Serikali kujenga madarasa mapya manne katika kila shule ya Sekondari ya Serikali. Watoto wote 1M kuanza shule Januari 2022

Wewe mtu unanipa raha sana,

Unaeleza vitu mpaka natama Samia atawale milele,

Hongera Rais Wangu,
 
Mkuu pia kwa kuongezea mkapa alijenga madalasa matano kwa kila shule ya msingi Tanzania mzima. Hivyo mama Sio wa kwanza. Nampongeza kwa hatua hii.
 
Jamaa hoi
 
Update ya mwisho ya tozo za miamala ilikuwa inasoma 48B na viponit kadhaa walisema zinaenda kutengeneza vituo vya afya vip vituo vimefikia wapi au tusubiri baada ya mwaka ndio tuulize halafu mwezi huu wa tisa zimekusanywa ngapi maana nadhani ndio zinenda kujenga madarasa kabla ya januari inamaana kuna miezi mitatu kukamilisha madarasa elfu 15 kama vituo vya afya 160 havijafikia hatua ya ukamilishaji vipi tuamini tutaona madarasa elfu 15 kabla ya januari!?
 
Hii Id imeanza mwaka huu baada ya mama wa kambo kuwa rais. Iko maalum kwa ajili ya kumpigia Mama Samia propaganda mfu. Ila kwa bahati mbaya wananchi tumeshajitambua hivyo tunawachora tu.
 
Huyu nahisi atakuwa lizardboy a.k.a Lizaboni na ID mpya.
Hii Id imeanza mwaka huu baada ya mama wa kambo kuwa rais. Iko maalum kwa ajili ya kumpigia Mama Samia propaganda mfu. Ila kwa bahati mbaya wananchi tumeshajitamvubua hivyo tunawachora tu.
 
Haya mapambio yapungue ili afanye kazi
 
Mbona kasema Vijifedha kapata mahali,

Sasa wewe unasemaje tena ni kodi yako,

Nadhani tuendelee Kumuunga mkono Rais anafanya makubwa sana,

Haya ni machache tu kati ya mengi

Vijifedha? Kapata mahali? Wapi? Kwa namna na masharti gani? Aseme vizuri.

Ni mkopo au msaada? Pesa ya nchi si kama ya michezo au vicoba.
 
UPUUZI MTUPU!!!! Alikuwa wapi huyu wa jinsia ya kike kuyajenga madarasa hayo 2016 au 2017 hadi asubiri 2021!?

 

 
Dhana yako ndio sio nzuri

Rais akifanya vizuri tunyamaze?
Uzur upi mzee? At the end of the day ndipo unamsifia mtu kwakua unapomsifia hata hajamaliza robo ya muda wake ndipo mtu hujaa zaid sifa . Ni vzr tukawapa viongoz muda zaid wafanye kazi kwa ajil ya Taifa then mwisho wa cku tutaona ubora wa hizo kaz!!
 
Serikali inaongea maneno mengi lkn ukienda kwenye mashule hakuna kinachoendelea
 
Hii Id imeanza mwaka huu baada ya mama wa kambo kuwa rais. Iko maalum kwa ajili ya kumpigia Mama Samia propaganda mfu. Ila kwa bahati mbaya wananchi tumeshajitamvubua hivyo tunawachora tu.
Tatizo lenu hamna Uzalendo ndio maana mnajadili " ID"

Mlitamani sana mama akosee mseme,

Mambo kwa Upande wenu sio mazuri kabisa,


#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…