Serikali kugawa vishikwambi kwa walimu Nchini

Ikitokea hivyo, basi maandalizi kwa ajili ya 2025 yatakuwa yameanza rasmi.
 
Hivyo vishkwambi vina RAM ya ukubwa gani?
Maana kama kweli ni gb 64, bado ni ndogo sana kwa kujaza material za ufundishaji na ujifunzaji.
Bora wangetoa computer na projector kwa kila shule.

Vishkwambi vyenyewe waliovitumia wanasema muda wowote vinajizima!

Walimu waongezewe mshahara, wapewe teaching allowance.
+rent allowance. Hizo ipad wapewe polisi
 
Nyoosha maelezo vizuri, ni vishkwambi vya sensa wanapewa kwasababu havina kazi tena,
watatumia tu kama simu janja.
 
Haitasaidia kitu! Tunahitaji madarasa, vitabu, madawati, maabara na walimu wa kutosha. Vishikwambi ni kupoteza tu fedha za umma!
 
Haitasaidia kitu! Tunahitaji madarasa, vitabu, madawati, maabara na walimu wa kutosha. Vishikwambi ni kupoteza tu fedha za umma!
Vyote ivyo vipo mkuu na kama kuna sehemu havijafika utekelezaji unaendelea llakini upande wa elimu Rais Samia Suluhu amejitahidi sana
 
Nyoosha maelezo vizuri, ni vishkwambi vya sensa wanapewa kwasababu havina kazi tena,
watatumia tu kama simu janja.
Hapana mkuu ni kwaajili ya masomo ya TEHEMA na sio matumizi binafsi maana Rais Samia analengo la kukuza somo la Tehama nchini
 
Kila kitu kinaenda na wakati wake Rais Samia Suluhu bado anaendelea kuboresha elimu wataanza na hivi na mwisho projector na computa zitanunuliwa tu
 
Vimetolewa ili kufundishia somo la TEHAMA
 
Siamini Kuna watu wanaumia walimu kupewa Vishikwambi .

Hakika Kuna watu Wana wivu bila sababu..
 
Tatizo la afrika wanasiasa wanafanya maamuzi bila basis za maana za hayo maamuzi na wataalamu wanabaki kutekeleza tu hata kama wanajua ukweli hiilo jambo lita-fail wanakaa kimya maana wakijifanya kusema ukweli kupinga maamuzi ya wakubwa (politicians) wanaweza kutumbuliwa.

Ina maana wakati hivyo vishikwambi vinanunuliwa hawakuwa na plan B ya matumizi ya hivyo vishikwambi baada ya sensa?

Nia ya serikali ya kuwapa walimu hivyo vishikwambi ni nzuri ila tusitarajie mabadiliko ya ELIMU katika shule zetu za msingi na sekondari yaletwe na hivyo vishikwambi. Changamoto za matumizi ya hizi technolojia katika shule zetu ni nyingi sana na sioni plan ya hvi karibuni ya kuziaddress hizo changamoto.

Remember: IF YOU FAIL TO PLAN YOU ARE. PLANNING TO FAIL. Hili suala naona ni mihemiuko ya kisiasa tu.
 
Siamini Kuna watu wanaumia walimu kupewa Vishikwambi .

Hakika Kuna watu Wana wivu bila sababu..
Siyo kwamba watu hawataki walimu wapewe hivyo vishikwambi tatizo ni impact yake katika ELIMU yetu kwa kuzingatia mazingira na hali halisi za shule zetu hasa maeneo ya vijijini lakini pia usimamizi wa matumizi sahihi ya hivyo vifaa.
 
Ni wazo kwema kabisa, naunga mkono hoja hii ila hili halinifanyi kupinga kabisa wanaokataa suala hili.
 
Well Said !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…