Serikali iwe Makini Kabla TLS Haijajigeuza Kuwa ‘Chama cha Siasa kali’

Serikali iwe Makini Kabla TLS Haijajigeuza Kuwa ‘Chama cha Siasa kali’

TLS ni chama cha kitaaluma bado hata hayo matamko unayoona wewe yanavuruga amani kama unavyodai yako kisheria.

Mfano ni kuwa waziri kafuta vijiji vya Ngorongoro kwa matakwa yake haijulikani mamlaka hayo kayatoa wapi kikatiba, alipokuja rais wa TLS katengua maamuzi hayo kwa kunukuu vifungu vya sheria na kuonyesha wazi ni waziri ndio kavunja sheria na sio wamasai kuwepo kwenye eneo lao asili.

Hiki ulichoandika hapa hakuna kifungu chochote ulichofanya rejea kuonyesha TLS imegeuka chama cha siasa.


Ni vyema mada zingine usizipandishe hapa japo unapata ujira wako kwa taabu ila mada zingine ukubali zinakuzidi kimo.
IMG-20240628-WA0014.jpg
 
Unafikiri bungeni ni uwanja wa mazoezi kwamba kila mtu anaingia tu kufanya mazoezi? Nani mwenye akili Timamu anayeweza kumpigia kura ya ndio mwabukusi?
Kweni hilo Bunge ni la Baba yako?! Mwabukusi akishinda Uchaguzi anaingia kwenye Bunge letu la Wananchi.
 
Mwabukusi akiingia Bungeni nitaanza "rasmi" kuangalia Bunge Live.

Bunge limeharibiwa na hawa "Wabunge wapiga Meza" tunataka Bunge MOTO MOTO😁😂
 
Kweni hilo Bunge ni la Baba yako?! Mwabukusi akishinda Uchaguzi anaingia kwenye Bunge letu la Wananchi.
Ashinde kwa kura za nani na kutokea jimbo lipi? Unajuwa kuwa amewahi kutaka ubunge na akatupwa mtaroni kama jongoo? Au wewe ndio umemjuwa leo?
 
Bungeni wanaingia wenye akili Timamu na wanaojitambua vizuri.siyo kila mtu anaingia Bungeni kama sokoni.
Mumejaza "Mazezeta" Bungeni ambao wengi wameingia kwa AMRI ya MAGUFULI sisi WANANCHI safari hii tunaingiza Wabunge "Machachari" wenye UCHUNGU na NCHI hii TANZANIA.😀✊️✊️
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna hatari ninayoiona ikija kupitia chama cha wanasheria Wa Tanganyika yaani TLS.Naona ni kama kinataka kutolewa kutoka kuwa chama cha kitaaluma na kujigeuza kuwa chama cha siasa kali na kinachoweza kuivuruga serikali na hata kuleta Masuala yatakayochochea vurugu,chuki,uhasama na ubaguzi miongoni Mwetu kwa kupandikiza maneno ya uongo na uzushi.

Naona chama hiki kikigeuzwa kuwa pango la wanaharakati wenye nia ovu na kuvuruga amani ya Nchi yetu. naona kuna hatari chama hiki kikaanza kuwa uchochoro wa kupitishia maburungutu ya pesa chafu kwa ajili ya kufadhili na kuwafadhili watu ambao watatumika kuvurugu amani na utulivu wa Taifa Letu. Naona chama hiki kinataka kutumika kama kichaka cha kutolea matamko ya hovyo kwa mwamvuli wa TLS.

Ni Muhimu serikali ianze kutupia jicho lake la kijasusi na kiupelelezi kuangalia muenendo mzima wa shuguli za chama hiki ,kama zinafuata taratibu au ni mtu tu au kikundi cha watu na wafadhili wao nyuma ya pazia wanataka kukitumia chama hiki kwa maslahi yao binafsi kuvuruga amani ya Taifa letu

Nasema haya kwasababu nimeona chama hiki kinakoelekea siyo kuzuri kwa mstakabali mzima wa Aman na usalama wa Taifa letu. naona ni kama kinataka kitumiwe na wanaharakati uchwara na wenye ajenda ovu kwa kutumiwa na watu wenye mapesa yao kusukuma au kupenyeza ajenda zao kwa lengo ya kuivuruga serikali yetu na kuihamisha kiajenda pamoja na kuhatarisha usalama wa Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Pumbaf kweli ww na bado
 
Mumejaza "Mazezeta" Bungeni ambao wengi wameingia kwa AMRI ya MAGUFULI sisi WANANCHI safari hii tunaingiza Wabunge "Machachari" wenye UCHUNGU na NCHI hii TANZANIA.😀✊️✊️
Mwabukusi hawezi kuingia Bungeni hata kwa kusukumwa tu.ndio maana alipojaribu jambo hilo alifyekwa vibaya sana na kubaki na aibu kuu.
 
Mwabukusi lazima aingie MJENGONI DAADEKI....😄 HII NI NCHI YETU SOTE✊️
 
TLS ni chama Cha kitaaluma ila limesha poteza lengo,kimekuwa kisiasa zaidi
Kimepoteza kabisa dira yake na kutaka kujigeuza kuwa chama cha siasa.kwa hiyo ni bora ieleweke Kuwa ni chama cha siasa badala ya kukitumia kwa malengo ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom