Serikali isikubali mtafaruku wa Bandari kuchukua mkondo wa kidini, ni ngumu kuidhibiti

Ule mkataba hauna shida yoyote ile, mbaya ni kwamba, wanaojadili na wanaopiga kelele ni watu wasio na uelewa na masuala ya Uwekezaji.

1. Ukomo wa mkataba.
Uwekezaji wa Long term tena wenye, kuweka new Fixtures and fittings, miundombinu, kulipa kodi ndani yake always hauna time limit, isipokuwa huwa na utaratibu wa kufanya maboresho na utenganifu ikitokea kuna mgogoro.

2. Umiliki wa Ardhi.
Hii nchi hakuna anayemiliki ardhi bali hupewa mamlaka ya kuitumia, na endapo serikali itaihitaji huichukua, hata hivyo huwezi kumpa mtu uwekazaji then asiwe na right of use kwa hiyo Ardhi.

Wengi wanaochangia au kutoa mawazo yao ni wale wasiojua uwekezaji.

NB: Waliosoma ECONOMICS, FINANCE, ACCOUNTING nk wamesoma BUSINESS LAW ili kudeal na aina mbalimbali za mikataba ya kiuwekezaji na Biashara.
Zero brain
 
SERIKALI ISIKUBALI MTAFARUKU WA BANDARI KUCHUKUA MKONDO WA KIDINI, NI NGUMU KUIDHIBITI.

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Haya mambo yanayoendelea ndani ya nchi Kwa kweli hayavutii na kuna Wakati yanatia wasiwasi. Serikali inahitaji kutiiwa lakini nayo inaowajibu wa kusikiliza kile wananchi(wengi) wanachokitaka. Serikali isiyosikiliza Watu wake kamwe haiwezi kutiiwa.

Sakata la Bandari limezua mengi. Pia limeibua Pande mbili, wanaokubali Mkataba na kundi la pili ni wale wanaokataa mkataba. Kundi la wanaoukataa mkataba wao wanasema wanataka mkataba huo uboreshwe na kufanyiwa mabadiliko kwenye baadhi ya vifungu. Na kama Hilo halifanyiki basi automatically hawataki huo mkataba(huo mkataba haufai).

Wote wanajinasibu kuwa wanaipenda Nchi. Wote wanashutumiana na kutupiana maneno Makali na mengine ni machafu.

Swali moja muhimu ambalo litaleta tija na kuwaunganisha Watu hawa ni hili?

" Kwa nini hivyo vifungu au hayo madai yanayotolewa kuhusu vifungu ambavyo ni Tata visitolewe au kurekebishwa kwenye huo Mkataba?"

Yaani ni kipi serikali inashindwa kuufanyia marekebisho huo mkataba?

Hapo ndipo hata Sisi tusio na upande tunaona kuna tatizo. Kama madai ya wanaoukataa mkataba Kwa kigezo cha baadhi ya vifungu kuwa na dosari ni Kwa nini hizo dosari au mapungufu yasifanyiwe kazi ili kuwaleta Watu wote pamoja?

Je ni kiburi?

Je ni kukosa Uzalendo?

Au je ni kweli Bandari imeuzwa(Jambo ambalo binafsi najua haijauzwa).

Serikali tuseme imakataa kusikiliza Maoni ya wanasiasa wa upinzani labda Kwa kuhofia kuwa watawapa bichwa.

Haya vipi kuhusu Chama cha Wanasheria TLS. Ikiwa hao waliowataalamu wa sheria wameona mkataba unakasoro na unahitaji marekebisho kadhaa iweje serikali ikatae.

Serikali haioni umuhimu wa kufikiria Jambo hili licha ya wataalamu WA Kada husika kushauri.

Ni kweli Katiba inampa mamlaka Rais kuamua Jambo lolote pasipo kuomba ushauri lakini Jambo Hilo lisivunje Katiba Kwa sababu ya kiapo cha kuilinda Katiba.

Lakini kuyapuuza mawazo ya wataalamu wa Kada husika kimakusudi ni kujaribu kuiweka rehani nchi kimakusudi.

