Ni kweli kabisa, Mungu tayari ameshajibu. Ndio maana hata hao mapadri wa TEK wameokoteza vifo vya kutoka Januari. Habari ya misiba imepungua Sana na ni vifo vya kawaida!
 
Balozi wa Amerika hapa nchini aende kwao akawashsuri jimbo la Texas kuendelea kuchukua tahadhari na kuendelea kuwa na lockdown!!
 
Nikirejea usemi wa raisi mh Magufuli anapozungumzia corona nikimnukuu,"Hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko corona".Niweke wazi kwamba sina lengo lakuleta hofu wala sijatumwa na mabeberu ila kuusema ukweli juu ya janga la corona tutaokoa maisha ya wengi.

Rafiki yangu alifiwa na mjomba wake wiki iliopita hospitali ya Mount Meru lakini mshangao ndugu waliambiwa mochwari imejaa hivyo wajaribu kutafuta hifadhi nje ya hospitali.Ndugu walihangaika kutafuta hifadhi hospitali nyingine zilizopo jijini Arusha kama Seriani na nyinginezo lakini nako hali ikawa hivyohivyo nako kumejaa.

Kimsingi kunaviashiria kwamba corona ni tatizo na ndio chanzo cha kuongezeka kwa vifo nchini.Sidhani kama hospital kubwa kama Mount Meru ina mochwari ndogo kiasi cha kuzidiwa lazima kunajambo haliko sawa.

Sote ni mashahidi tumesikia taarifa ya kanisa katoliki wakieleza idadi ya mapadre,masista na watawa waliokufa ndani ya kipindi kifupi kwa changamoto za upumuaji.Kinachosikitisha taarifa hii haijaipendeza serikali badala ya kuhangaika na corona wameanza kutoa onyo kwa utoaji taarifa zihusuzo corona.

Ni vema serikali yetu ikaonesha seriousness kwenye mapambano ya corona kwani ni dhahiri viongozi wetu bado hawajaonesha mkazo kwenye mapambano ya janga hili.Sisi sote tunaiunga mkono serikali yetu kwenye msimamo kama wakitoweka lockdown lakini msukumo lazima uwekwe kwenye vyombo vya usafiri visijaze kupitiliza,maji tiririka,walau miili ya corona isimamiwe na watu wa afya wakati wa maziko kama mwanzo.

Wiki chache zilizopita mh Raisi akiwa kanisani alimpongeza padri kwakutokuvaa barakoa jambo ambalo yeye kama kiongozi wa nchi ameonesha kwenda tofauti na ushauri wakisayansi.

CORONA ipo tuchukue hatua sisi kama wananchi wenyewe kwani ni dhahiri viongozi wetu hawaeleweki.

Nimalizie kwakusema lengo langu si kuleta taharuki,kama habari hizi si za kweli ni jambo jema ila ni vizuri wakalifuatlia kuliko kila mnapoambiwa ukweli mnakimbilia kwenye vita vya uchumi/vibaraka wa mabeberu mnaacha kuhangaika na hoja ya msingi.
 
Kuhusu Korona kama ni wakufa utakufa tuuu, wala tusitishane sana , wa kusurvive atasurvive nothing to do , gonjwa halina dawa hlo , juzi nimezika babu yangu hvi hvi, kwenye mazishi ndo mana huwa nawasifu waislamu , hakuna kupoteza mda , mtu amekufa weka kaburini immediately watu waendelee na mambo mengine , ...

Maiti mpak zinarundikana mochwari, zinamsubiri Nani ???? Aaah
 
Lengo sio kutishana ila ukiwaamisha watu kwamba tuko vizuri hawachukui tahadhari mwisho maambukizi yanaongezeka,huku vijijini sasahivi wanasema corona na ugonjwa wa matajiri hapa utaona hawa watu wanahitaji kuelimishwa vinginevyo tunapoteza nguvu kazi,hakuna mwenye lengo lakuleta taharuki ila ni vema tahadhari ziwepo
 
Mtu akishakufa na thamani yake inakua imeisha tayari, inatakiwa akazikwe bila kuchelewesha , Sasa wafu wanahifadhiwa ili uweje , mpaka wanajaza machwari.
Tuendelee kuchukua tahadhari corona ipo
 
Una maana gani unaposema ugonjwa hauna dawa?

Kwani Waziri wa Fedha Dr.Philip Mpango alitumia dawa gani mpaka ameweza kupona?
 
Kama kuna usafiri kwanini alazwe mortuary?

Wakati mwingine watu wanataka maiti ikae hata wiki sijui maana yake ni nini
 
Nimesoma Waraka wa Katibu wa TEC na nimesikiliza clip ya Mwanaharakati mmoja. Kwa maneno yangu tunaelekea pabaya. Watanzania tupendane sisi ni nchi moja, wamoja na tuna mshikamano. Yale maneno ya yule Mwanaharakati kwa kweli hayapendezi hata kidogo.
 
Nimesoma Waraka wa Katibu wa TEC na nimesikiliza clip ya Mwanaharakati mmoja. Kwa maneno yangu tunaelekea pabaya. Watanzania tupendane sisi ni nchi moja, wamoja na tuna mshikamano. Yale maneno ya yule Mwanaharakati kwa kweli hayapendezi hata kidogo.
Ungeyaweka hapa hayo maneno au hiyo clip nasi tusikilize ndipo tuchangie.!
 
Nikirejea usemi wa raisi mh Magufuli anapozungumzia corona nikimnukuu,"Hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko corona".Niweke wazi kwamba sina lengo lakuleta hofu wala sijatumwa na mabeberu ila kuusema ukweli juu ya janga la corona tutaokoa maisha ya wengi...
ni kawaida mochwari kujaa kipindi cha kabla ya corona?
 
Tuacheni utani huu ugonjwa mikoa mingine Kuna nafuu ukienda Moshi Kijiji kimoja kwa siku wanaweza wakafa watu mpaka watatu.pengine Ni kwa sababu ya muingiliano wa pale himo ila bado wengine wanatoka huko mikoa mbalimbali.

Imefikia mpaka wachaga wanaogopa kurudi nyumbani..acheni tu tufe maana si mlishasema ugonjwa hamna Sasa mnaona aibu kusema upo.
 
Wanakunywa sana pombe hawa. Huenda ikawa sababu.


Ni utani tu.
 
Ni watu wa rika gani ambao wanafariki..??
 
Ushauri ukitaka kujiua usijiue nenda Moshi.
Ndugu zangu Wahehe mmeelewa lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…