Kufungwa shule sio sawa na lockdown! Mimi sihitaji lockdown,ni mvuja jasho tu,siwezi kumudu ugumu wa maisha kwa kujifungia ndani.
Nilichomaanisha kama walimu waugua,huoni watoto wetu wapo hatarini pia?
Mimi wa kwangu wapo private,nimelipa mahitaji yao yote kisha nimekwenda kuwaomba walimu ruhusa kwamba tuna matatizo kijijini,hivyo watoto hawatahudhuria masomo kwa mwezi mmoja.
Watakaa ndani,mimi nitatoka kuwatafutia mkate,huko nitachukua tahadhari zote ili nisiubebe ugonjwa huko kwenye mihangaiko kuupeleka nyumbani.