#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kuhusiana na Corona sio mbali wanaotuongoza wataachana na aibu ya kuukiri ukweli. Watajitokeza na kutoa mwongozo kukabiliana na janga hili badala ya kujikita kubishana na hali halisi
 
Afe nani ili tushituke? Afe nani tushawishike kufunga shule na vyuo? Wafe kina nani ili daladala na mabasi mengine ya abiria yasijae hadi pomoni? Afe nani tuzuie mashabiki viwanjani na katika kumbi za starehe? Nani afe ili Waziri wa Afya atoke hadharani akiri hatari inayotukabili? Ukimya wetu pengine ni jawabu la kwamba tumepanga sote tufe! Eeee Mungu Baba Tuokoe.

By Manyerere Jackton

WA.jpg
 
Ikiwa tulinusurika hapo awali na Covid_19 kwa kufuata taratibu tulizopewa na wataalamu za kunawa mikono kwa maji tiririka (ilikuwa kila sehemu kuna ndoo ya maji na sabuni )na sabuni,kutumia vitakasa mikono,kuepuka kuwa katika makundi na kushikana mikono,kuepuka kujishika maeneo ya usoni,kutumia njia za asili za kujifukiza na utumiaji wa vyakula,viungo au matunda vinavyoimarisha kinga ya mwili,kufanya mazoezi ya mwili,kuvaa barakoa na kuepuka safari zisizo na ulazima.

Serikali pia iliamrisha maeneo ya starehe yapewe utaratibu mzuri ili kukinga wateja na Covid_19.

Hali ya sasa hayo mambo ni kama hayajatiliwa mkazo kweli kweli,hata yale maeneo yaliyotengwa kupokea wagonjwa hayapo tena!!!

Nashauri viongozi wa juu toeni maelekezo chini haya mambo yatekelezwe haraka sana ili kunusuru umma wa Tanzania.

Pamoja na kumuomba MWENYENZ MUNGU haya pia yalichangia kwa kiasi kikubwa.

Acheni woga toeni maelekezo kwa barua ili kutunusuru na Gonjwa hili kabla halijasambaa zaidi.

MWENYENZ MUNGU IBARIKI TANZANIA, MWENYENZ MUNGU IBARIKI DUNIA.
 
We jitilie msisitizo mwenyewe na jamaa zako, serikali haiwezi kupoteza Muda na vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku!!!
 
Kila MTU achukue tahadhari kivyake na mwisho wote tutakuwa salama.Kama nakumbuka vyena sasa hivi hakuna anayejadili ukimwi tunachujua tahadhar wenyewe kuvaa condom.
 
Mpaka saa 99% ya wanaoondoka na COVID ni watu wazima na wazee hasa kuanzia miaka 55 na kuendelea. Ukichunguza kwa umakini utagundua watu wengi wanakufa kwa changamoto ya kupumua hata hao watu wazima ni watu wa class fulani hasa wanaotembelea na kukaa kwenye viyoyozi kwenye magari, maofisini na majumbani.

Wenyewe wanaona wapo tofauti kumbe ndo wanafuga virusi kwenye baridi. Kwa joto la Dar na kubanana kwenye mwendokasi na madaladala tungezika watu 400 kila siku. Hata wazee wanaokufa hakuna mzee wa Tandale,Mbagala wala Manzese. Ni haohao wastaafu vigogo wa zamani waliofunga ma AC kwenye majumba yao.

Hivi virusi vya Corona haviwezi survive joto la Dar ndo maana daladala bado ni safe hata ukibanana kuliko lift ya Rav 4 mpya ya mwanasheria aliyevaa tai kwenye kiyoyozi.

Ukiingia kwenye WhatsApp group zao wanaojiita wanasheria wasomi kila siku TANZIA kumbe wanafuga virusi kwenye magari na maofisini kwenye viyoyozi.

Kuhakiki hilo hata mwaka jana miezi ya joto ulaya Mambo yalirudi kawaida shule,masoko,maofisi vikafunguliwa. October mwishoni hali ikawa mbaya tena. Hadi June hali itakuwa shwari tena sababu miezi ya baridi kwao itakuwa imeisha.

Hitimisho ni kuwa kwa wanaofanya kazi maofisi yenye viyoyozi na muda mwingi kuwa kwenye viyoyozi hata wanaposafiri, vaa barakoa muda wote, sanitize muda wote, kaa nyumbani kama sio muhimu kutoka, usisahau kuchemsha mix ya tangawizi na limao mara 2 kwa siku(muhimu).

Huku mtaani kwenye madaladala tuachie sisi tuliokwishakuota sugu, viCOVID vinaingia na kupotea vyenyewe daily kutokana na kuchumia juani. Kwa wale wabishi mnaokomaa na serikali itoe tamko endeleeni kusubiri kama mnadhani itawasaidia lolote. Jikinge na uwakinge na wenzako.
 
Mpaka saa 99% ya wanaoondoka na COVID ni watu wazima na wazee hasa kuanzia miaka 55 na kuendelea. Ukichunguza kwa umakini utagundua watu wengi wanakufa kwa changamoto ya kupumua hata hao watu wazima ni watu wa class fulani hasa wanaotembelea na kukaa kwenye viyoyozi kwenye magari, maofisini na majumbani...
Mkuu hao unaowajua ni watu maarufu. Unadhani Covid-19 inataka watu maarufu pekee
 
Mpaka saa 99% ya wanaoondoka na COVID ni watu wazima na wazee hasa kuanzia miaka 55 na kuendelea. Ukichunguza kwa umakini utagundua watu wengi wanakufa kwa changamoto ya kupumua hata hao watu wazima ni watu wa class fulani hasa wanaotembelea na kukaa kwenye viyoyozi kwenye magari, maofisini na majumbani....
Wewe kama mfuasi wa namba moja, unamshauri nini kuhusu hili.
 
Kuanzia mwezi wa kumi na mbili hadi leo nimefiwa na ndugu zangu wa damu sita.
Hii misiba yote ni ya ghafla sana, kuishiwa pumzi na kushindwa kupumua.
Hii hali najiuliza Ni kwangu tu?
Tujulishane hali ya kadudu ilivyo.
IMG-20210216-WA0017.jpg
 
Back
Top Bottom