Katika wimbi la kwanza kama nchi tuliweza ku "take risk through herd immunity" kwa hiyo athari za COVID 19 kwa ujumla wake hazikuweza kubainika. Hii ni kwa kuwa tuliacha kwa makusudi kupima watu na hata kuripoti visa na vifo vitokanavyo na gonjwa hali tukijua ili kuwa ni mojawapo ya maazimio ya afya ya kimataifa ambayo "our country had ratified".
Awali tulileta janja janja nyingi "on questioning the efficacy of the protective kits". Sasa limekuja wimbi la pili, na kwa kuwa huduma za kuaminika hutolewa na hospitali nyingi binafsi, ambazo watendaji wake wengi ni waumini waaminifu wa dini na madhehebu mbalimbali. Wameona sehemu stahiki ya kupeleka ukweli juu ya hali halisi ilivyo ni kwa viongozi wao wa dini.
Watu makini wakiwemo waliopo hata serkalini, wanatambua serikali yao inafanya kila jtihada kukwepa gharama za kuweza kukabiliana kisayansi na gonjwa hili. Ndiyo maana inacheza mchezo wa bahati nasibu dhidi yake. Mgeni kesha ingia ndani ya nyumba yetu kupitia wimbi jipya, sasa si wakati wa kuleta masikhara isipokuwa ni kupitia kukabiliana na gonjwa hili kwa vitendo vyenye tija, kabla hatujajikuta tumechelewa sana kama taifa.
Hongereni sana viongozi wa dini kwa kujitokeza hadharani na kupata ujasiri wa kuandika waraka na hata kuongelea wimbi hili jipya hadharani na tena kwa uwazi mkubwa. Hakuna heshima yoyote ile wala si uzalendo kuungana na watawala ambao haiyumkini wapo "naive" juu ya tishio halisi la gonjwa hili na hata kujaribu kuficha ukweli halisi unaolihusu taifa letu.