendelea katika taifa hili? Asitafiti wala kutoa ufafanuzi kama ilivyo kawaida yake?

hakuna mtu mwenye akili asiyependa uwekezaji katika nchi hii ambao utatuboreshea mambo yetu. Lakini altitude ya serikali kuhusu ukosoaji na jinsi mambo yanavyoenda ni hali yenye kutia mashaka sana kwa mtu mwenye akili.
 
Inawezekana mkataba una kasoro kweli ila ukiwasikiliza wabongo hamna kitu utafanya, watakupangia hadi mambo ya faragha.

Soon masheikh nao watatoa tamko kuunga mkono hoja. Hili sakata lishachukua sura ya kidini, ni ujinga wa kiwango cha juu.
 
Inawezekana mkataba una kasoro kweli ila ukiwasikiliza wabongo hamna kitu utafanya, watakupangia hadi mambo ya faragha.

Soon masheikh nao watatoa tamko kuunga mkono hoja. Hili sakata lishachukua sura ya kidini, ni ujinga wa kiwango cha juu.

Wabongo ndio wenye Nchi.
Na watawala ni lazima waongoze nchi kulingana na matakwa ya wananchi hivyo ndivyo Katiba inasema.

Wewe kiongozi unaona unaakili lakini inaongozwa wajinga wengi wanaotaka Jambo Fulani lifanyike alafu hutaki basi achia ngazi.

Watu wamekuchagua kuwaongoza vile wanachotaka(wengi wao) sio vile utakavyo(wachache).
 
je hivyo vifungu vikirekebishwa DP World watakubali kuendelea kuwekeza?

Hiyo Ipo juu Yao.
Tunachoangalia ni nchi na wananchi wetu. Hatutaangalia MTU au Taifa la nje ikiwa wananchi na taifa letu linaumia.

Ndio Yale ya kujenga viwanda ambavyo vinawageuza watanzania Misukule badala ya wafanyakazi.
 
Ndugu mbona wanasheria kibao wametoa ufafanuzi kwa yale yanayopingwa? Wakili Msando akiwa namba moja kwenye kutoa utetezi. Halafu sio kila watu wanaopinga wanamaanisha kuwa wana nia njema. Hao wanaoitwa wanasheria nguli wakati mwingine hutumia sheria hizohizo kuiingiza nchi kwenye shida. Wakati Zitto akiwa mbunge na Idris Rashid akiwa boss Tanesco, alipeleka hoja bungeni kuwa serikali inunue mitambo ya Dowans na kujitengenezea umeme ambapo pia Dowans iliahidi mitambo ikinunuliwa watafuta kesi waliyokuwa wamefungua. Wasomi wakapinga na kudai anachoshauri Zitto ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Kilichofuatia ni Dowans kushinda kesi huku mitambo wakiiuzia Symbions na hao Symbions kutuuzia sisi umeme. Kwahiyo wanasheria kama Shivji wanaweza kutumia sheria hizohizo kwa maslahi binafsi.

Huo ufafanuzi upo kwenye mkataba? Au ni Maneno tuu.
Huo ufafanuzi Watu wanataka uwepo kwenye Mkataba. Sio mkataba unasema hivi alafu ufafanuzi vile.
Mkataba unatakiwa ujieleza wenyewe na ujijibu wenyewe.
 
Sisi wazanzibari tunachotaka huu muungano ufe, maana wenzetu wadini na wabaguzi

Mangapi mmeyaamua kupitia muungano na yakaathiri Zanzibar na hatukutishia kuangusha serikali
 
Ule mkataba hauna shida yoyote ile, mbaya ni kwamba, wanaojadili na wanaopiga kelele ni watu wasio na uelewa na masuala ya Uwekezaji.

1. Ukomo wa mkataba.
Uwekezaji wa Long term tena wenye, kuweka new Fixtures and fittings, miundombinu, kulipa kodi ndani yake always hauna time limit, isipokuwa huwa na utaratibu wa kufanya maboresho na utenganifu ikitokea kuna mgogoro.

2. Umiliki wa Ardhi.
Hii nchi hakuna anayemiliki ardhi bali hupewa mamlaka ya kuitumia, na endapo serikali itaihitaji huichukua, hata hivyo huwezi kumpa mtu uwekazaji then asiwe na right of use kwa hiyo Ardhi.

Wengi wanaochangia au kutoa mawazo yao ni wale wasiojua uwekezaji.

NB: Waliosoma ECONOMICS, FINANCE, ACCOUNTING nk wamesoma BUSINESS LAW ili kudeal na aina mbalimbali za mikataba ya kiuwekezaji na Biashara.
 
Nawaza pengine wale wa upande wa pili wakija na kauli kinzani SI elewi itakuwaje
Robert ameeleza Jambo la Msingi na ameuliza swali ambalo Wenye busara wengi wanajiuliza. Kama watu wengi wanaona kuna shida kwenye Mkataba ikiwemo Mahakama iliyojizongazonga lakini ikatoa hukumu ya Sare pale Mbeya nayo ikasema kuna maeneo kwenye mkataba inayashangaa. Lakini bado serikali na vibaraka wake Bunge wanasema mkataba ubaki kama ulivyo hauna tatizo, nini kiko nyuma ya pazia?
Umesema upande wa pili unaweza kuja na tamko tofauti. Mimi naijua serikali imejaa vilaza wasiojua kupima kina cha maji. Hao ndio waliomwambia Rais tuwakamate wanaopinga. Sitashangaa wakawashawishi upande wa pili waje na tamko tofauti. Nalisubiri ili Vita iwe nzuri zaidi lakini atakayeumia ni nyasi (Chama). Kuna watu wanadhani TEC ndo ya Kwanza kutoa tamko, wa Kwanza kutoa tamko ni Shura ya Maimamu. Katika tamko Lao walihusisha mpaka MoU ya hospitali Teule kitu ambacho kiko nje ya mjadala wa Bandari lakini walioshitumiwa hawakuwajibu. Wamekuja kuibuka na Waraka mzito juzi ndo tunawaona Mapapeti wanaotumiwa na serikali kina Kitenge wanaotumia viungo vya kutolea uchafu kufikiri wanajaribu kutikisa Baraza la Maaskofu eti tamko walilotoa ni tofauti na alilosoma Katibu wa Baraza Fr Kitima.
Shura ya Maimamu ilipotoa Waraka wake Kwa vile ulikuwa unaipaka mafuta mkataba mbovu Kwa kusema "huko mbele serikali iwe makini" hatukuona wakipigwa mawe.
Narudia kumuunga mkono Robert, kama Hakuna maslahi haramu yaliyojificha nyuma ya Mkataba huu, basi serikali ichukue hatua ya kuboresha vifungu vinavyolalamikiwa Sasa na si baadaye ili nchi iondoke kwenye mtanziko iliyomo. Kusema kwamba Mambo yatatulia yenyewe ni kujidanganya.
 
Natamani UPANDE wa pili, waje na wao watoe TAMKO lenye kuunga MKONO huu "mkataba" tena kwa hoja nzito kama walivyofanya TEC, labda Mh Rais ndio ataamini ya kwamba "MKATABA", huu umeligawa taifa, hivyo haufai, UFUTWE
Sasa ukiufuta si utakuwa umeunga mkono upande mmoja?
 
Wabongo ndio wenye Nchi.
Na watawala ni lazima waongoze nchi kulingana na matakwa ya wananchi hivyo ndivyo Katiba inasema.

Wewe kiongozi unaona unaakili lakini inaongozwa wajinga wengi wanaotaka Jambo Fulani lifanyike alafu hutaki basi achia ngazi.

Watu wamekuchagua kuwaongoza vile wanachotaka(wengi wao) sio vile utakavyo(wachache).

Well, I agree to disagree. Kuna muda inabidi uwe kauzu kufanya jambo kwa manufaa mapana ya nchi
 
Back
Top Bottom