Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Last year nilikuw na best wangu kutoka Latvia huko aliniambia

"If you want to success as nation you should control your population first"
 
Hiv ww unaongea hayo ukiwa umelala au umesimama au ndio huna uzazi? Zaaa tu
 
Acha watu wazaane, hizo habar za kutotosha madarasa ni uzembe wa serkal kufuja kodi kwa mambo ya hovyo wakat kuna mambo ya msingi ya kufanya, ujui kuwa idadi ya watu inachangia maendeleo? , ujui kuwa idadi kubwa ya watu inachangia kutanuka kwa miji, vijiji na majiji? , mimi husema sana hata idadi ya watu TZ ni zaid ya milion60, huwenda hata tuko mil70-80 kwamaana kuna jamii hazikuhesabiwa kipind cha sensa, na wapo pia waliokwepa kubesabiwa kwa makusud, pia wapo waliotoa data za uongo ktk ujazwaji wa idad ktk familia kipind cha kuzipata izo data, pia wapo watahalam walio foji data, na pia zipo jamii ambazo zinaish maeneo hatar ambayo kwa wale wenzetu walokulia mjini si rahis kufika, mfano ktk jamii za wahdzabe/watindiga waishio maporin, si rahis kujua idad yao kamil, hivyo hayo yote yanatosha kusema kuwa, idadi ya watz ni zaid ya milion70-80, mpka kufika 2025 tutakuwa zaid ya mili100,.....KUZAA KUENDELEE[emoji41][emoji41]
 
Kwa kweli hali ni mbaya sana.
Umetoa wazo zuri.
Kama hutaki kuzaa ni wewe. Wengine tunaona serikali iweke ukomo uwe watoto 6 kwa mke mmoja. Mwanaume akiwa na wake zaidi ya mmoja aendelee mpaka atakaposhindwa mwenyewe.
 
Jinga kabisa

Idadi ya watu ni sehemu mojawapo iliyo kubwa kuliko zote za kukuua kiuchumi
 
Kila mtu azae anavyoweza. Nchi bado ina mapori mengi
 
Utajiri gani wa watu ambao ni masikini? Hata mstaafu Jk Kikwete mwaka 2012 kipindi anapokea riport ya sensa ya watu na makazi alionya ongezeko kubwa la watu wakati uchumi ni mbovu.
Tukuze kwanza uchumi badae ndo tuzaliane.
JPM rais mpendwa dunia nzima aliposema watu wafyatue hasa wa kanda ya ziwa alikuwa anawaongopea?
 
Tatizo mleta mada hakusoma shule nzuri, kuna swali lilirindima kwenye past papers miaka kibao huko nyuma liliuliza hivi! ili tuendelee tunahitaji mambo/vitu vinne navyo ni............ cha kwanza kabisa ni (1)watu, (2) ardhi..........sasa eti leo tupunguze mweee!
 
Utajiri gani wa watu ambao ni masikini? Hata mstaafu Jk Kikwete mwaka 2012 kipindi anapokea riport ya sensa ya watu na makazi alionya ongezeko kubwa la watu wakati uchumi ni mbovu.
Tukuze kwanza uchumi badae ndo tuzaliane.
kikwete hajui kila kitu!! kwani yeye nani? ndo maana alikwambia hivi akili za kuambiwa changanya na zako, kama hujakuza uchumi miaka zaidi ya 50,ya uhuru, kubali tu kuwa wewe ni failure mbaya, wacha ije damu mpya!

kasome upya mzee!! hizo sheria zako kandamizi hatutaki kawambie hao wakoloni wako tumekataa! kwani wewe au wao ndo unabeba hizo mimba? wabebaji hawajalalamika wewe nani ulalamike? au siyo riziki?

km umeshindwa kumtotolesha Mama Koku ulie tu! Usituletee kikwapa hapa ! na usirudie tena huu upupu! unanisikia? ukithubutu kufanya hivi usije nilaumu!! sisi ni waafrica wayahudi original, Tuliagizwa na Mungu wetu kuzaa!

Na kizazi cha Babu yetu kitakuwa km Nyota wa mbinguni, au mchanga wa Bahari km unaweza kuuhesabu kahesabu alafu ndo uje utupe huu ujinga wako! usikubali kutumika hovyo! na hao wazungu, wao hawezi kufanyana km sisi!! kwanza hawana genye! kabisaa!

sasa km mtu huna genyege utazaa nini paka au, kuzaa kwao mwisho miaka 30, sisi hapo ndo kumekucha!
 
Anayeweza kufyatua afyatue asiyeweza atulie mambo yatajibalansi yenyewe.
 
Last year nilikuw na best wangu kutoka Latvia huko aliniambia

"If you want to success as nation you should control your population first"
Unaamini kila kitu na kila mtu? IQ yako itakuwa chini sana,
 
Mapori ya kuishi bado yapo mengi kwelikweli. Tatizo tunapenda kukusanyika sehemu moja.
 
Tatizo watoto wanaozaliwa hawapati basic needs .Wengi wametelekezwa ndo shida yangu iko hapo.Swala la mapoli sio ishu .
Hahahahahah "babe la wachovu"

Mada yako ya Mungu mfalme sijui nini nini Umeikimbiaaa, vipi ulitumwa kupima upepo Kama DnoJ?
 
Marehemu hasn pope kweli ni mwanaume watoto 7 umri miaka 64 ma mdogo ni miakav2..
Sisi wa leo tunataka utajiri tu tunaogopa kuwazalisha hawa viumbe.
Hebu tuwaonee huruma tuwazalishe tu hata mtoto mmoja mmoja wasiteseke mwanzo wa uzee wao.
 
 
Naunga mkono hoja, na hii sheria ipelekwe bungeni haraka kwa hati ya dharura.
 
Kuna watoto wa jirani wanazunguka kuomba omba barabarani na wengine wamegeuka vibaka wanatukaba mitaani.
 
Yaani kweli kabisa, utitiri wa kuzaana tu,na kulazimisha serikali kuongeza mzigo wa kuhudumia midomo mingi, wakati nchi ni maskini na wazalishaji wa chakula ni wachache na miundombinu yote ya maji,afya,mawasiliano,elimu, makazi nk kila leo inazidi kuelemewa na hakuna anayejali! Yaani population ya sensa iliyopita tu serikali imeelemewa kuweza kujaribu kuihudumia sasa na huu utitiri uliongezeka bila mpango sijui itakuwaje??... yaani kuokoa gharama za sensa inayokuja wange' extrapolate' tu namba iliyopita na angalau hiyo pesa itakayookolewa kuelekezwa kuongeza matundu ya vyoo vya shule vijijini..... Kaazi iendelee.
Kwa kweli hali ni mbaya sana.
Umetoa wazo zuri.
 
Nchi hii ni kubwa sana. Mfano kutoka Chalinze mpaka Morogoro ni mapori na misitu yenye utajiri mkubwa. Kwa maoni yangu tuendelee kuzaana ili tuwe na uhakika wa soko la ndani. Uwingi sio tatizo tatizo ni fikra na juhudi.
Uhakika wa soko hautokani na kuzaliana bali kipato cha wato, hata mkizaliana kama kumbikumbi kama ni mafukara hakuna chochote cha maana kitafanyika zaidi ya uharibifu wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…