#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Mkuu pole sana naona thread yako imegeuka kua coment, hivi nyie mods JamiiForums hua hamheshimu muda mtu anaotumia kuandika thread?
Aaah hawa jamaa(mods) huwa ni wavivu wa kusoma wakiona Covid tu wanaunganisha uzi na wengi wao Wana upeo mdogo. Hawawezi kuona utofauti Kati ya uzi na uzi. Mi naongelea kitu kingine kuhusu Covid wameunganisha na uzi wa serikali isiwaache watu kwenye mataa.
 
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.

Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.

Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc

Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo

Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc

Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.

Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!

Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.

Tunataka kusikia kauli ya serikali. Je, Corona ipo Tanzania? Je, serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?

Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?

Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana! Je, ngoma imerudi kama mwaka jana?

Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata.

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
Nionavyo mimi suala la korona serikali inalichukulia kama vita na Watanzania ni Askari wake. Watakaokufa tutawazika na watakaobaki wataendelea na mapambano maisha yaendelee.
 
Nionavyo mimi suala la korona serikali inalichukulia kama vita na Watanzania ni Askari wake. Watakaokufa tutawazika na watakaobaki wataendelea na mapambano maisha yaendelee.

Serikali yenye akili huwa haipeleki askari wake msitari wa mbele bila nyenzo muhimu, taarifa muhimu, userious na ari ya kutaka kushinda na silaha thabiti siyo mishale la sivyo adui atafyeka askari wote!
 
Sasa isiwaache kwenye mataa kivipi yaani unataka kusema tusitoke ndan!? Fara ww af ndiomana jf hatuishi kusumburiwa naserikali kwa mambo kama haya
 
Serikali yenye akili huwa haipeleki askari wake msitari wa mbele bila nyenzo muhimu, taarifa muhimu, userious na ari ya kutaka kushinda na silaha thabiti siyo mishale la sivyo adui atafyeka askari wote!
Inategemea na msimamo na maono ya kamanda mkuu. Kama anaamini in numbers kwamba akiweka askari wengi mbele watajufa wengi lakini hawataisha wote na watakaobaki wataleta ushindi. Huyu ni kamanda anaetaka ushindi bila kujali sacrifice Lakini kuna kamanda anaeenda vitani akitafuta ushindi huku akijaribu kupunguza kwa kadri ya uwezo wake kupunguza athari kwa askari wake. Hawa ni makamanda wawili tofauti.
 
Mabibi na mabwana sera ya Corona ya serikali ya awamu hii iko wazi. Yaani ni kila mtu na lwake.

Kwani pana hata haja ya kujidanganya tena? Kila mtu anajijua yupo katika kundi lipi katika mawili tu yaliyopo. Yaani kundi salama au hatarini.

Kama wangekuwa wameji lockdown ni wazi kuwa wapendwa wetu wengi (wakiwamo hawa wa karibuni) waliotutangulia kuwa wangekuwa hai leo.

Kila mtu anaijua hali yake. Ninaijua hali yangu na kuwa bila ya kuchukua hatua za msingi, ni dhahiri kuwa, ndi mfu ninayetembea.

Hali hii inaniacha bila njia nyingine vinginevyo kukisabiria kifo.

Kwa hakika sina njia nyingine na sasa ni rasmi ninauchukua ule ushauri pendwa wa wale mazwazwa gwiji. Wala isiwe taabu hata kama nitashindia uji ninaji lockdown.

Kwa hali hii nitashangaa mno kama kuna mtu atatokea kunidai kodi labda kwa baba mwenye nyumba.

Ni heri nishindie uji nikiwa hai kuliko kufa nikijaribu kuishi maisha ya kawaida.

Ni heri nikafa nikipambana kujaribu kuishi, kuliko kukisabiria kifo kilichokuwa dhahiri kama hiki.

Si uamuzi rahisi ninaouchukua bali ni kwa sababu sina namna nyingine.

Tutapeana mrejesho.
 
Niombee basi mkuu mimi kesho niko safarini na hizi ndege zetu za ardhini nikipasua anga kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine! Ila nitavaa barakoa bila shaka yoyote ile. Maana hali si hali.

Hapa penyewe nilipo tu, hofu kibao!! Ufupi tu siumwi! Ila nina hofu mwili mzima!! ☹️ Yaani hii Corona ni nyoko kweli kweli.
 
Mabibi na mabwana sera ya Corona ya serikali ya awamu hii iko wazi. Yaani ni kila mtu na lwake.

Kwani pana hata haja ya kujidanganya tena? Kila mtu anajijua yupo katika kundi lipi katika mawili tu yaliyopo. Yaani kundi salama au hatarini....

Lk 12:20 SUV​

Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?

Inawezekana una sh mia mbili tatu za kubadilisha mboga hivyo unaona utakuwa safer ukikaa ndani.

Kuna siku nikajisemea wacha nisitoke out nikae ndani kuepuka majanga yanayoweza kunikuta bara barani.
Basi nikawa nimekaa kwenye meza nabrowse huku nimezima taa. Mara nikasikia kitu 'kizito' kinanigonga kwenye mguu, nikapanda juu ya kiti nikawasha taa.

Kucheki hivi nikakuta ni nyoka mkubwa amenigusa (ila hakuniuma). Nikamuua na kumtupa nje. Unaona! Nilikuwa naogopa kutoka out ili 'kuepuka kifo' kumbe kifo nilikuwa nimejifungia nacho ndani.

