Serikali Kugharamia Mashabiki 55 Kwenda Kutoa Hamasa Africa Kusini

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika juhudi za hamasa kuendelea kuunga mkono michezo nchini hususani katika mashindano ya kimataifa, imeamua kugharamia jumla ya mashabiki 55 watakaosafiri kuelekea nchini Afrika Kusini, kwenda kuishangilia klabu ya Yanga katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, utakaopigwa tarehe 17 Mei, 2023 kwenye uwanja wa Royal Bafokeng uliopo katika mji wa Rustenburg nchini humo.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Said Yakubu alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari leo tarehe 13 Mei 2023, katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa msafara huo wa hamasa utaongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma.

"katika hii safari, Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka kesho jumapili tarehe 14 Mei, 2023 kueleka Afrika Kusini na huko wataungana na Watanzania waishio Afrika Kusini katika kuhakikisha wanatoa hamasa ya kutosha,na nimeongea na Balozi, wao pia wamejiandaa kuwapokea lakini pia wameandaa mabasi kutoka kila mji kuhakikisha Watanzania wanakuwa wengi katika mchezo huo,"amesema Yakubu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Andrew Ntime amesema kuwa wao kama timu wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo huku akiishukuru serikali kutokana na mchango wake wa kupeleka mashabiki hao.

 
Ni jambo zuri na ni aina fulani ya kutangaza ligi yetu lkn kubwa zaidi nafikiri Serikali inge ongeza juhudi ya kuimarisha miundo mbinu ya mpira kwa ujumla na hasa kwa yale ya upande wao serikalini

Viwanja viboreshwe kuanzia kwenye ‘pitch’ majengo yake, vyoo , usalama

Utachezaje kwa utulivu li kiwanja lina ma bonde bonde na usalama hafifu wa kila aina

Kama kuna vitu vinatoka nje ya nchi na vinavyohusiana na kuboresha viwanja na miundo mbinu yetu wanaweza hata kuvifanyia ‘exemption’ ya mambo ya kodi na tozo mbalimbali

Tunajitahidi ukilinganisha na majirani zetu lkn tunatakiwa kuboresha zaidi na yanayohusu serikali iyafanyie kazi ili hapa Tanzania iwe ndo ‘Hub’ yetu ya soka kwa ukanda huu wa Afrika ya kati,mashariki na kusini
 
Huu ni upumbavu wa 100%.
Mantiki ya hiyo safari haipo kabisa na hizo ni pesa za Umma zinakwenda kuchezewa.

Kama watu hamjui tu, nyinyi fahamuni haya.

-Hao 'mashabiki' 55 wa Yanga ni maafisa waandamizi wa serikali, safari hiyo watagharamiwa Usafiri wa kwenda na kurudi (nadhani watakwea pipa) , Posho ya chakula na malazi nk. Wastani wa kumgharamia 'mshabiki' mmoja huenda hautapungua milioni 3, na kwa mashabiki 55 hapo ni zaidi ya milioni 165.

-Wizara haikuwahi kuwa na bajeti ya pesa iliyotengwa kwa hiyo safari, hivyo hiyo ni pesa inachotwa kutoka eneo lingine lililotengewa bajeti, mwisho wa siku malengo ya kibajeti hayatafikiwa.

-Mashabiki 55 wa Yanga hawawezi kuwa ya impact yoyote ya kishabiki katika uwanja wa Marumo unaotegemewa kuingiza zaidi ya mashabiki elfu 40.


NINI KINGEPASWA KUFANYIKA.
1. Wizara ingemobilize watanzania waliopo South Africa kuhakikisha walau wanafikia elfu Tano kuwepo uwanjani. (Hao wapewe nauli/usafiri wa kuja na kuondoka uwanjano, Jezi za Yanga/Taifa, Bendera za Yanga/Taifa)

2. Kwa kuwa mechi hii ni bure, hivyo uwanja utafurika wasouth Afrika watupu, basi wizara ingepambana walau jukwaa moja lenye kukidhi mashabiki 5000 liwe reserve kwa ajili ya watanzania tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…