Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haitasaidia kitu! Tunahitaji madarasa, vitabu, madawati, maabara na walimu wa kutosha. Vishikwambi ni kupoteza tu fedha za umma!Mhe. Rais Samia Suluhu amekuwa akihimiza matumizi ya TEHAMA ili kuboresha huduma kwa jamii.
Kuonesha mfano, Serikali anayoiongoza itagawa vishkwambi zaidi ya 300,000 kwa walimu wote nchini ili kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.
Rais Samia Suluhu amedhamiria kuboresha elimu ya Tanzania
Rais Samia Suluhu ameamua kuifungua nchiIkitokea hivyo, basi maandalizi kwa ajili ya 2025 yatakuwa yameanza rasmi.
Vyote ivyo vipo mkuu na kama kuna sehemu havijafika utekelezaji unaendelea llakini upande wa elimu Rais Samia Suluhu amejitahidi sanaHaitasaidia kitu! Tunahitaji madarasa, vitabu, madawati, maabara na walimu wa kutosha. Vishikwambi ni kupoteza tu fedha za umma!
Hapana mkuu ni kwaajili ya masomo ya TEHEMA na sio matumizi binafsi maana Rais Samia analengo la kukuza somo la Tehama nchiniNyoosha maelezo vizuri, ni vishkwambi vya sensa wanapewa kwasababu havina kazi tena,
watatumia tu kama simu janja.
Kila kitu kinaenda na wakati wake Rais Samia Suluhu bado anaendelea kuboresha elimu wataanza na hivi na mwisho projector na computa zitanunuliwa tuHivyo vishkwambi vina RAM ya ukubwa gani?
Maana kama kweli ni gb 64, bado ni ndogo sana kwa kujaza material za ufundishaji na ujifunzaji.
Bora wangetoa computer na projector kwa kila shule.
Vishkwambi vyenyewe waliovitumia wanasema muda wowote vinajizima!
Walimu waongezewe mshahara, wapewe teaching allowance.
+rent allowance. Hizo ipad wapewe polisi
Vimetolewa ili kufundishia somo la TEHAMAHii ipo kisiasa zaidi, mwalimu anafundisha kwa chaki ubaoni huko Nanjilinji unampa kishkwambi cha nini? Kuangalizia muvi?
Labda kama wameona baada ya sensa hawana pa kuvipeleka wakaamua kuwapa walimu.
Ila kusema vitaboredha utoaji wa elimu nchini ni uongo.
Vishkwambi vya sensa full stop.Hapana mkuu ni kwaajili ya masomo ya TEHEMA na sio matumizi binafsi maana Rais Samia analengo la kukuza somo la Tehama nchini
aiseeHivyo vishkwambi vina RAM ya ukubwa gani?
Maana kama kweli ni gb 64, bado ni ndogo sana
Tatizo la afrika wanasiasa wanafanya maamuzi bila basis za maana za hayo maamuzi na wataalamu wanabaki kutekeleza tu hata kama wanajua ukweli hiilo jambo lita-fail wanakaa kimya maana wakijifanya kusema ukweli kupinga maamuzi ya wakubwa (politicians) wanaweza kutumbuliwa.Mkuu mimi sijadharau mtu hapa.
Wangefanya pilot study kwanza kwa shule chache hasa vijijini huko, waone kama hivyo vishikwambi ni feasible kwenye kutolea elimu.
Kitendo cha kuchkua mzigo wa tablets na kuzigawa bila kufanya utafiti wa ufanisi wake ni risk kubwa, inaeza kuleta hasara tu.
Hizo tablets zinafaa zaidi kwenye higher learning institutions kufanyia survey na data collection, ila kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi tutadanganyana.
Shule nyingi ziko huko vijijini (usiangalia shule za mjini tu) huko bush umeme shida na network hamna. Hizo tablets wanazitumiaje? Fanyeni pilot study muone feasibility ya huo mradi wenu
Siyo kwamba watu hawataki walimu wapewe hivyo vishikwambi tatizo ni impact yake katika ELIMU yetu kwa kuzingatia mazingira na hali halisi za shule zetu hasa maeneo ya vijijini lakini pia usimamizi wa matumizi sahihi ya hivyo vifaa.Siamini Kuna watu wanaumia walimu kupewa Vishikwambi .
Hakika Kuna watu Wana wivu bila sababu..
Acha wivu mkuu impact gani unaitaka boss?Kwanini wasivipeleke kwenye shule chache Ili wavifanyie pilot project ya mambo ya ICT badala ya kuvigawa hivyo mwisho wa siku hakuna impacts yeyote.
Well Said !!Tanzania kubadilika ni ngumu sana tunajikwamisha wenyewe hsa watendaji wa serikali wanakwamisha mambo mengi sana mazuri.
Mimi ni shuhuda 2021 nilipeleka a very good ict project kwa tamisemi na wizara ya elimu kwaajili ya shule zetu hizi za umma na ilikuwa simple na inayoendana mazingira yetu.
Kilichotokea huko ni kusifiwa tu good project ooh hii itaeta mabadiliko sasa kwenye ushirikiano hupewi hata kupata kibali tu nilisota mwaka na sikupata the end vijana wa ict waliograduate kama 13 ambao ndio waliunda mfumo huo wa elimu walianza kutawanyika mmoja mmoja na ndio mchezo ukausha hivyoo.
Hii nchi ni ngumu sana kufanikiwa hasa km wewe ni mtu wa kunyoosha mambo.
Ni ngumu sana hii nchi.