Serikali iwe Makini Kabla TLS Haijajigeuza Kuwa ‘Chama cha Siasa kali’

Serikali iwe Makini Kabla TLS Haijajigeuza Kuwa ‘Chama cha Siasa kali’

Usitumie hisia kwenye mambo ya kitaaluma,ingelikuwa vema kama hoja yako ingelijengwa kwenye uvunjifu wa katiba ya nchi na katiba ya Chama cha wanasheria Tanganyika TLS kama zimevunjwa na kwa namna gani.
 
Mimi huwa natumia akili na siyo hisia katika kuzungumzia jambo lolote lile
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna hatari ninayoiona ikija kupitia chama cha wanasheria Wa Tanganyika yaani TLS.Naona ni kama kinataka kutolewa kutoka kuwa chama cha kitaaluma na kujigeuza kuwa chama cha siasa kali na kinachoweza kuivuruga serikali na hata kuleta Masuala yatakayochochea vurugu,chuki,uhasama na ubaguzi miongoni Mwetu kwa kupandikiza maneno ya uongo na uzushi.

Naona chama hiki kikigeuzwa kuwa pango la wanaharakati wenye nia ovu na kuvuruga amani ya Nchi yetu. naona kuna hatari chama hiki kikaanza kuwa uchochoro wa kupitishia maburungutu ya pesa chafu kwa ajili ya kufadhili na kuwafadhili watu ambao watatumika kuvurugu amani na utulivu wa Taifa Letu. Naona chama hiki kinataka kutumika kama kichaka cha kutolea matamko ya hovyo kwa mwamvuli wa TLS.

Ni Muhimu serikali ianze kutupia jicho lake la kijasusi na kiupelelezi kuangalia muenendo mzima wa shuguli za chama hiki ,kama zinafuata taratibu au ni mtu tu au kikundi cha watu na wafadhili wao nyuma ya pazia wanataka kukitumia chama hiki kwa maslahi yao binafsi kuvuruga amani ya Taifa letu

Nasema haya kwasababu nimeona chama hiki kinakoelekea siyo kuzuri kwa mstakabali mzima wa Aman na usalama wa Taifa letu. naona ni kama kinataka kitumiwe na wanaharakati uchwara na wenye ajenda ovu kwa kutumiwa na watu wenye mapesa yao kusukuma au kupenyeza ajenda zao kwa lengo ya kuivuruga serikali yetu na kuihamisha kiajenda pamoja na kuhatarisha usalama wa Taifa letu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Aiseeeee......
 
Yaani wadau sijawahi kuelewa akili ya mwashambya ata kama ni njaa au uchawi hawa ndo maadui wa nne wa TAIFA ukiachana na wale watatu
 
Pia Serikali iwe makini kabla Chama tawala haijamaliza fedha za umma kwa kampeni yake ya uchaguzi 2024 na 2025 kama ilivyokuwa 2019 na 2020.
 
Yaani wadau sijawahi kuelewa akili ya mwashambya ata kama ni njaa au uchawi hawa ndo maadui wa nne wa TAIFA ukiachana na wale watatu
Uwepo wa Mwashambwa, kwa kweli ihesabike ni laana kwa familia yake, na laana kwa jamii inayomzunguka. Ukiwa na mtu wa namna hii kwenye familia utabaki unajiuliza ulikosea wapi mpaka kuwa na mwanagfamilia wa hivi!!
 
ed7444724e8f9923e5bf480fc2791886.jpg
 
Pia Serikali iwe makini kabla Chama tawala haijamaliza fedha za umma kwa kampeni yake ya uchaguzi 2024 na 2025 kama ilivyokuwa 2019 na 2020.
CCM Ina pesa za kutosha na vitega uchumi kila kona ya Taifa letu.ndio maana haiteteleki sala kusuasua katika jambo lolote lile
 
Back
Top Bottom