Haiwezekani Umeenda hospitalini umeshauriwa na Madaktari kuwa utumiaji wa Dawa Fulani Mpya ambayo hujawahi Kutumia, Kwa jinsi mwili wako ulivyo kuanzia kinga na mifumo ya mwili, itakuletea shida alafu Kwa Makusudi utake Kutumia Dawa hizo Mbaya zaidi unataka familia nzima itumie. Kwa kweli hiyo haina maana nzuri.

Msimamo wangu ni kuwa, serikali Ione haja ya kusikiliza Maoni ya msingi hasa Kwa wataalamu wa sheria kuhusu huo Mkataba. Kama haitaki kusikiliza wanasiasa wenzao basi wasikilize Wanasheria wenye utaalamu wa sheria.

Kipi kinashindikana kuboresha kwenye Huo mkataba? Kwa nini kisiboreshwe ikiwa Watanzania wengi hasa wataalamu WA sheria wameona kuna dosari?

Serikali katika madai yake inasema, pale bandarini sijui wafanyakazi sio waaminifu, sijui wengine ni Wezi ndio wanaozotesha kazi za bandarini. Nilimsikia Spika akizungumzia Jambo hili.

Unajua kauli kama hizo zinajaribu kueleza kuwa serikali Ipo corrupted. Yaani serikali Kabisa inasema pale bandarini sijui kuna Wezi sijui kuna watendaji wabovu, kwani hakuna Mahakama?

Kwani hakuna vyombo vya kushughulikia wahalifu, au ukifanya kazi bandarini upo juu ya sheria kiasi cha kuepuka kuwajibishwa?

Kusema watanzania milioni 60 hakuna waadilifu wa kuweza kufanya kazi katika vitengo nyeti kama bandarini ni kujaribu kutukana taifa. Serikali inashindwa kupika na kutengeneza Vijana waadilifu ambao watafanya kazi zao Kwa ufanisi?

Haya, mitafafuku kama hii Watu wanakosa hoja na matokeo yake kuingiza dini kwenye Siasa.
Kikawaida dini ikishaingia kwenye Siasa inakuwa na nguvu kuliko serikali.

Ili serikali iwe na nguvu ni sharti iweke dini upande wa pili shilingi. Kwa sababu Dini ni upande wa pili wa serikali, au tuseme ni mkono wa kushoto wa serikali.

Serikali inaweza kupuuzia wataalamu, sayansi na uwekezaji na mapesa lakini kamwe haiwezi kupuuzia suala la Dini, ambayo msingi Mkuu ni Imani.

Imani inanguvu kuliko Kitu chochote Baada ya Upendo.

Njia kuu ya kudhibiti Imani na Dini za Watu ni Upendo. Huwezi Kutumia nguvu kudhibiti dini. Ila upendo unaweza Kutumika kudhibiti Dini.

Najua serikali inajua nini chakufanya muda huu. Lakini Njia Bora ni kuyafanyia kazi Yale yanayotolewa na upande wa pili Kwa sababu sio mambo mabaya.

Kupuuzia Watu sio Njia sahihi. Kuwatisha pia sio Njia sahihi. Na pia ikiwa lengo ni kuiletea Maendeleo nchi yetu, kuufuta kabisa huo mkataba sio Njia Sahihi.

Njia sahihi ni kuurekebisha ili ulinde maslahi ya nchi kama ilivyoshauriwa na Watalaamu.

Angalizo, ikiwa kuna kundi la Watu wameingiza maslahi Yao binafsi katika mkataba huu na kuacha Nyuma maslahi ya Watanzania hao ndio wanaotuletea shida na kutugawanya kama taifa.
Na Siku zote kikombe kikivunjika hata kiungwe hakiwi kilekile tena.

Watu wasitumie Dini kuitisha na kuishinikiza serikali au kumyumbisha Rais aliyepo madarakani. Ila kama Rais au kiongozi atakuwa mkaidi na kutoisikiliza Sauti ya wengi basi Watu nao hawatakuwa na wajibu wa kuitii serikali.

Lakini kama serikali inafanya Yale ambayo wananchi wanataka, wakitokea wakaidi washughulikiwe Kwa mujibu wa sheria.

Tunahitaji tuachane na haya mambo.

Imetosha, Muafaka chanya upatikane.

Tuzingatie kwenye hili hakuna mshindi, Ila mshindi awe ni taifa. Kuzozana kwetu kuwe kwaajili ya maslahi ya Nchi.

Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Kurekebisha ulipokosea sio kujiabisha Bali ni uungwana. Na uungwana ni vitendo.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
Huo mkataba haufai Rais anauza nchi haina haja hata ya kurekebisha ikulu haina nia njema hakuna ni kuufuta tu hamna ziada
 
Wabongo ndio wenye Nchi.
Na watawala ni lazima waongoze nchi kulingana na matakwa ya wananchi hivyo ndivyo Katiba inasema.

Wewe kiongozi unaona unaakili lakini inaongozwa wajinga wengi wanaotaka Jambo Fulani lifanyike alafu hutaki basi achia ngazi.

Watu wamekuchagua kuwaongoza vile wanachotaka(wengi wao) sio vile utakavyo(wachache).
Serikali haiongozwi hivyo, ina taratibu zake. Huwezi ipangia serikali cha kufanya, mark my word ili uishi kwa amani.
 
Robert ameeleza Jambo la Msingi na ameuliza swali ambalo Wenye busara wengi wanajiuliza. Kama watu wengi wanaona kuna shida kwenye Mkataba ikiwemo Mahakama iliyojizongazonga lakini ikatoa hukumu ya Sare pale Mbeya nayo ikasema kuna maeneo kwenye mkataba inayashangaa. Lakini bado serikali na vibaraka wake Bunge wanasema mkataba ubaki kama ulivyo hauna tatizo, nini kiko nyuma ya pazia?
Umesema upande wa pili unaweza kuja na tamko tofauti. Mimi naijua serikali imejaa vilaza wasiojua kupima kina cha maji. Hao ndio waliomwambia Rais tuwakamate wanaopinga. Sitashangaa wakawashawishi upande wa pili waje na tamko tofauti. Nalisubiri ili Vita iwe nzuri zaidi lakini atakayeumia ni nyasi (Chama). Kuna watu wanadhani TEC ndo ya Kwanza kutoa tamko, wa Kwanza kutoa tamko ni Shura ya Maimamu. Katika tamko Lao walihusisha mpaka MoU ya hospitali Teule kitu ambacho kiko nje ya mjadala wa Bandari lakini walioshitumiwa hawakuwajibu. Wamekuja kuibuka na Waraka mzito juzi ndo tunawaona Mapapeti wanaotumiwa na serikali kina Kitenge wanaotumia viungo vya kutolea uchafu kufikiri wanajaribu kutikisa Baraza la Maaskofu eti tamko walilotoa ni tofauti na alilosoma Katibu wa Baraza Fr Kitima.
Shura ya Maimamu ilipotoa Waraka wake Kwa vile ulikuwa unaipaka mafuta mkataba mbovu Kwa kusema "huko mbele serikali iwe makini" hatukuona wakipigwa mawe.
Narudia kumuunga mkono Robert, kama Hakuna maslahi haramu yaliyojificha nyuma ya Mkataba huu, basi serikali ichukue hatua ya kuboresha vifungu vinavyolalamikiwa Sasa na si baadaye ili nchi iondoke kwenye mtanziko iliyomo. Kusema kwamba Mambo yatatulia yenyewe ni kujidanganya.
Kila tawala lazima ipitie kipindi kama hiki na sisi wananchi ni maneno yetu ya kila siku kuwa hatuwapi kura lakini mwisho wa siku ushindi wa kishindo kwa chama. Hili nalo litapita na maisha mengine yataendelea. Kama maaskofu wanabetia tabiri za hayati Sheikh Yahya Hussein ya kwamba katika kipindi cha Kiongozi mwanamke ndipo Ccm itapigwa chini.
 
Watanzania sio watu wa mambo hayo
Bandari itakuwa chini ya DP wodi na itapita kimyakimya kama hakuna kilichotokea.
 
Serikali ni wananchi.
Sikupingi kiongozi, ila hilo linatambuliwa kipindi cha uchaguzi na mazoezi ya kitaifa, nje ya hapo not applicable.
Pili, wananchi wanawakilishwa na wabunge ambao tayari wameridhia, iweje umtoe ubaya ambaye umempa idhini akuongoze na afanye maamuzi kwa niaba yako!?
 
Hilo ndio tatizo
 
Ule mkataba hauna shida yoyote ile, mbaya ni kwamba, wanaojadili na wanaopiga kelele ni watu wasio na uelewa na masuala ya Uwekezaji.

1. Ukomo wa mkataba.
Uwekezaji wa Long term tena wenye, kuweka new Fixtures and fittings, miundombinu, kulipa kodi ndani yake always hauna time limit, isipokuwa huwa na utaratibu wa kufanya maboresho na utenganifu ikitokea kuna mgogoro.

2. Umiliki wa Ardhi.
Hii nchi hakuna anayemiliki ardhi bali hupewa mamlaka ya kuitumia, na endapo serikali itaihitaji huichukua, hata hivyo huwezi kumpa mtu uwekazaji then asiwe na right of use kwa hiyo Ardhi.

Wengi wanaochangia au kutoa mawazo yao ni wale wasiojua uwekezaji.

NB: Waliosoma ECONOMICS, FINANCE, ACCOUNTING nk wamesoma BUSINESS LAW ili kudeal na aina mbalimbali za mikataba ya kiuwekezaji na Biashara.
Mbona namba moja hujasema ukomo ni miaka mingapi?
 
Najaribu kuwaza yani hivi ni kweli:
TLS-Imekosoa mkataba kisa mwekezaji mwarabu ama waislam na rais muislam
Wapinzani-Wamekosoa mkataba kisa mwarabu ama waislamu na rais muislam
Wabobevu wa Kisheria-Wamekosoa kisa mwarabu ama waislamu na rais muislam
TEC- Wamekosoa kisa mwekezaji mwarabu ama waislam na rais muislam

Unaona kabisa hii agenda ya kuingiza dini ni Upuuzi tu. Ila uko umuhimu wa mkataba kuwekwa sawa, na kusahau mambo ya kidini.

[emoji120][emoji120][emoji120]
 
SERIKALI ISIKUBALI MTAFARUKU WA BANDARI KUCHUKUA MKONDO WA KIDINI, NI NGUMU KUIDHIBITI.

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Haya mambo yanayoendelea ndani ya nchi Kwa kweli hayavutii na kuna Wakati yanatia wasiwasi. Serikali inahitaji kutiiwa lakini nayo inaowajibu wa kusikiliza kile wananchi(wengi) wanachokitaka. Serikali isiyosikiliza Watu wake kamwe haiwezi kutiiwa.

Sakata la Bandari limezua mengi. Pia limeibua Pande mbili, wanaokubali Mkataba na kundi la pili ni wale wanaokataa mkataba. Kundi la wanaoukataa mkataba wao wanasema wanataka mkataba huo uboreshwe na kufanyiwa mabadiliko kwenye baadhi ya vifungu. Na kama Hilo halifanyiki basi automatically hawataki huo mkataba(huo mkataba haufai).

Wote wanajinasibu kuwa wanaipenda Nchi. Wote wanashutumiana na kutupiana maneno Makali na mengine ni machafu.

Swali moja muhimu ambalo litaleta tija na kuwaunganisha Watu hawa ni hili?

" Kwa nini hivyo vifungu au hayo madai yanayotolewa kuhusu vifungu ambavyo ni Tata visitolewe au kurekebishwa kwenye huo Mkataba?"

Yaani ni kipi serikali inashindwa kuufanyia marekebisho huo mkataba?

Hapo ndipo hata Sisi tusio na upande tunaona kuna tatizo. Kama madai ya wanaoukataa mkataba Kwa kigezo cha baadhi ya vifungu kuwa na dosari ni Kwa nini hizo dosari au mapungufu yasifanyiwe kazi ili kuwaleta Watu wote pamoja?