Live your life, siku yako ikifika hata wewe utafurahia kuondoka kwenye huu ulimwengu uliojaa kila aina ya dhiki!
 
Lk 12:20 SUV​

Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?

Inawezekana una sh mia mbili tatu za kubadilisha mboga hivyo unaona utakuwa safer ukikaa ndani.

Kuna siku nikajisemea wacha nisitoke out nikae ndani kuepuka majanga yanayoweza kunikuta bara barani.
Basi nikawa nimekaa kwenye meza nabrowse huku nimezima taa. Mara nikasikia kitu 'kizito' kinanigonga kwenye mguu, nikapanda juu ya kiti nikawasha taa. Kucheki hivi nikakuta ni nyoka mkubwa amenigusa (ila hakuniuma). Nikamuua na kumtupa nje. Unaona! Nilikuwa naogopa kutoka out ili 'kuepuka kifo' kumbe kifo nilikuwa nimejifungia nacho ndani...
Live your life, siku yako ikifika hata wewe utafurahia kuondoka kwenye huu ulimwengu uliojaa kila aina ya dhiki!

Kwamba ninaijua hali yangu iko hatarini kiasi gani? Kwamba ninatambua ni mfu ninayetembea? Kwamba ni tayari kushindia uji? Kwamba ni heri nife nikipambana ili niwewe kuishi? Kwamba wa kodi sina cha kumlipa? .... Kwamba...? .. kwamba... ? Na kwamba nyingi tu?

Askofu Rashid, uko out of touch, out of context and out of point! Nukuu yako haina inapoakisi lolote la kuhusiana na mada hii zaidi ya kuonyesha ulivyokuwa mburula!

Nasikitika kukutaarifu nukuu na maelezo yako marefu yako yasiyohusiana kabisa na mada iliyopo, ni utopolo mtupu yenye kuakisi wazi wazi haswa wale manabii wa uongo wa siku za mwisho!

Ndiyo maana mnatoa vyeti fake vya kufuzu kuondosha magonjwa kwa maombi.

Unajisemea tu kwa sababu wewe uko kwenye kundi salama? Nyie si ndiyo hawa anaowasema Prof. Bisanda?

"Watanzania wengi wanadhani ugonjwa huu utawapata wengine, wasitambue kuwa hata pale wanapopata maambukizi, huwa wamekuwa wazembe kujilinda."

Kwa mawazo yako unadhani ninafurahi kufikia uamuzi huu niliofikia?

Au wewe ni hawa?

IMG_20210218_174254_207.jpg

Ambao wao kuelewa lolote ni heri ya mbwa mzee kujifunza jina jipya?

Disgusting.
 
Yaani we jamaa unaangaika utadhani umepakwa pilipili kwenye makalio
 
Niombee basi mkuu mimi kesho niko safarini na hizi ndege zetu za ardhini nikipasua anga kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine! Ila nitavaa barakoa bila shaka yoyote ile. Maana hali si hali.

Hapa penyewe nilipo tu, hofu kibao!! Ufupi tu siumwi! Ila nina hofu mwili mzima!! ☹️ Yaani hii Corona ni nyoko kweli kweli.

Mkuu ni mazwazwa peke yao kama hawa:

IMG_20210218_174325_816.jpg

wasioweza kuona hatari iliyoko mbele yao. Wanaweza hata kuthubutu kuja na nukuu tokea katika misahafu.

Wakisahau kuwa misahafu hiyo hiyo imeandikwa "usimjaribu bwana Mungu wako, achilia mbali kulitaja jina la bwana Mungu wako bure."

Kwenye mkusanyiko kama huo wa kwa hakika kwa sasa barakoa ni babalao.
 
Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali.

Ila ni wachache sana wanakuja na ushauri au solution kutokana na wingi wa vifo hivyo.

Inajulikana Corona ipo nchi nyingi, imeua na inaendelea kuua watu duniani kote.

Hivyo kama watanzania wenye akili timamu bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa, kidini, kikabila n.k ni vizuri tukawekeza nguvu kubwa katika kutoa mawazo ya kujenga kuhusu namna ya kupambana na huu ugonjwa.

Hivyo kwa yeyote mwenye mawazo mazuri ya namna ya kupambana na huu ugonjwa ni vizuri akashauri vyema sababu Corona haichagui mtu wa kumuondoa, pia ugonjwa wa Corona haujaletwa na serikali au Raisi Magufuli hivyo matusi, kejeli, dharau na vitu vya namna hiyo kwa serikali sio sawa.
 
Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali.

Ila ni wachache sana wanakuja na ushauri au solution kutokana na wingi wa vifo hivyo.

Inajulikana Corona ipo nchi nyingi, imeua na inaendelea kuua watu duniani kote.

Hivyo kama watanzania wenye akili timamu bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa, kidini, kikabila n.k ni vizuri tukawekeza nguvu kubwa katika kutoa mawazo ya kujenga kuhusu namna ya kupambana na huu ugonjwa.

Hivyo kwa yeyote mwenye mawazo mazuri ya namna ya kupambana na huu ugonjwa ni vizuri akashauri vyema sababu Corona haichagui mtu wa kumuondoa, pia ugonjwa wa Corona haujaletwa na serikali au Raisi Magufuli hivyo matusi, kejeli, dharau na vitu vya namna kwa serikali sio sawa.
Sasa wewe umetoa mchango gani wa jinsi ya kupambana na corona? Au umekuja kuandika bla bla tu na kuondoka ?
 
Back
Top Bottom