Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema serikali ina mpango wa kugawa Vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa kwa walimu wote kwa lengo la kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Akijibu maswali ya Wabunge, leo Septemba 15, 2022 Jijini Dodoma Naibu Waziri Kipanga amesema kutokana na idadi ya vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa kuwa ndogo na haitoshi, wizara hiyo imeamua kuongeza vingine ili kutosheleza walimu wote nchini.

"Vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa ni zaidi ya laki mbili na elfu tano, lakini sisi kama wizara tumeongeza vishikwambi vingine zaidi ya laki moja, kwahiyo niwaondoe hofu kwamba idadi ya vishikwambi ambavyo wizara imeratibu na kununua vitatosheleza kwa walimu wetu wote," - Kipanga.
 
Hii ipo kisiasa zaidi, mwalimu anafundisha kwa chaki ubaoni huko Nanjilinji unampa kishkwambi cha nini? Kuangalizia muvi?

Labda kama wameona baada ya sensa hawana pa kuvipeleka wakaamua kuwapa walimu.

Ila kusema vitaboredha utoaji wa elimu nchini ni uongo.
 
Tanzania kubadilika ni ngumu sana tunajikwamisha wenyewe hsa watendaji wa serikali wanakwamisha mambo mengi sana mazuri.

Mimi ni shuhuda 2021 nilipeleka a very good ict project kwa tamisemi na wizara ya elimu kwaajili ya shule zetu hizi za umma na ilikuwa simple na inayoendana mazingira yetu.

Kilichotokea huko ni kusifiwa tu good project ooh hii itaeta mabadiliko sasa kwenye ushirikiano hupewi hata kupata kibali tu nilisota mwaka na sikupata the end vijana wa ict waliograduate kama 13 ambao ndio waliunda mfumo huo wa elimu walianza kutawanyika mmoja mmoja na ndio mchezo ukausha hivyoo.

Hii nchi ni ngumu sana kufanikiwa hasa km wewe ni mtu wa kunyoosha mambo.

Ni ngumu sana hii nchi.
 
Serikali ina mpango wa kugawa vishkwambi vilivyotumika katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mwezi Agosti, 2022 kwa walimu wote nchini kwa lengo la kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.”

-Naibu Waziri wa Elimu, Juma Kipanga alijibu swali Leo Bungeni..


Je vitafika Kweli Kwa Kila mwalimu? Au Ndio Kila shule kimoja na vingine vipotee kusikojulikana!
 
Sasa kishikwambi kitamsaidia nini mwalimu kuandaa masomo yake, ni bora hata wapewe laptop. Bongolala kuna watu wanakurupuka sana.
 
Kimoja ni bei gani? Tuzidishe kwa 305,000 ili tuone ni bil ngapi zinaenda kuliwa
 
Tunaposema serikali ya mama Ina Nia njema kwa watanzania wa Hali zote ndo hii Sasa, hongera sana serikali ya awamu ya sita, nasubiri kishikwambi changu kwa hamu. Niko huku Mpigamiti-liwale
 
Back
Top Bottom