Serikali kuendelea na uwekezaji wa Bandari na DP World kama ilivyopangwa

Kwa hiyo mnapiga makelele ili mradi ukwame? Sasa wanakuja kuwekeza na kwa kuwa faida ni kwa nchi nzima, endeleeni tu kupiga kelele
 
Maamuzi ya mwananchi wa kawaida ni ile siku ya kupiga kura! Pale ndio chanzo cha yote tunayoyaona
 
Tunalipia upumbavu uliosainiwa na marais wajinga waliotangulia,

Ndio maana nikasema akija Rais mwingine mwenye akili atakuwa tayari kulipa mabilioni ili kuondokana na upumbavu wa namna hii!
Huo upumbavu ukija kulipa na bandari ikaongeza mapato mengi zaidi ya haya ya sasa, huwa hatukumbuki haya yote tunayoyaandika. Hatukumbuki hizi laana zote tunazoziongea kupitia midomo yetu.
 
Mapato yapi?

Yani mwarabu aje akuongezee wewe mapato?
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
TRA itakusanya mapato kama inavyofanya lakini kwa kasi zaidi kwani mzunguko wa ushushaji na upakiaji wa makontena utakuwa ni wa viwango vya juu tofauti na huu wa sasa.

Wingi wa meli zinazoshughulikiwa unaongeza ufanisi wa kazi, ambao unaongeza mapato ya TRA.

Huyo mwarabu yupo dunia nzima Antwerp, London, Southampton na kwenye mataifa mengine, Kote huko kuna ufanisi mkubwa na ndio maana wao ni mataifa ya dunia ya kwanza wakati sisi wabishi na wajuaji tupo katika dunia ya tatu.
 
Watu wote hatujaona hayo unayoyasema isipokuwa wewe na Samia tu!?
 
Panua ubongo wako ili ujue kinachoendelea huko duniani. Mengi watanzania hatuyajui na tunaendelea kuzeeka na ujinga vichwani kwa sababu tu ya kutopenda kufikiria nje ya boksi.
Hayo yanayoendelea huko duniani hatujui isipokuwa wewe na Samia tu ndio maana mkagawa bandari?
 
Hayo yanayoendelea huko duniani hatujui isipokuwa wewe na Samia tu ndio maana mkagawa bandari?
Kutokujua haina maana hakuna kinachofanyika na kuendelea. Kwa taarifa yako Samia ni rais mjanja sana kuliko tunavyodhania.

Anao mpango wa kuligeuza jiji la Dar liwe ni HUB ya kibiashara, tafuta maana ya hub mitandaoni ili upanue uelewa wako.

Tatizo la kwako ndio lile lile la watanzania wengi, kudhani kuwa kile kidogo wanachokifahamu ndio kila kitu maishani.

Unaweza ukawa na PHD kichwani mwako lakini ukakosa ufahamu mpana wa dunia inavyokwenda. Unaweza ukawa ni wa form four tu huna shahada yoyote ile lakini upeo wako ukawa mkubwa sana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Unajaribu kushawishi nini?
 
Samia huyu huyu wa Kizimkazi ni mjanja? Anataka kugeuza Dar iwe Hub? Samia??
Kuna watu mna utani halafu hamjui wa kuwatania.
 
Samia huyu huyu wa Kizimkazi ni mjanja? Anataka kugeuza Dar iwe Hub? Samia??
Kuna watu mna utani halafu hamjui wa kuwatania.
Huyu huyu wa kizimkazi, anataka kuigeuza Dar iwe Hub akiwa na madaraka yote ya rais wa awamu ya sita wa JMT na sio mwanamama fulani wa kiunguja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…