Serikali kuendelea na uwekezaji wa Bandari na DP World kama ilivyopangwa

Serikali kuendelea na uwekezaji wa Bandari na DP World kama ilivyopangwa

Msijali watz!

Atakuja rais mwingine mwenye akili atatunasua kwenye hili tego hata kama tutalipa fidia ya mabilioni itakuwa bora zaidi kuliko kuendelea kuukumbatia huu uharo!
 
CASE CLOSED!
Tukalime watu wa roporopo Mtashindwa kilimo simple namna hii.
FB_IMG_1693154015844.jpg
 
Tumeongea na Papa tumejieleza kwa kilatini sijui kwa kiingilishi, tumeomba msamaha.

Tunataka bandari zetu.
 
Wanaukumbi.

Kila hatua na kadri majadiliano yatakavyokuwa yanaendelea ikiwemo kuafikiana au kukubaliana pande zote kati ya Serikali ya Tanzania na mwekezaji kwenye uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam , umma wa Watanzania tumehakikishiwa kuwa utajulishwa.

Hayo yamesemwa Agosti 26, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna mkataba wowote wa utekelezaji kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa bandari ambao umeshasainiwa.

Msigwa amesema, baada ya hatua ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai hatua itakayofuata ni mikataba ya utekelezaji.

Kuhusu mikataba hiyo ya utekelezaji, Msigwa amesema

"Baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kinachofuata sasa ni mikataba ya utekelezaji, katika mikataba hiyo ya utekelezaji ndio itasema sasa miradi itakuwa ni ya muda gani"

Msigwa ameendelea kwa kusema kuwa, hatua itakayofuata ni uandaaji wa nyaraka na katika hatua hii ndipo miradi ya utekelezaji itaandaliwa huku akiendelea kusisitiza kuwa hakuna bandari iliyouzwa.
 
Hawa waarabu nao ni matapeli, yaani unaendeleaje kuwekeza sehemu ambayo ina makele kibao kuhusu mradi wako bila woga wowote?

Yaani ni sawa na wewe kuendelea na mchakato kununua nyumba ya urithi ambayo tayari wanafamilia hawaelewani - itakuwa ni ujinga wa mwaka.
 
Hawa waarabu nao ni matapeli, yaani unaendeleaje kuwekeza sehemu ambayo ina makele kibao kuhusu mradi wako bila woga wowote?

Yaani ni sawa na wewe kuendelea na mchakato kununua nyumba ya urithi ambayo tayari wanafamilia hawaelewani - itakuwa ni ujinga kwa mwaka.
Hizo kelele ni zipi?
Au za wadandia hoja?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Watazingatia maoni gani wakati IGA imeshapitishwa na bunge bila kusikiliza maoni ya wadau?

Msigwa anaeopoka ujinga tu.
 
"Baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kinachofuata sasa ni mikataba ya utekelezaji, katika mikataba hiyo ya utekelezaji ndio itasema sasa miradi itakuwa ni ya muda gani"
Huyu mtu ni very stupid. Mikataba hiyo inakuwa governed na IGA, haiwezi kukiuka kipengele cha " mpaka shughuli zitakapoisha". Shughuli za bandari znaisha line? Nawashauri Dubai wasije maana hata jeshi litawageuka. hakuna atakayekubali kuuza bandari zetu...
 
"Baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kinachofuata sasa ni mikataba ya utekelezaji, katika mikataba hiyo ya utekelezaji ndio itasema sasa miradi itakuwa ni ya muda gani"
Mbona tunaambiwa Dubai si serikali mara ni nchi muda mwingine tunaambiwa si nchi ni kampuni ukweli ni upi
 
.....hakuna bandari iliyouzwa...

[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
Msigwa anaongea uongo, ile IGA inamruhusu mwarabu kuanza kazi tangu siku iliposainiwa, October 2022.

Kama mwarabu yupo huru kuanza kazi tangu wakati huo, maana yake anatembea na makubaliano ya kwenye IGA ambayo haijaweka ukomo wa utekelezaji wa shughuli za uwekezaji.

Hawa wajinga baada ya kuona wamekosa majibu kuhusu IGA, sasa wameona watupeleke kwenye HGA kuficha utupu wao, kwasababu wanajua hizo HGA watazificha tusizione.
 
Back
Top Bottom