Je ni kiburi?

Je ni kukosa Uzalendo?

Au je ni kweli Bandari imeuzwa(Jambo ambalo binafsi najua haijauzwa).

Serikali tuseme imakataa kusikiliza Maoni ya wanasiasa wa upinzani labda Kwa kuhofia kuwa watawapa bichwa.

Haya vipi kuhusu Chama cha Wanasheria TLS. Ikiwa hao waliowataalamu wa sheria wameona mkataba unakasoro na unahitaji marekebisho kadhaa iweje serikali ikatae.

Serikali haioni umuhimu wa kufikiria Jambo hili licha ya wataalamu WA Kada husika kushauri.

Ni kweli Katiba inampa mamlaka Rais kuamua Jambo lolote pasipo kuomba ushauri lakini Jambo Hilo lisivunje Katiba Kwa sababu ya kiapo cha kuilinda Katiba.

Lakini kuyapuuza mawazo ya wataalamu wa Kada husika kimakusudi ni kujaribu kuiweka rehani nchi kimakusudi.

Haiwezekani Umeenda hospitalini umeshauriwa na Madaktari kuwa utumiaji wa Dawa Fulani Mpya ambayo hujawahi Kutumia, Kwa jinsi mwili wako ulivyo kuanzia kinga na mifumo ya mwili, itakuletea shida alafu Kwa Makusudi utake Kutumia Dawa hizo Mbaya zaidi unataka familia nzima itumie. Kwa kweli hiyo haina maana nzuri.

Msimamo wangu ni kuwa, serikali Ione haja ya kusikiliza Maoni ya msingi hasa Kwa wataalamu wa sheria kuhusu huo Mkataba. Kama haitaki kusikiliza wanasiasa wenzao basi wasikilize Wanasheria wenye utaalamu wa sheria.

Kipi kinashindikana kuboresha kwenye Huo mkataba? Kwa nini kisiboreshwe ikiwa Watanzania wengi hasa wataalamu WA sheria wameona kuna dosari?

Serikali katika madai yake inasema, pale bandarini sijui wafanyakazi sio waaminifu, sijui wengine ni Wezi ndio wanaozotesha kazi za bandarini. Nilimsikia Spika akizungumzia Jambo hili.

Unajua kauli kama hizo zinajaribu kueleza kuwa serikali Ipo corrupted. Yaani serikali Kabisa inasema pale bandarini sijui kuna Wezi sijui kuna watendaji wabovu, kwani hakuna Mahakama?

Kwani hakuna vyombo vya kushughulikia wahalifu, au ukifanya kazi bandarini upo juu ya sheria kiasi cha kuepuka kuwajibishwa?

Kusema watanzania milioni 60 hakuna waadilifu wa kuweza kufanya kazi katika vitengo nyeti kama bandarini ni kujaribu kutukana taifa. Serikali inashindwa kupika na kutengeneza Vijana waadilifu ambao watafanya kazi zao Kwa ufanisi?

Haya, mitafafuku kama hii Watu wanakosa hoja na matokeo yake kuingiza dini kwenye Siasa.
Kikawaida dini ikishaingia kwenye Siasa inakuwa na nguvu kuliko serikali.

Ili serikali iwe na nguvu ni sharti iweke dini upande wa pili shilingi. Kwa sababu Dini ni upande wa pili wa serikali, au tuseme ni mkono wa kushoto wa serikali.

Serikali inaweza kupuuzia wataalamu, sayansi na uwekezaji na mapesa lakini kamwe haiwezi kupuuzia suala la Dini, ambayo msingi Mkuu ni Imani.

Imani inanguvu kuliko Kitu chochote Baada ya Upendo.

Njia kuu ya kudhibiti Imani na Dini za Watu ni Upendo. Huwezi Kutumia nguvu kudhibiti dini. Ila upendo unaweza Kutumika kudhibiti Dini.

Najua serikali inajua nini chakufanya muda huu. Lakini Njia Bora ni kuyafanyia kazi Yale yanayotolewa na upande wa pili Kwa sababu sio mambo mabaya.

Kupuuzia Watu sio Njia sahihi. Kuwatisha pia sio Njia sahihi. Na pia ikiwa lengo ni kuiletea Maendeleo nchi yetu, kuufuta kabisa huo mkataba sio Njia Sahihi.

Njia sahihi ni kuurekebisha ili ulinde maslahi ya nchi kama ilivyoshauriwa na Watalaamu.

Angalizo, ikiwa kuna kundi la Watu wameingiza maslahi Yao binafsi katika mkataba huu na kuacha Nyuma maslahi ya Watanzania hao ndio wanaotuletea shida na kutugawanya kama taifa.
Na Siku zote kikombe kikivunjika hata kiungwe hakiwi kilekile tena.

Watu wasitumie Dini kuitisha na kuishinikiza serikali au kumyumbisha Rais aliyepo madarakani. Ila kama Rais au kiongozi atakuwa mkaidi na kutoisikiliza Sauti ya wengi basi Watu nao hawatakuwa na wajibu wa kuitii serikali.

Lakini kama serikali inafanya Yale ambayo wananchi wanataka, wakitokea wakaidi washughulikiwe Kwa mujibu wa sheria.

Tunahitaji tuachane na haya mambo.

Imetosha, Muafaka chanya upatikane.

Tuzingatie kwenye hili hakuna mshindi, Ila mshindi awe ni taifa. Kuzozana kwetu kuwe kwaajili ya maslahi ya Nchi.

Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Kurekebisha ulipokosea sio kujiabisha Bali ni uungwana. Na uungwana ni vitendo.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
serikali yenyew imekuwa ikitumia masheikh kuwashambulia wakosoaj wa mkataba halaf unataka serikali isiruhusu udini ? wamekaa kimya kipind masheikh wanadanganya watu kuwa samia anapingwa kisa muislam wkt hoja anazielewa hazihusiani na dini yake , Serikali ndo mlez wa udini huu ,kisa masheikh walikuwa upande wao bas hawakuwa wazuia walipokuwa wanajadili mambo haya misikitin
 
Nafasi aliyoitoa ya Watu kutoa Maoni nafikiri imetosha. Huu ni muda wa kushughulikia Maoni ya msingi ili tuendelee na mambo mengine
kama alikuwa timamu tang alioambiwa kuwa mkataba hauna kikomo ilibidi either akanushe kwa kutaja muda wa mkataba au ashughulikie mkataba na sio kuwahonga wakina Kitenge na Zembwela na kuwatuma wakina mwaipopo kuwashambulia maprofesa walihoonesha kasoro za mkataba huo , Udini huu umeletwa na serikali
 
kuna mtu aliyetumia hizo zaid ya ccmu na machawa wa mama ?
 
Ndugu mbona wanasheria kibao wametoa ufafanuzi kwa yale yanayopingwa? Wakili Msando akiwa namba moja kwenye kutoa utetezi. Halafu sio kila watu wanaopinga wanamaanisha kuwa wana nia njema. Hao wanaoitwa wanasheria nguli wakati mwingine hutumia sheria hizohizo kuiingiza nchi kwenye shida. Wakati Zitto akiwa mbunge na Idris Rashid akiwa boss Tanesco, alipeleka hoja bungeni kuwa serikali inunue mitambo ya Dowans na kujitengenezea umeme ambapo pia Dowans iliahidi mitambo ikinunuliwa watafuta kesi waliyokuwa wamefungua. Wasomi wakapinga na kudai anachoshauri Zitto ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Kilichofuatia ni Dowans kushinda kesi huku mitambo wakiiuzia Symbions na hao Symbions kutuuzia sisi umeme. Kwahiyo wanasheria kama Shivji wanaweza kutumia sheria hizohizo kwa maslahi binafsi.
kipi kinakufanya useme wakosoaji hawana nia njema na uwekezaj wa bandarini ? ila hawa wanaoshabikia mkataba usio na muda wala conditions za kuivunja incase tusiporidhishwa au dp world wakikiuka sheria zetu ,ndo useme unawaona wana nia njema na taifa
 
Back
Top Bottom