Ikiwa tulinusurika hapo awali na Covid_19 kwa kufuata taratibu tulizopewa na wataalamu za kunawa mikono kwa maji tiririka (ilikuwa kila sehemu kuna ndoo ya maji na sabuni )na sabuni,kutumia vitakasa mikono,kuepuka kuwa katika makundi na kushikana mikono,kuepuka kujishika maeneo ya usoni,kutumia njia za asili za kujifukiza na utumiaji wa vyakula,viungo au matunda vinavyoimarisha kinga ya mwili,kufanya mazoezi ya mwili,kuvaa barakoa na kuepuka safari zisizo na ulazima.
Serikali pia iliamrisha maeneo ya starehe yapewe utaratibu mzuri ili kukinga wateja na Covid_19.
Hali ya sasa hayo mambo ni kama hayajatiliwa mkazo kweli kweli,hata yale maeneo yaliyotengwa kupokea wagonjwa hayapo tena!!!
Nashauri viongozi wa juu toeni maelekezo chini haya mambo yatekelezwe haraka sana ili kunusuru umma wa Tanzania.
Pamoja na kumuomba MWENYENZ MUNGU haya pia yalichangia kwa kiasi kikubwa.
Acheni woga toeni maelekezo kwa barua ili kutunusuru na Gonjwa hili kabla halijasambaa zaidi.
MWENYENZ MUNGU IBARIKI TANZANIA, MWENYENZ MUNGU IBARIKI DUNIA.