Serikali Kugharamia Mashabiki 55 Kwenda Kutoa Hamasa Africa Kusini

Akili kubwa [emoji1666]
 
55 huku wenzenu wanaujaza uwanja bure?!

Hiyo pesa inayochezewa hapo bora ikatolewe kwenye vituo vya kulelea watoto yatima wapate hata pilau.
Hivi timu km Namungo ina uwezo wa kuujaza Benjamin mkapa kiingilio kikiwa ni Bure?
Mamelodi wenyewe walishindwa kuujaza uwanja walipocheza na Al Ahly pamoja na kutokuwepo na kiingilio sembuse Marumo Gallants?
 

Wakati mnapokea hizo hela za magoli ya mama mbona kusema hela za umma zaenda kuchezewa?
Au zile za magoli ni tofauti na hizi zilitolewa kwa ajili ya mashabiki kwenda kushangilia?

Vyo vyote vile itavyowezekana mpira wa Tanzania utangazwe na faida itaja onekana mbeleni huko
Kuyatafuta mafanikio hakuna njia maalum
 
Yote yatafanyika
 
Hujajibu hoja badala yake umehamisha hoja. Lakini ngoja nikujibu hapa hapa.

Pesa za magoli (za mama Samia) japokuwa zina utata (tukizichambua kiundani sana) lakini at least ziko justifiable&reasonable. Ni pesa kutoka Ikulu (kila mwaka Ikulu inatengewa pesa zake kibajeti kwa matumizi mbali mbali ya kukirimu), ambapo mwenye maamuzi nazo ni rais mwenyewe. Sasa kuliko kuwaleta Ikulu wafungaji na kupiga sherehe, mama anazitoa kwa timu na wachezaji watakwenda kunywa soda!. Kwa kifupi sana zile ni pesa kidogo (tips), ziko wazi, zimenyooka, zinawafikia walengwa kikamilifu na zinaongeza hamasa.

Sasa hizi pesa za kupeleka maafisa 55 wa serikali huko South Afrika kwa kivuli cha mashabiki wa Yanga, zina maslahi gani kwa Yanga?
Bajeti yake inatokea wapi?
 
Yote yatafanyika
Yote yatafanyika wapi na lini wakati wizara iko busy sasa kuwakatia tiketi za ndege na kufanya booking ya hoteli kali huko South Africa maafisa wa wizara kwenda kutalii kwa kivuli cha 'mashabiki' 55 wa Yanga.
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaidia kugharamia usafiri wa mashabiki 55 wa timu ya Yanga kwenda Afrika Kusini katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) huku Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma akitarajia kuongoza msafara huo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Saidi Yakubu ikiwa ni hatua ya kuiunga mkono timu ya Yanga ambao wanatarajia kucheza mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya timu ya Marumo Gallants katika mchezo uliopangwa kuchezwa Mei 17 2023 kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng uliopo mji wa Rustenburg nchini humo.

Bw. Yakubu amesema kuwa Serikali imesaidia safari hiyo kwa kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka Jumapili Mei 14, 2023 na wataungana na Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini ili kuwapa hamasa ya kutosha wachezaji kushinda mchezo huo muhimi kulelekea hatua ya fainali ya mashindano hayo.


"Hii safari Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka kesho Jumapili kueleka Afrika Kusini na huko wataungana na Watanzania waishio Afrika Kusini katika kuhakikisha wanatoa sapoti ya kutosha, nimeongea na Balozi nawao wamejiandaa kuwapokea kwa sababu pia wameanda mabasi kutoka kila mji kuhakikisha Watanzania wanakuwa wengi”


Katibu Mkuu ameongeza kuwa "Katika mechi hizi, lolote linaweza kutokea lakini Serikali pamoja na Yanga kupitia idara tofauti tumejipanga vizuri, Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana anatoa salamu nyingi, pongezi na kuwatakia ushindi katika mchezo wa marudiano. Naibu Waziri Mhe. Hamisi Mwinjuma ataungana na nyinyi kwa upande wa Serikali na anapenda kukaa na mashabiki kushangilia muda wote," alisema Bw. Yakubu.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa timu ya Yanga, Bw. Andrew Ntime amesema kuwa wao kama timu wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo huku akitoa shukrani kwa Serikali kuwa mstari wa mbele wakati wote wa mashindano hayo na kutoa mchango wake wa kupeleka mashabiki hao kwenye mchezo huo wa marudiano.View attachment 2620761View attachment 2620762View attachment 2620763
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…