Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

Hapo kabla ya kugawa watajichukulia vishkwambi mia kadhaa kifisadi. Wenzetu wanaportal za kuendesha minada ya serikali na watu wanabid kwa uwazi. Hivyo vishkwambi vingepigwa mnada raia wavinunue serikali irudishe chochote.
 
Hii ipo kisiasa zaidi, mwalimu anafundisha kwa chaki ubaoni huko Nanjilinji unampa kishkwambi cha nini? Kuangalizia muvi?

Labda kama wameona baada ya sensa hawana pa kuvipeleka wakaamua kuwapa walimu.

Ila kusema vitaboredha utoaji wa elimu nchini ni uongo.
Acha dharau wewe. Hujui kuwa siku hizi kuna online books na other teaching materials tena kuanzia level ya shule ya msingi. Si kila kitu lazima ucomment ndugu, kama huna taarifa pita kimya au uliza ufahamishwe.
 
Sasa kishikwambi kitamsaidia nini mwalimu kuandaa masomo yake, ni bora hata wapewe laptop. Bongolala kuna watu wanakurupuka sana.
mkuu, vitasaidia kama vitatumika vizuri na kama walimu wana uelewa wa ict.
shule zenye nafasi zinaweza kununua proojector chache na kutumika kwa masomo hasa ya sayansi. bila shaka vishkwambi vinaweza kuunganishwa na projector.
pia ni rahisi walimu kubadilishana notes na kuboresha ufundishaji.
zaidi, ni rahisi kuperuzi internet kupata maarifa zaidi.
kusema vishkwambi havitasaidia ni kwenda kinyume na maendeleo ya teknohama.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema serikali ina mpango wa kugawa Vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa kwa walimu wote kwa lengo la kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Akijibu maswali ya Wabunge, leo Septemba 15, 2022 Jijini Dodoma Naibu Waziri Kipanga amesema kutokana na idadi ya vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa kuwa ndogo na haitoshi, wizara hiyo imeamua kuongeza vingine ili kutosheleza walimu wote nchini.

"Vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa ni zaidi ya laki mbili na elfu tano, lakini sisi kama wizara tumeongeza vishikwambi vingine zaidi ya laki moja, kwahiyo niwaondoe hofu kwamba idadi ya vishikwambi ambavyo wizara imeratibu na kununua vitatosheleza kwa walimu wetu wote," - Kipanga.
Walimu wanaweza kutembelewa na panya road wakihtaji kishikwambi tu. Kazi ipo
 
Wakiongeza na vile alivyopokea waziri mkuu toka chima cjuwi wakijumlisha havitoshi?
 
Hii ipo kisiasa zaidi, mwalimu anafundisha kwa chaki ubaoni huko Nanjilinji unampa kishkwambi cha nini? Kuangalizia muvi?

Labda kama wameona baada ya sensa hawana pa kuvipeleka wakaamua kuwapa walimu.

Ila kusema vitaboredha utoaji wa elimu nchini ni uongo.
Acha ushamba, Walimu kibao tu wanatumia technology kufundishia. Mbona mna chuki sana kwa walimu?
 
Kimoja ni bei gani? Tuzidishe kwa 305,000 ili tuone ni bil ngapi zinaenda kuliwa

Huu ni ujinga mtupu tuu sasa vishikwambi vitamsaidia nini mwalimu? Zaidi vitawekwa bondi tuu! Kwanini wasingewapa pesa?Walimu wapewe kila mmoja hata posho ya laki tatu! Hivi vishikwambi Mwalimu wa Nanjilinji itamsidia nini kufindisha?
 
Tanzania kubadilika ni ngumu sana tunajikwamisha wenyewe hsa watendaji wa serikali wanakwamisha mambo mengi sana mazuri.

Mimi ni shuhuda 2021 nilipeleka a very good ict project kwa tamisemi na wizara ya elimu kwaajili ya shule zetu hizi za umma na ilikuwa simple na inayoendana mazingira yetu.

Kilichotokea huko ni kusifiwa tu good project ooh hii itaeta mabadiliko sasa kwenye ushirikiano hupewi hata kupata kibali tu nilisota mwaka na sikupata the end vijana wa ict waliograduate kama 13 ambao ndio waliunda mfumo huo wa elimu walianza kutawanyika mmoja mmoja na ndio mchezo ukausha hivyoo.

Hii nchi ni ngumu sana kufanikiwa hasa km wewe ni mtu wa kunyoosha mambo.

Ni ngumu sana hii nchi.
Just curious, what was the project about ? How did it work ?
 
Na bundle watatuwekea au wanatupatia tukaangalizie movie?
 
Back
Top Bottom