Kiongozi anapokosa weledi wa kuliongoza taifa, haya ndio matokeo yake. Siku zote tatizo linatakiwa kufanyiwa kazi pale ambapo dalili pekee zinaanza kujionesha juu ya jambo husika, na sio kuamini upepo tu utapita!.
Kiongozi mzuri lazima ajue kutazama reaction ya watu wake, agundue tatizo lilipo, na ajue namna ya kulikabili, kabla halijawa kubwa zaidi na kugeuka gumu kulitatua.
Sasa pale ambapo kiongozi katikati ya tatizo anajitokeza hadharani, anasema ametuzibia masikio, huyu anaonesha vile hajielewi binafsi, hawaelewi wale anaowaongoza, na wala hajui namna ya kutatua matatizo yao.
Matokeo yake sasa, wengi zaidi wanaibuka kuupinga mkataba tofauti na mwanzo, na kadri siku zinavyozidi kwenda mambo yanazidi kuwa magumu, asijue tena ahangaike na kundi lipi, matokeo yake anazidi kupotea.
Frankly speaking, Samia anatakiwa kujiuzulu nafasi yake, amepwaya sana, ameiacha nchi ijiendee tu, yupo yupo tu, sasa haaminiwi na wale anaowaongoza, naamini hata nae hana habari nasi, yeye kwa sasa yupo na baraza lake la mawaziri, na waarabu wa Dubai.