We unaongelea data gani mkuu hizo za maelfu? Mpaka sasa new cases ni 50,000 za Marekani nyuma ya France na China akiongoza. Wewe hizo taarifa za vifo vya maelfu umezipatia wapi?!Acha zako bhana,!
Watu wamejifungia ndani wakiwa na maambukizi ya watu wasiozidi 100 na vifo visivyozidi 10 na bado wakafa kwa maelfu kisha unasema walichelewa?
Mkuu kwani marekani mapaka sasa hivi ana vifo vingapi na visa vingapi vya maambukizi tangu huu ugonjwa ulipotiwe?We unaongelea data gani mkuu hizo za maelfu? Mpaka sasa new cases ni 50,000 za Marekani nyuma ya France na China akiongoza. Wewe hizo taarifa za vifo vya maelfu umezipatia wapi?!
cha kushangaza ni wewe bado huchukui hatua za kujikinga.Hali ni mbaya kwa sasa hilo halina ubishi.
Cha kushangaza serikali bado iko na msimamo wake kwamba nchi haina korona, lengo ni nini hasa kuhusu huu msimamo wa serikali wakati hili ni janga la dunia nzima?
Kuna ubaya na madhara gani kutoa tahadhari kwa watu ili wajikinge?
Sasa hivi hakuna anaejali tena au kuchukua tahadhari, ni wachache sana wanaofanya hivyo.
Sikia dada! Hapa tz kutangaza tu corona ipo huku huna la kufanya inasaidia nini?Unakosea sana kama huoni damage ya kusema Tanzania hamna Corona, siwezi kuendelea kubishana na wewe sababu umeamua mwenyewe kua mbishi tu, Leo kama Rais sema Tanzania hakuna ukimwi halafu seat back and watch the impact...
Utanishtua twende woteMe naona tuhamie tuu chato kwa muda kumfuata baba,hawezi kujificha pekeake watoto tunakufa....mm naenda huko huko aisee kama kufa tukafe wote..
UMeongea vizuri,watu wanasubiri tangazo kuna coronaMpaka sasa serikali haiweki wazi kuhusu lolote lile linaloendelea nchini, and we're already doomed sababu wabongo wengi wanasubiri matamko ya wanasiasa ndiyo wafanye maamuzi,
Wanao take precautions hivi sasa ni asilimia ndogo sana tofauti na mwaka Jana tamko lilivyotoka, hizi akili zetu hizi, watu wanaona misiba imeongezeka lakini bado wanaishi kawaida kusubiri kuambiwa na bahati mbaya hakuna wa kuwaambia..!
Ukija kwa wale matomaso walojaa mitandaoni ndiyo wanazidi kuwapa watu false hopes, eti ni hofu tu..! Hofu m*f' huku watu wanapukutika..?
Sikia dada! Hapa tz kutangaza tu corona ipo huku huna la kufanya inasaidia nini?
Nmekutolea mfano kwamba huko ambako kila hatua mnazosema zimechukuliwa na maelfu ya watu wamekufa unataka sisi tukuchukue hatua gani?
Yaani sasa hivi kila kifo ni corona eeh! Kwa hiyo kabla ya kuwepo corona vilisababishwa na nini!?Kwanza nitoe pole kwa wote waliofikwa na misiba ya wapendwa wao. Wapumzike kwa amani.
Kwa hakika sasa vifo vimeongezeka, hapa nazungumzia watu wenye nyadhifa mbalimbali serikalini, achilia mbali wananchi wa kawaida ambao habari zao hazitangazwi. Kama hawa viongozi hawafi kwa corona, je ni nini kinachowaua tena kwa mfululizo namna hii?
Kama sio corona basi hali ya hospitali na huduma zetu za afya nchini ni dhaifu mno tofauti kabisa na jinsi hii serikali inavyojinasibu kuboresha miondumbinu ya afya. Kama watu wanaopewa first class treatment on everything wanapoteza maisha hivi basi raia wa kawaida don't stand a chance.
Kama ni corona, serikali ifanye jitihada za makusudi na za haraka za kuongeza vifaa tiba na kuhimiza tahadhari juu ya huu ugonjwa kuokoa maisha ya watu.
Huyu naye, ukibishana na watu wa aina yako kwanza unaweza jikuta hata wamekuambukiza 'viakili vyao'..!Yaani sasa hivi kila kifo ni corona eeh! Kwa hiyo kabla ya kuwepo corona vilisababishwa na nini!?
Hebu tuliza munkari! Pressure, kisukari, AIDS, ajali, pneumonia, malaria, saratani, nk ni baadhi tu!