Serikali isikubali mtafaruku wa Bandari kuchukua mkondo wa kidini, ni ngumu kuidhibiti

Serikali isikubali mtafaruku wa Bandari kuchukua mkondo wa kidini, ni ngumu kuidhibiti

Well, I agree to disagree. Kuna muda inabidi uwe kauzu kufanya jambo kwa manufaa mapana ya nchi

Ni kweli lakini hilo haliwezekaniki kwenye katiba inayotaka mamlaka itoke Kwa wananchi.

Kwa sababu hata uwepo wa Mtawala unatokana na maamuzi ya wengi waliomchagua. Hivyo kuenda kinyume Chao ni usaliti usiovumilika
 
SERIKALI ISIKUBALI MTAFARUKU WA BANDARI KUCHUKUA MKONDO WA KIDINI, NI NGUMU KUIDHIBITI.

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Haya mambo yanayoendelea ndani ya nchi Kwa kweli hayavutii na kuna Wakati yanatia wasiwasi. Serikali inahitaji kutiiwa lakini nayo inaowajibu wa kusikiliza kile wananchi(wengi) wanachokitaka. Serikali isiyosikiliza Watu wake kamwe haiwezi kutiiwa.

Sakata la Bandari limezua mengi. Pia limeibua Pande mbili, wanaokubali Mkataba na kundi la pili ni wale wanaokataa mkataba. Kundi la wanaoukataa mkataba wao wanasema wanataka mkataba huo uboreshwe na kufanyiwa mabadiliko kwenye baadhi ya vifungu. Na kama Hilo halifanyiki basi automatically hawataki huo mkataba(huo mkataba haufai).

Wote wanajinasibu kuwa wanaipenda Nchi. Wote wanashutumiana na kutupiana maneno Makali na mengine ni machafu.

Swali moja muhimu ambalo litaleta tija na kuwaunganisha Watu hawa ni hili?

" Kwa nini hivyo vifungu au hayo madai yanayotolewa kuhusu vifungu ambavyo ni Tata visitolewe au kurekebishwa kwenye huo Mkataba?"

Yaani ni kipi serikali inashindwa kuufanyia marekebisho huo mkataba?

Hapo ndipo hata Sisi tusio na upande tunaona kuna tatizo. Kama madai ya wanaoukataa mkataba Kwa kigezo cha baadhi ya vifungu kuwa na dosari ni Kwa nini hizo dosari au mapungufu yasifanyiwe kazi ili kuwaleta Watu wote pamoja?

Je ni kiburi?

Je ni kukosa Uzalendo?

Au je ni kweli Bandari imeuzwa(Jambo ambalo binafsi najua haijauzwa).

Serikali tuseme imakataa kusikiliza Maoni ya wanasiasa wa upinzani labda Kwa kuhofia kuwa watawapa bichwa.

Haya vipi kuhusu Chama cha Wanasheria TLS. Ikiwa hao waliowataalamu wa sheria wameona mkataba unakasoro na unahitaji marekebisho kadhaa iweje serikali ikatae.

Serikali haioni umuhimu wa kufikiria Jambo hili licha ya wataalamu WA Kada husika kushauri.

Ni kweli Katiba inampa mamlaka Rais kuamua Jambo lolote pasipo kuomba ushauri lakini Jambo Hilo lisivunje Katiba Kwa sababu ya kiapo cha kuilinda Katiba.

Lakini kuyapuuza mawazo ya wataalamu wa Kada husika kimakusudi ni kujaribu kuiweka rehani nchi kimakusudi.

Haiwezekani Umeenda hospitalini umeshauriwa na Madaktari kuwa utumiaji wa Dawa Fulani Mpya ambayo hujawahi Kutumia, Kwa jinsi mwili wako ulivyo kuanzia kinga na mifumo ya mwili, itakuletea shida alafu Kwa Makusudi utake Kutumia Dawa hizo Mbaya zaidi unataka familia nzima itumie. Kwa kweli hiyo haina maana nzuri.

Msimamo wangu ni kuwa, serikali Ione haja ya kusikiliza Maoni ya msingi hasa Kwa wataalamu wa sheria kuhusu huo Mkataba. Kama haitaki kusikiliza wanasiasa wenzao basi wasikilize Wanasheria wenye utaalamu wa sheria.

Kipi kinashindikana kuboresha kwenye Huo mkataba? Kwa nini kisiboreshwe ikiwa Watanzania wengi hasa wataalamu WA sheria wameona kuna dosari?

Serikali katika madai yake inasema, pale bandarini sijui wafanyakazi sio waaminifu, sijui wengine ni Wezi ndio wanaozotesha kazi za bandarini. Nilimsikia Spika akizungumzia Jambo hili.

Unajua kauli kama hizo zinajaribu kueleza kuwa serikali Ipo corrupted. Yaani serikali Kabisa inasema pale bandarini sijui kuna Wezi sijui kuna watendaji wabovu, kwani hakuna Mahakama?

Kwani hakuna vyombo vya kushughulikia wahalifu, au ukifanya kazi bandarini upo juu ya sheria kiasi cha kuepuka kuwajibishwa?

Kusema watanzania milioni 60 hakuna waadilifu wa kuweza kufanya kazi katika vitengo nyeti kama bandarini ni kujaribu kutukana taifa. Serikali inashindwa kupika na kutengeneza Vijana waadilifu ambao watafanya kazi zao Kwa ufanisi?

Haya, mitafafuku kama hii Watu wanakosa hoja na matokeo yake kuingiza dini kwenye Siasa.
Kikawaida dini ikishaingia kwenye Siasa inakuwa na nguvu kuliko serikali.

Ili serikali iwe na nguvu ni sharti iweke dini upande wa pili shilingi. Kwa sababu Dini ni upande wa pili wa serikali, au tuseme ni mkono wa kushoto wa serikali.

Serikali inaweza kupuuzia wataalamu, sayansi na uwekezaji na mapesa lakini kamwe haiwezi kupuuzia suala la Dini, ambayo msingi Mkuu ni Imani.

Imani inanguvu kuliko Kitu chochote Baada ya Upendo.

Njia kuu ya kudhibiti Imani na Dini za Watu ni Upendo. Huwezi Kutumia nguvu kudhibiti dini. Ila upendo unaweza Kutumika kudhibiti Dini.

Najua serikali inajua nini chakufanya muda huu. Lakini Njia Bora ni kuyafanyia kazi Yale yanayotolewa na upande wa pili Kwa sababu sio mambo mabaya.

Kupuuzia Watu sio Njia sahihi. Kuwatisha pia sio Njia sahihi. Na pia ikiwa lengo ni kuiletea Maendeleo nchi yetu, kuufuta kabisa huo mkataba sio Njia Sahihi.

Njia sahihi ni kuurekebisha ili ulinde maslahi ya nchi kama ilivyoshauriwa na Watalaamu.

Angalizo, ikiwa kuna kundi la Watu wameingiza maslahi Yao binafsi katika mkataba huu na kuacha Nyuma maslahi ya Watanzania hao ndio wanaotuletea shida na kutugawanya kama taifa.
Na Siku zote kikombe kikivunjika hata kiungwe hakiwi kilekile tena.

Watu wasitumie Dini kuitisha na kuishinikiza serikali au kumyumbisha Rais aliyepo madarakani. Ila kama Rais au kiongozi atakuwa mkaidi na kutoisikiliza Sauti ya wengi basi Watu nao hawatakuwa na wajibu wa kuitii serikali.

Lakini kama serikali inafanya Yale ambayo wananchi wanataka, wakitokea wakaidi washughulikiwe Kwa mujibu wa sheria.

Tunahitaji tuachane na haya mambo.

Imetosha, Muafaka chanya upatikane.

Tuzingatie kwenye hili hakuna mshindi, Ila mshindi awe ni taifa. Kuzozana kwetu kuwe kwaajili ya maslahi ya Nchi.

Muungwana akivuliwa nguo huchutama. Kurekebisha ulipokosea sio kujiabisha Bali ni uungwana. Na uungwana ni vitendo.

Nawatakia Sabato njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
TATIZO NI CCM KILA ANAYEPINGA MKATABA ANAULIZWA DINI AU CHAMA
 
Nahisi wanadhani ndio njia ya kuukosesha maana mjadala, ila hawajui tu kwa hapa wanaleta kasheshe kubwa. Sasa hivi Masheikh baadhi wakiongea na waumini wao wanasema Mama anachukiwa kisa anavaa hijab! Imagine, kutoka kwenye discussion ya bandari mpaka hijab!! Wanawatia moto waumini waone hamna la ziada zaidi ni hijab ya mtu. Haijengi hii, inabomoa.
 
Inawezekana mkataba una kasoro kweli ila ukiwasikiliza wabongo hamna kitu utafanya, watakupangia hadi mambo ya faragha.

Soon masheikh nao watatoa tamko kuunga mkono hoja. Hili sakata lishachukua sura ya kidini, ni ujinga wa kiwango cha juu.
Mashekhe ni watu wenye nidhamu sana usipowachokoza wanaweza kuchagua kukaa kimya, naamini watamuongoza mama vyema lkn hawezi kutoa tamko la kuigemea serikali nao wanajua watakuwa wanaukoleza moto, wataka kimya kama Wabunge tunaowafahamu kuwa ni wachambuzi wazuri wa mijadara mbalimbali, na yewezenaka hao wabunge kuna ahadi wamepewa dpw
 
Inawezekana mkataba una kasoro kweli ila ukiwasikiliza wabongo hamna kitu utafanya, watakupangia hadi mambo ya faragha.

Soon masheikh nao watatoa tamko kuunga mkono hoja. Hili sakata lishachukua sura ya kidini, ni ujinga wa kiwango cha juu.
Tunakaribia njia panda na tukifika hapo itakuwa shida kujua njia ipi sahihi. Bora kurudi au kuendelea?
 
Mama aliiingizwa mkenge na wajanja hakuuelewa vizur.
Kanisa ni sauti ya watu
 
Soon ataufuta au kurekebisha vifungu.
Mkataba unatakiwa uwe 50 kwa 50 kwa faida ya nchi na Sio kama Yale ya kutuachia maandaki kwenye madini.
Tulichofaidika nacho ni kujengewa vyoo
 
Mama aliiingizwa mkenge na wajanja hakuuelewa vizur.
Kanisa ni sauti ya watu

Marekebisho yafanyike.
Yakifanyika alafu Watu wakaleta fyokofyoko tutaona wao( hao Watu) ndio wenye matatizo. Lakini yasipofanyika tutajua tatizo lipo Kwa serikali
 
Mi bado Nina Imani na rais hasa Nia yake ya kuleta mageuzi ya kiuchumi hasa ukilinganisha na tulipotoka. Mageuzi siku zote yanapata upinzani hasa kutoka wale wansofaidika na hali iliyopo. Pia naami rais amesikilia hizi kelele hasa zile ambazo ni genuine na nashuuri zitumike jitihada za closed door zaidi hasa kwa viongozi wetu badala ya kuzidi kuleta migawanyiko kwa wananchi.viongozi wote washirikiane wao kwa wao kwanza ikishindikana ndio watoke hadharani hiyo ndio hekima , mambo yakiharibika hakuna atayepata cha maana zaidi sana watafaidi mawakala WA vita.
Tuibebe Nia hii nzuri kwa Nia nzuri pia katika kutoa ushauri kwa hekima, tulienda amani yetu
 
Umenijibia mkuu. Itakuwa kheri sana kama Waislam wataamua kutotoa Tamko lolote Katika hili swala la BANDARI.
 
Umenijibia mkuu. Itakuwa kheri sana kama Waislam wataamua kutotoa Tamko lolote Katika hili swala la BANDARI.
 
Mi bado Nina Imani na rais hasa Nia yake ya kuleta mageuzi ya kiuchumi hasa ukilinganisha na tulipotoka. Mageuzi siku zote yanapata upinzani hasa kutoka wale wansofaidika na hali iliyopo. Pia naami rais amesikilia hizi kelele hasa zile ambazo ni genuine na nashuuri zitumike jitihada za closed door zaidi hasa kwa viongozi wetu badala ya kuzidi kuleta migawanyiko kwa wananchi.viongozi wote washirikiane wao kwa wao kwanza ikishindikana ndio watoke hadharani hiyo ndio hekima , mambo yakiharibika hakuna atayepata cha maana zaidi sana watafaidi mawakala WA vita.
Tuibebe Nia hii nzuri kwa Nia nzuri pia katika kutoa ushauri kwa hekima, tulienda amani yetu

Ni Kweli.
Nia ya kweli utaiona kwenye kukubali mazuri na Matokeo mazuri. Hiyo ndio Nia ya kweli
 
"ni bora tufe kuliko kuishi kitumwa kwenye nchi yetu" amani amani kwenye unyanyasaji sisi sio wajinga.
wewe mwehu unaropoka tu.Unajua madhara ya vita au unaropoka tu?.Eti ni heri tufe.Naomba uwe mstari wa mbele kupambana siku kikinuka.Je,ukiulizwa umenyanyaswa nini unaweza kujibu?
 
hawa wanalichukulia hili jambo kiulahisi ila naona kabisa red light kwaajili ya huu udini wanao utanga majukwaani watakuja kushtuka Taifa halitawaliki tena
Leo kanisani tumeelezwa maana muungano wa Tanganyika na Zanzibar wengi tulikuwa hatujui chanzo cha huo muungano, Na serikali ilikuwa haijawahi kusema au kuandika mahala popote pale.
 
Dawa ni kurekebisha hayo mambo yaliyoainishwa na wananchi wakitaka yabadilishwe maana maoni yametolewa na watu mbalimbali bila kujali dini,kabila wala utaifa
Serekali iseme tu mkataba huu ni mkataba wa miaka 5 ya trial baada ya hapo tutaangalia either tusign mkataba mrefu au la
 
Back
Top Bottom