Kwani lazima wao? Au labda kilishapokelewa cha juu miaka ya nyuma kwa ahadi ya kupewa hiyo bandari sasa huu ndio wakati wa utekelezaji, nchi ina siri nyingi sana, haiwezekani mother akashupaza shingo namna hii.je hivyo vifungu vikirekebishwa DP World watakubali kuendelea kuwekeza?
hawa wanalichukulia hili jambo kiulahisi ila naona kabisa red light kwaajili ya huu udini wanao utanga majukwaani watakuja kushtuka Taifa halitawaliki tenaKwani lazima wao? Au labda kilishapokelewa cha juu miaka ya nyuma kwa ahadi ya kupewa hiyo bandari sasa huu ndio wakati wa utekelezaji, nchi ina siri nyingi sana, haiwezekani mother akashupaza shingo namna hii.
Dawa ni kurekebisha hayo mambo yaliyoainishwa na wananchi wakitaka yabadilishwe maana maoni yametolewa na watu mbalimbali bila kujali dini,kabila wala utaifa
Natamani UPANDE wa pili, waje na wao watoe TAMKO lenye kuunga MKONO huu "mkataba" tena kwa hoja nzito kama walivyofanya TEC, labda Mh Rais ndio ataamini ya kwamba "MKATABA", huu umeligawa taifa, hivyo haufai, UFUTWE
Inawezekana mkataba una kasoro kweli ila ukiwasikiliza wabongo hamna kitu utafanya, watakupangia hadi mambo ya faragha.
Soon masheikh nao watatoa tamko kuunga mkono hoja. Hili sakata lishachukua sura ya kidini, ni ujinga wa kiwango cha juu.
Hadi tulipofika huyu mtu anahitaji kujiuzulu sababu atalitia Taifa kwenye machafuko.
je hivyo vifungu vikirekebishwa DP World watakubali kuendelea kuwekeza?
Utaambiwa umeandika haya sababu aliyepo ni Mwislamu, mwanamke afu mzanzibari😳😳
Ndugu mbona wanasheria kibao wametoa ufafanuzi kwa yale yanayopingwa? Wakili Msando akiwa namba moja kwenye kutoa utetezi. Halafu sio kila watu wanaopinga wanamaanisha kuwa wana nia njema. Hao wanaoitwa wanasheria nguli wakati mwingine hutumia sheria hizohizo kuiingiza nchi kwenye shida. Wakati Zitto akiwa mbunge na Idris Rashid akiwa boss Tanesco, alipeleka hoja bungeni kuwa serikali inunue mitambo ya Dowans na kujitengenezea umeme ambapo pia Dowans iliahidi mitambo ikinunuliwa watafuta kesi waliyokuwa wamefungua. Wasomi wakapinga na kudai anachoshauri Zitto ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Kilichofuatia ni Dowans kushinda kesi huku mitambo wakiiuzia Symbions na hao Symbions kutuuzia sisi umeme. Kwahiyo wanasheria kama Shivji wanaweza kutumia sheria hizohizo kwa maslahi binafsi.
Robert ameeleza Jambo la Msingi na ameuliza swali ambalo Wenye busara wengi wanajiuliza. Kama watu wengi wanaona kuna shida kwenye Mkataba ikiwemo Mahakama iliyojizongazonga lakini ikatoa hukumu ya Sare pale Mbeya nayo ikasema kuna maeneo kwenye mkataba inayashangaa. Lakini bado serikali na vibaraka wake Bunge wanasema mkataba ubaki kama ulivyo hauna tatizo, nini kiko nyuma ya pazia?Nawaza pengine wale wa upande wa pili wakija na kauli kinzani SI elewi itakuwaje
Sasa ukiufuta si utakuwa umeunga mkono upande mmoja?Natamani UPANDE wa pili, waje na wao watoe TAMKO lenye kuunga MKONO huu "mkataba" tena kwa hoja nzito kama walivyofanya TEC, labda Mh Rais ndio ataamini ya kwamba "MKATABA", huu umeligawa taifa, hivyo haufai, UFUTWE
Wabongo ndio wenye Nchi.
Na watawala ni lazima waongoze nchi kulingana na matakwa ya wananchi hivyo ndivyo Katiba inasema.
Wewe kiongozi unaona unaakili lakini inaongozwa wajinga wengi wanaotaka Jambo Fulani lifanyike alafu hutaki basi achia ngazi.
Watu wamekuchagua kuwaongoza vile wanachotaka(wengi wao) sio vile utakavyo(wachache).