#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Toa maoni nini kifanyike badala ya kila mmoja kulialia na kutupa lawama huku na kule.

Watanzania tunapaswa kupambana kivyetu kwa sababu Corona haijatuathiri kama yale mataifa ya Ulaya tutiane moyo badala ya kutishana.

Karibu kwa maoni.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani yale maombi yetu yame-expire? Kama vipi labda tufanye tena maombi na kuwaombea na wengine, kwa vile sisi ni vipenzi vya mungu zaidi ya misikiti mikuu ya Makka n Madina au kanisa la Roma!
 
Mambo matatu tu yanahitajika.
1. TAARIFA SAHIHI kuhusu hali ya ugonjwa ilivyo hapa Tanzania.
2. USHAURI WA KITAALAMU uzingatiwe.
3. JAMII NZIMA ISHIRIKISHWE namna ya kuukabili ugonjwa.
 
Hatuwezi kupambana na Corona ikiwa bado tumejificha kwenye huu upumbavu;
-Kutangaza kuwa Corona haipo Tanzania.
-Kuaminisha watanzania kuwa Nyungu, madawa ya kienyeji nk vinatosha kutibu Corona.
-Kuaminisha kuwa chanjo za Corona zimetengenezwa ili kuja kutumaliza.
-Kuficha takwimu sahihi kuhusu vifo na maambukizi ya corona.
-Kukaa kusubiri rais aseme hakuna Corona ili tushangilie.
 
Toa maoni nini kifanyike badala ya kila mmoja kulialia na kutupa lawama huku na kule.

Watanzania tunapaswa kupambana kivyetu kwa sababu Corona haijatuathiri kama yale mataifa ya Ulaya tutiane moyo badala ya kutishana.

Karibu kwa maoni.

Maendeleo hayana vyama!
Iache kujiimbia mapambio afya ya imma ni zaidi ya madaraka.
 
Toa maoni nini kifanyike badala ya kila mmoja kulialia na kutupa lawama huku na kule.

Watanzania tunapaswa kupambana kivyetu kwa sababu Corona haijatuathiri kama yale mataifa ya Ulaya tutiane moyo badala ya kutishana.

Karibu kwa maoni.

Maendeleo hayana vyama!
Ihabarishe watu kuhusu hatari iliyopo na hatua stahiki za kuchukua kwa mtoto mmoja mmoja, taasisi na mashule
 
Hii wimbi la pili msiwe na mashaka nayo tutaishinda kama tulivyoishinda ya kwanza. Huko mnakosema kuna chanjo watu wanapukutika kila siku halafu bado unaamini chanjo itafanya kazi?
 
IMG_20210129_162645.jpg
 
Katika wimbi la kwanza kama nchi tuliweza ku "take risk through herd immunity" kwa hiyo athari za COVID 19 kwa ujumla wake hazikuweza kubainika. Hii ni kwa kuwa tuliacha kwa makusudi kupima watu na hata kuripoti visa na vifo vitokanavyo na gonjwa hali tukijua ili kuwa ni mojawapo ya maazimio ya afya ya kimataifa ambayo "our country had ratified".

Awali tulileta janja janja nyingi "on questioning the efficacy of the protective kits". Sasa limekuja wimbi la pili, na kwa kuwa huduma za kuaminika hutolewa na hospitali nyingi binafsi, ambazo watendaji wake wengi ni waumini waaminifu wa dini na madhehebu mbalimbali. Wameona sehemu stahiki ya kupeleka ukweli juu ya hali halisi ilivyo ni kwa viongozi wao wa dini.

Watu makini wakiwemo waliopo hata serkalini, wanatambua serikali yao inafanya kila jtihada kukwepa gharama za kuweza kukabiliana kisayansi na gonjwa hili. Ndiyo maana inacheza mchezo wa bahati nasibu dhidi yake. Mgeni kesha ingia ndani ya nyumba yetu kupitia wimbi jipya, sasa si wakati wa kuleta masikhara isipokuwa ni kupitia kukabiliana na gonjwa hili kwa vitendo vyenye tija, kabla hatujajikuta tumechelewa sana kama taifa.

Hongereni sana viongozi wa dini kwa kujitokeza hadharani na kupata ujasiri wa kuandika waraka na hata kuongelea wimbi hili jipya hadharani na tena kwa uwazi mkubwa. Hakuna heshima yoyote ile wala si uzalendo kuungana na watawala ambao haiyumkini wapo "naive" juu ya tishio halisi la gonjwa hili na hata kujaribu kuficha ukweli halisi unaolihusu taifa letu.
 
Tukubali kwanza tatizo lipo, hatua ya pili iwe kusisitiziana kuchukua tahadhari kila inapowezekana.

Kama Mtu itakukumba ikukumbe tu lakini walau uwe umejaribu kujikinga badala ya kukaa tu fwaaa kwa sababu Wenye Mamlaka wamesema haipo.
 
Ni ajabu sana kwa wabezaji...kuna wakati natamani hawa wabezaji wajidhihirishe na wabeze dhahiri shahiri.....maana wana kera sana
 
Jamani tunapaswa kuwa makini sana na haya mafua, kuna vitu vingi hatuvielewi! Hebu someni hapa, nimekutana nayo njiani!
 

Attachments

  • IMG-20210131-WA0001.jpg
    IMG-20210131-WA0001.jpg
    80.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom