#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Acha zako bhana,!

Watu wamejifungia ndani wakiwa na maambukizi ya watu wasiozidi 100 na vifo visivyozidi 10 na bado wakafa kwa maelfu kisha unasema walichelewa?
We unaongelea data gani mkuu hizo za maelfu? Mpaka sasa new cases ni 50,000 za Marekani nyuma ya France na China akiongoza. Wewe hizo taarifa za vifo vya maelfu umezipatia wapi?!
 
Mpaka sasa serikali haiweki wazi kuhusu lolote lile linaloendelea nchini, and we're already doomed sababu wabongo wengi wanasubiri matamko ya wanasiasa ndiyo wafanye maamuzi,

Wanao take precautions hivi sasa ni asilimia ndogo sana tofauti na mwaka Jana tamko lilivyotoka, hizi akili zetu hizi, watu wanaona misiba imeongezeka lakini bado wanaishi kawaida kusubiri kuambiwa na bahati mbaya hakuna wa kuwaambia..!

Ukija kwa wale matomaso walojaa mitandaoni ndiyo wanazidi kuwapa watu false hopes, eti ni hofu tu..! Hofu m*f' huku watu wanapukutika..?
 
Tuko vizuri-.jpg
 
Habari wakuu, ndio hivyo changamoto ni yetu sote,Kulaumu hakutasaidia chochote. Kulalamika nako hakutasaidia chochote ni bora tukachukua hatua kila mmoja kumuomba MUNGU kwa imani yake atuepushe, atuondolee kabisa janga hili katika nchi yetu. Ni kweli Mungu alituvusha ila wengi waligeuka nyuma na hawakuamini. Mtakuja ambao mtakataa its OK lakini ukweli ulikuwa ni huo.

Kwahivyo, kila mmoja kwa imani yake aombe atie dua janga hili lipite mbali, hata kama hutaondoka, hutaondokewa na mpendwa kumbuka kuna kazi zinasimama kwasababu ya chan gamoto kuna familia zinaharibika kwasababu ya Changamoto.

Mungu uliyewavusha wana wa Israel bahari ukaifanya nchi kavu ni wewe tunakuita. Tunatubu utusamehe kwa kutokukuamini katikati ya machozi yetu utusimamie, Mungu tuepushie tuondolee balaa hili Yarabi wengine tuna watoto wadogo sana hata tukiwatizama tunaishia kulia tu kuwaacha ni uchungu usiopimika. Wengine ni maboss zetu Mungu Riziki yetu inapitia mikononi mwao wanaondoka Mungu. Tutapatia wapi Riziki? Wengine viongozi wa Dini, wengine ma wengine ee Mungu wewe ndie kimbilio kaa nasi uvuli wako usiondoke Tanzania.

Tuondolee hofu maana ni mlango wa kifo, tupe kutulia, ukatuongoze nn cha kufanya. Hata huyu Mzee aliyeamua kukutegemea wewe wanampiga mawe mtie Busara na hekima asiingiwe kigeugeu chochote. Anasemwa kwanini alikuchagua Mungu usimuache mpe hekima ya nini akifanye. Sijaona mwenye haki aliyekutegemea ukamwacha au akaaibika kamwe; kaa nasi Mungu tupiganie usituaibishe Mungu sisi tulioamua kukutazama Yarabi uisikie dua yetu utujibu wala usikae kimya tumeomba na kushukuru.

Amina.

Jamani karibuni kwa imani yako ni kuachia dua yako tu tusiweke mabishano au mambo ya katikati ya Uzi kuandika mitano tena naamini humu ndani watu ni wasomi na very matured hii ni kwaajili yetu Ndg waTz wote.
 
We unaongelea data gani mkuu hizo za maelfu? Mpaka sasa new cases ni 50,000 za Marekani nyuma ya France na China akiongoza. Wewe hizo taarifa za vifo vya maelfu umezipatia wapi?!
Mkuu kwani marekani mapaka sasa hivi ana vifo vingapi na visa vingapi vya maambukizi tangu huu ugonjwa ulipotiwe?
 
Hali ni mbaya kwa sasa hilo halina ubishi.

Cha kushangaza serikali bado iko na msimamo wake kwamba nchi haina korona, lengo ni nini hasa kuhusu huu msimamo wa serikali wakati hili ni janga la dunia nzima?

Kuna ubaya na madhara gani kutoa tahadhari kwa watu ili wajikinge?

Sasa hivi hakuna anaejali tena au kuchukua tahadhari, ni wachache sana wanaofanya hivyo.
cha kushangaza ni wewe bado huchukui hatua za kujikinga.
serikali imeshatoa maelekezo kila mtu achukue tahadhari ya kujikinga na pia kutumia dawa zetu za asili.
hakuna kingine zaidi ya hucho.
ni kama vile unavyo ambiwa jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa ukimwi...ukikiuka taratibu za kujikinga lazima utaambukizwa ukimwi na matokeo yake ni kifo.
Tujikinge na pia tutumie dawa zetu asili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakosea sana kama huoni damage ya kusema Tanzania hamna Corona, siwezi kuendelea kubishana na wewe sababu umeamua mwenyewe kua mbishi tu, Leo kama Rais sema Tanzania hakuna ukimwi halafu seat back and watch the impact...
Sikia dada! Hapa tz kutangaza tu corona ipo huku huna la kufanya inasaidia nini?

Nmekutolea mfano kwamba huko ambako kila hatua mnazosema zimechukuliwa na maelfu ya watu wamekufa unataka sisi tukuchukue hatua gani?
 
Akili za wapi hizi!Mungu huwa halipi maombi bali huwa analipa jitihada.Usitegemee Corona itaisha Tanzania kwa kujidanganya kuwa haipo na kujificha kwenye mgongo wa maombi badala ya kukiri kuwa ipo na kuja na strategy sahihi za kupambana nayo.Taifa linaangamia kwa sababu ya akili kama za mleta mada!
 
Mpaka sasa serikali haiweki wazi kuhusu lolote lile linaloendelea nchini, and we're already doomed sababu wabongo wengi wanasubiri matamko ya wanasiasa ndiyo wafanye maamuzi,

Wanao take precautions hivi sasa ni asilimia ndogo sana tofauti na mwaka Jana tamko lilivyotoka, hizi akili zetu hizi, watu wanaona misiba imeongezeka lakini bado wanaishi kawaida kusubiri kuambiwa na bahati mbaya hakuna wa kuwaambia..!

Ukija kwa wale matomaso walojaa mitandaoni ndiyo wanazidi kuwapa watu false hopes, eti ni hofu tu..! Hofu m*f' huku watu wanapukutika..?
UMeongea vizuri,watu wanasubiri tangazo kuna corona
They don't take any precautions.
Tumeambiwa tunawe na maji tiririka, tuvae barakoa,tutumie sanitizer, tukeep distance
Bado tunasubiri tangazo kuna nchi INA corona, this is ignorance of the highest caliber
 
Kwanza viongozi wakubali ipo hatuwezi ili tuoneshe utiifu kwa Mungu
 
Tunasubiri nyungu version 4.5 kutoka kwa muheshimiwa jafo, huku tukiendelea kumuomba Mungu atuepushe.
 
Sikia dada! Hapa tz kutangaza tu corona ipo huku huna la kufanya inasaidia nini?

Nmekutolea mfano kwamba huko ambako kila hatua mnazosema zimechukuliwa na maelfu ya watu wamekufa unataka sisi tukuchukue hatua gani?

Nimekuelewesha naona hunielewi huko ambako unasema watu wamekufa je wangesema hakuna corona nchini kwao, wananchi wasichukue any measures impact yake vifo wangekua wamekufa wangapi? Huoni Kama ingekua disaster zaidi ???????.....nimekupa mfano wa ukimwi, kwamba Rais atangaze hakuna ukimwi nchini, uone impact yake

,,,sidhani kama kuna nchi imeweza ku control hili janga 100%, kila nchi inafanya jitihada kuweka infection low mpaka tutakapoweza kulidhibiti hili janga, na katika kutimiza hili tunashauriwa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka Misongamano Sio kwamba itamaliza tatizo bali itapunguza maambukizi, ,

again is to be irresponsible kuwaambia wananchi wako hamna corona nchini , sisi sio kisiwa,,,,,
 
Kwanza nitoe pole kwa wote waliofikwa na misiba ya wapendwa wao. Wapumzike kwa amani.

Kwa hakika sasa vifo vimeongezeka, hapa nazungumzia watu wenye nyadhifa mbalimbali serikalini, achilia mbali wananchi wa kawaida ambao habari zao hazitangazwi. Kama hawa viongozi hawafi kwa corona, je ni nini kinachowaua tena kwa mfululizo namna hii?

Kama sio corona basi hali ya hospitali na huduma zetu za afya nchini ni dhaifu mno tofauti kabisa na jinsi hii serikali inavyojinasibu kuboresha miondumbinu ya afya. Kama watu wanaopewa first class treatment on everything wanapoteza maisha hivi basi raia wa kawaida don't stand a chance.

Kama ni corona, serikali ifanye jitihada za makusudi na za haraka za kuongeza vifaa tiba na kuhimiza tahadhari juu ya huu ugonjwa kuokoa maisha ya watu.
Yaani sasa hivi kila kifo ni corona eeh! Kwa hiyo kabla ya kuwepo corona vilisababishwa na nini!?
Hebu tuliza munkari! Pressure, kisukari, AIDS, ajali, pneumonia, malaria, saratani, nk ni baadhi tu!
 
Yaani sasa hivi kila kifo ni corona eeh! Kwa hiyo kabla ya kuwepo corona vilisababishwa na nini!?
Hebu tuliza munkari! Pressure, kisukari, AIDS, ajali, pneumonia, malaria, saratani, nk ni baadhi tu!
Huyu naye, ukibishana na watu wa aina yako kwanza unaweza jikuta hata wamekuambukiza 'viakili vyao'..!
 
Back
Top Bottom